Hapana. Unachokisema siyo sahihi.
Anayekosea anastahili kuambiwa hata kwa lugha kali. Hubembelezwi ukikosewa.
Biblia inasema unapotakiwa kuonya, onya hata kwa ukali.
Kiongozi siyo malaika, anaweza kukosea, anaweza kuwa mwovu kupindukia kuwazidi hata majambazi. Ndiyo maana kuna viongozi wanaondolewa kwenye madaraka bila staha, wanashitakiwa, na kuna wengine wanahukumiwa hata kunyongwa hadi kufa.
Hivyo, tunatakiwa kuangalia kauli na vitendo vya Rais ili kutambua tuna kiongozi wa namna gani, na kisha kumpongeza, kumuonya, kumkosoa au hata kumfukuza kwenye uongozi kwa njia yoyote yenye tija kwa nchi.