Itashangaza Dunia kama Waziri wa Afya na Naibu wake hawatafukuzwa kazi ya uwaziri

Itashangaza Dunia kama Waziri wa Afya na Naibu wake hawatafukuzwa kazi ya uwaziri

Kumshahuri pombe inahitaji ujasiri wa kujitoa mhanga kama Ndugulile alivyo ambulia kutumbuliwa. Ila uzuri wa pombe baada ya maamuzi uwa anafanya pondering na akigundua kuna kasoro hubadiri gia na kumchukua mtu yule yule kwa kazi zaidi. Hiyo tu ndio uwa naikubali kutoka kwa pombe. Kukosea kupo na hasa ukiwa na madaraka makubwa, ni vizuri kupitia maamuzi yako nyuma ya pazia na kujikosoa inapobidi.
 
Hivi nyungu inasaidia? Kama haisaidii waziri wa Afya na wizara yake wawe held accountable for misleading the nation, then waweke proper guidelines za kufuata kama nchi nyingine.
Kwani hiyo ya kutumia nyungu ililetwa kwa wananchi na mawaziri husika?
 
Wana Jf kwa jinsi tulivyo katika kipindi kigumu ambacho kimezua hofu kwa kila mtu ni wazi kuwa Waziri wa afya na naibu wake hawastahili kuwepo kwenye hii nafasi mpaka sasa.

Mwaka jana bila kupepesa macho Dk Faustine Ndugulile alieleza ukweli umma wa Watanzania kuwa kujifukisha hakuwezi kuua wadudu wa Covid 19, hii ni sababu hawa virus wakiingia kwa binadamu huingia moja kwa moja kwenye mfumo wa kupumua( mapafu) hivyo hata ukijifukiza ni ngumu kuwaua huko ndani ya mapafu.

Mwaka huu baada ya dalili kuwa hili janga limerudi Tanzania kwa namna nyingine,maana inadaiwa sasa hivi kirusi cha korona kimejibadili. Tumeshuhudia madaktari wawili ambao wanasimamia wizara ya afya wakisisitiza watu kujifukiza. Je hawa watu kwa nini hawakutoa ushauri wa kitaalamu unaozingatia taaluma yao kama Faustine Ndugulile?

Leo hii toka watoe demostrantion namna ya kujifukiza hali inaonekana kuwa mbaya. Maana vifo vya vigogo mpaka makabwela vinazidi kupamba moto. Na tatizo ni hilo la kukosa uwezo wa kupumua.

Karne ya ishirini na moja kuongozwa na wasomi ambao hawezi kusimamia taaluma yao na kumshauri rais namna ya kukabiliana na magonjwa kisayansi ni aibu kubwa. Mawaziri hawa wawili wasisubiri vifo vya watanzania iwe sababu ya wao kujiuzulu.
Kuamini kua wizara ya afya wanafanya wanayo fanya bila ruhusa ya alfa na omega wa tanganyika, ni matumizi mabaya ya akili.
 
Kwa nini wasimshauri kitalaam? Maana ni madaktari.
Ndungulile alipo shauri nini kilimtokea?
Wewe mwenyewe ulikuwa unakenua meno kipindi viongozi wenu wakituaminisha kuwa Tanzania ipo salama kisa tunapiga nyungu na maombi.

Leo hii unakurupuka kuwaangushia lawama wataalam masikini wasiyo na maamuzi yoyote zaidi ya kutumikia matumbo yao.
 
Achana na watu wanaohangaikia ugali wao hawajali afya za wengine. Uzuri Kovidi haichagui cheo wala rangi inakwenda tu.
Tuachane nao?...kwa nn wamekubali dhamana waliyopewa?,...eti tuachane nao,au wao ndo waachie nafasi zao
 
Hukuiona ile picha Waziri na mumewe wakipiga nyunguziiii halafu mazoezi....
Hao wameingia juzi,kesi yenyewe ilianza mwaka jana wakati tuna aminishwa kuwa tunafanya maombi ili kuidhibiti korona.

Tukaaminishwa kuwa nyungu ndiyo kila kitu
 
Unasema??
IMG-20210218-WA0008.jpg
View attachment 1705303
 
Back
Top Bottom