SI KWELI ITV wamechapisha taarifa Lissu amesema, "safari yetu imejaa mashaka, hatuaminiani ndani ya chama chetu"

SI KWELI ITV wamechapisha taarifa Lissu amesema, "safari yetu imejaa mashaka, hatuaminiani ndani ya chama chetu"

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
katika pitapita zangu katika mtandao wa X nimekutana na chapisho hili kumhusu Tundu Lissu

Wakuu uhalisia wa chapisho hili ni upi?
Lisu ITV.jpg
 
Tunachokijua
Tundu Lissu ni makamu mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA ambaye pia kitaaluma ni mwanasheria ambapo mwaka 2017 Alikuwa Rais wa chama cha wanasheria Tanzania (TLS) kwa miezi mitano kabla ya kushambuliwa kwa risasi akiwa mkosoaji mkubwa wa serikali katika awamu ya tano ya urais wa Tanzania. Mwaka 2010 mpaka 2020 alikuwa ni mwakilishi wa wananchi Bungeni wa jimbo la Singida Mashariki.

Mara kadha wapotoshaji wamekuwa wakitumia kauli za Lissu kupotosha uhalisia wa yale yanayosemwa na Lissu juu ya masuala mbalimbali hasa katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa Novemba 27, 2024. Unaweza kurejea hapa, hapa na hapa.

Kumekuwapo na chapisho linalodaiwa kuwa limetolewa na ITV ambalo linadai Tundu Lissu alisema "safari yetu imejaa mashaka, hatuaminiani ndani ya chama chetu"
Chapisho hilo limehifadhiwa hapa.

Ni upi uhalisia wa chapisho hilo linalodaiwa kuwa la ITV?

Ufuatiliaji uliofanywa na JamiiCheck umebaini kuwa Chapisho hilo si la kweli na halijatolewa na ITV. Kadhalika picha ya Lissu iliyotumika imetokana na mkutano na waandishi wa habari ambao aliufanya mnamo Novemba 12, 2024 mkoani Singida ambapo hakusema "safari yetu imejaa mashaka, hatuaminiani ndani ya chama chetu"

Aidha JamiiCheck imebaini mapungufu kadhaa katika chapisho hilo lisilo la kweli, ukilinganisha na machapisho rasmi yanayotolewa na ITV, moja kati ya mapungufu hayo ni kutofauntiana kwa mwandiko (fonts) uliotumika kuandika kichwa cha habari si ule ambao hutumiwa na ITV, pia sehemu ya nyuma ya maandishi ya kichwa cha habari haifanani na machapisho rasmi ya ITV ambapo sehemu hiyo kwa mbali inaonesha picha iliyofifia, tazama mfano wa chapisho rasmi la ITV hapa

Hivyo chapisho hilo halina ukweli wowote bali linatumika na wapotoshaji kupotosha umma.​
Back
Top Bottom