Itashangaza Dunia kama Waziri wa Afya na Naibu wake hawatafukuzwa kazi ya uwaziri

Sahihi kabisa njia Bora ya kutokomeza huu ugonjwa ni haohao Mabeberu waliouleta waamue usiwepo ila ni ngumu kuisha kwa kuvaa barakoa na kujifungia ndani tumuunge mkono muheshimiwa Rais yupo sahihi.
 
Sahihi kabisa njia Bora ya kutokomeza huu ugonjwa ni haohao Mabeberu waliouleta waamue usiwepo ila ni ngumu kuisha kwa kuvaa barakoa na kujifungia ndani tumuunge mkono muheshimiwa Rais yupo sahihi.
Kwahiyo unashauri tujifukizie?[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kweli kabisa ifike mahali tuwe tunashtaki watu kwa uzembe wao pale wanaposababisha vifo kwakuzembea utaalamu na kuficha taarifa sahihi.
Marne hii tuongozane kiukweli na kisomi sio kama enzi za kinjekitile. Daktari mzima umesoma na kodi zetu unakaa na mwanasheria tuliosomesha mnatuelekeza kujifusha itaponesha corona kweli?? Dunia nzima wasijifushe wapone nisisi tuu? Kuna uthibitisho gani wa kitaalamu kuwa kujifusha kunaponesha?? Tusileteane maujinga tafadhali
 
Kwahiyo unashauri tujifukizie?[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Ndio tujifukize pamoja na kula matunda na dawa za asili zenye kuongeza kinga za mwili au zinazotibu matatizo kama hayo ya upumuaji sababu Corona haina dawa bado ukikataa dawa za asili utatumia nini kama Tiba?
 
Kwani mkuu kuna dawa yoyote inayoponesha?
 
punguzen matumiz ya air coditiona kwene magar na oficin tegenezen mfumo wa mwili kupata joto
 
Nini kimekupata boss...Usibishane na Rais...nchi ipo salama achana propaganda za mabeberu
 
We Ndungulile, hebu muogope Mungu! Ndio maana ulikuwa umelitoa jicho kuhesabu kura za Makonda!
Aliyekudanganya kuwa kujifukiza hakuna faida ktk kupambana na corona ni nani! Na ana mamlaka gani kwenye tasnia ya sayansi! Hebu acha donge hilo ndugu, lile! Hawa mawaziri wa afya wapo poa sana, hawakurupuki wala kushupalia wazungu wanasema nini! Tunatumia vyetu vilivyodharauliwa kuviaibisha vyao!
Hebu jaribu basi hata kujisomea tafiti mbalimbali juu ya 'steam treament' ili uondoe huo ujinga!
 
Hakuna Mbunge wa kuja na hoja ya kura ya kutokuwa na imani na Rais, wabunge wote naamini kabisa wamepata Ubunge kwa HISANI na NGUVU ya wizi ya Rais + wale COVID19.

Katika Taifa lenye misingi ya demokrasia na kujitambua, JPM hakupaswa kuwa madarakani hadi muda huu.
 
Hii kasi mpya ya Corona ni majibu ya vilio vya walioumizwa na wizi wa kura na ubabe wa kuufuta upinzani kwa mabavu ya vyombo vya dola.
 
Alie toa ushauri wa kitaalamu alifukuzwa kazi, waliopo wameji-tune, wanaenda na mtimizie kafiri upate mradi wako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…