Itakusaidia kidogo

Itakusaidia kidogo

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,107
Reaction score
160,001
Kunywa maji ya mtoni pale ambapo Farasi anakunywa. Farasi hawezi kunywa maji machafu.

Weka kitanda chako mahali ambapo paka hupenda kulala.

Kula tunda ambalo limeguswa na mdudu au mnyoo.

Chuma Uyoga ambao wadudu huufata.

Panda mti mahali ambapo Panya wamechimba.

Wakati wa kusafisha kiwanja ikitokea mahali ambapo umemkuta Nyoka basi jenga nyumba yako eneo hilo.

Jenga Kisima mahali ambapo Ndege hujificha kukwepa joto.

Kalale na uamke muda ambao ndege huamka _ Utavuna mbegu adhimu za Dhahabu.

Hakikisha unakula Mboga saba halafu zote za Majani utakuwa na Miguu yenye nguvu, utakwepana na magonjwa ya Moyo, kama wanyama wa msituni.

Ogelea mara kwa mara na utajisikia upo Duniani kama samaki majini.

Tazama mawinguni mara kwa mara na Fikra zako zitakuwa Angavu na Safi.

Kuwa mkimya sana, Ongea kidogo - na Ukimya utakuja moyoni mwako, na Roho yako itatulia na kuwa na Amani.
 
Buji Buji hii Siri umeitoa wapi jamani?
Binadamu wa ckuiz Wana mashauzi Sana utamsikia akisema yeye kamwe hawezi kula chakula kilichosazwa hata awe na njaa kiasi gani.
Sasa kuhusu Hili la kula matunda yaliyodonolewa na ndege/ wadudu sizani Kama watakubaliana nalo.
 
Nyoka lini alikuwa shetani, Na kama nyoka ni shetani jambazi atakuwa nani?
 
Uzi mzuri sana.

Ungeongezea hekima iliyopo katika kila faida uliyotupatia, kama ulivyofanya kwenye aya ya kwanza hapo.
 
Kunywa maji ya mtoni pale ambapo Farasi anakunywa. Farasi hawezi kunywa maji machafu.

Weka kitanda chako mahali ambapo paka hupenda kulala.

Kula tunda ambalo limeguswa na mdudu au mnyoo.

Chuma Uyoga ambao wadudu huufata.

Panda mti mahali ambapo Panya wamechimba.

Wakati wa kusafisha kiwanja ikitokea mahali ambapo umemkuta Nyoka basi jenga nyumba yako eneo hilo.

Jenga Kisima mahali ambapo Ndege hujificha kukwepa joto.

Kalale na uamke muda ambao ndege huamka _ Utavuna mbegu adhimu za Dhahabu.

Hakikisha unakula Mboga saba halafu zote za Majani utakuwa na Miguu yenye nguvu, utakwepana na magonjwa ya Moyo, kama wanyama wa msituni.

Ogelea mara kwa mara na utajisikia upo Duniani kama samaki majini.

Tazama mawinguni mara kwa mara na Fikra zako zitakuwa Angavu na Safi.

Kuwa mkimya sana, Ongea kidogo - na Ukimya utakuja moyoni mwako, na Roho yako itatulia na kuwa na Amani.
Mkuu labda usiishi mjini. Hakika huu ndio utaratibu wa maisha aliotuumbia Mungu. Sema kinadamu amekuwa na mambo mengi mno ambayo yamepelekea siku za kuishi kupungua mno
 
Hiyo nilishambiwaga na Bibi

Ukiona Uyoga uko freshi haujaliwa jua huo ni sumu

Au mti wa matunda polini haujaliwa na ndege jua ni sumu pia.
 
Back
Top Bottom