SI KWELI Iwapo tunda la nyanya linaonesha dalili kama hizi, linaweza kuwa na sumu kwa kung'atwa na nyoka

SI KWELI Iwapo tunda la nyanya linaonesha dalili kama hizi, linaweza kuwa na sumu kwa kung'atwa na nyoka

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Katika pita pita zangu, nimekutana na maada inayosema kwamba matunda kama nyanya yanaweza kushambuliwa na popo, au nyoka. Hivyo basi Ukiona nyanya ikiwa hivi(pichani) usipende kula mbichi au kuitumia kabisa kwa sababu Kuna wakati inakuwa imezuliwa na Nyoka, Popo au aina ya wanyama fulani wenye sumu kali inayoweza kudhuru afya yako.

1732784921759.jpg
1732784927609.jpg
1732784932980.jpg

Tunachokijua
Nyoka ni reptilia watambaao wasio na miguu. Kuna takriban spishi 3,000 duniani: wako kwenye mabara yote nje ya Antaktiki na Aktiki.
Morelia-Amethistina.jpg

Kama reptilia wote wana damu baridi na ngozi ya magamba. Wote ni wala nyama na spishi mbalimbali hutumia sumu kwa kuwinda lakini nyoka walio wengi hawana sumu wanashika windo kwa miili yao au kwa mdomo tu.

Nyanyani aina ya tunda linalolimwa sana ulimwenguni na hutumika kama mboga au kiungo kwenye mapishi mbalimbali. Nyanya ni tunda la mmea wa kisayansi unaoitwa Solanum lycopersicum, ambalo ni sehemu ya familia ya mimea inayojulikana kama Solanaceae au nightshade. Familia hii pia inajumuisha mimea mingine maarufu kama viazi, pilipili, biringanya, na tumbaku. licha ya ladha yake tamu au kidogo ya uchachu, nyanya ni chanzo kizuri cha vitamini C, vitamini A, na antioxidants.
Tomatoes.jpg

Kumekuwa na picha inayosambaa mitandaoni ikimuonesha nyoka kang'ata nyanya huku ikiambatana na ujumbe unaodai kuwa Watu wakiona nyanya iliyotoboka(yenye vishimo) wasile nyanya hiyo kwani inaweza kuwa iling'atwa na nyoka na kuachiwa sumu na ivyo watu wakila watadhurika kwa sumu ya nyoka. Tazama hapa, hapa, hapa, hapa, hapa, hapa, hapa, hapa, hapa na hapa

Je, uhalisia ni upi?

JamiiCheck imefatilia Madai ya nyoka kula nyanya na kubaini kuwa Madai hayo Si ya Kweli kwani nyoka hawali mimea(majani) wala matunda kama nyanya au aina nyingine za matunda. Nyoka ni aina ya viumbe walao nyama (carnivores), chakula chao huwa ni wanyama wadogo kama panya, ndege, mijusi, mayai au hata nyoka wengine, kulingana na spishi.

Aidha, madai hayo yameeleza kuwa nyanya iliyoliwa na nyoka huacha sumu inayoweza kumdhuru Mwanadamu iwapo akila nyanya hiyo, Sumu ya nyoka huwa na madhara pale inapoingia kwenye mfumo wa damu, eidha kwa kung’atwa na nyoka au kupitia kwenye michubuko ya mwilini.

Sumu ya nyoka kwa kawaida haiwezi kudhuru mwili inapopitia kwenye mfumo wa mmeng'enyo wa chakula kwa sababu inaharibiwa na asidi ya tumbo na vimeng’enya vya mmeng'enyo wa chakula(enzymes). Hata hivyo, haishauriwi kunywa au kula sumu ya nyoka kwasababu iwapo kuna vidonda au michubuko kinywani, kooni, au tumboni, sumu inaweza kupenya kwenye mfumo wa damu, na hapo ndipo inaweza kuwa na madhara.

Vile vile inategemea na aina ya Sumu ya nyoka kwani baadhi huathiri damu (hemotoxic) na nyingine huathiri mfumo wa neva (neurotoxic). Hata hivyo, sumu hizi huwa na madhara makubwa zaidi zinapoingia moja kwa moja kwenye damu kupitia kuumwa na nyoka. Hii ni kwa sababu sumu ya nyoka inaundwa kwa protini, ambazo huvunjwa kama protini nyingine yoyote katika tumbo. Hivyo basi madai ya sumu ya nyoka inayoachwa kwenye nyanya kuweza kudhuru binadamu atakayekula yanakosa nguvu kutokana na hoja hii.

Upi uhalisia wa Picha inayoonekana nyoka kang’ata nyanya? Ni picha halisi?

Jamiicheck imefatilia picha inayoonekana nyoka kang’ata nyanya na kubaini kuwa ni picha ni halisi na haijatengezwa.

Mnamo Septemba 20, 2024 ilipostiwa Video kwenye mtandao wa Instagram, video hiyo ilimuonesha Nyoka aking'ata nyanya. Video hiyo ilikuwa chanzo cha Madai ya nyoka kula Nyanya bila kutazama kwa nini nyoka alinng'ata nyanya, kitu ambacho kilisababisha Mwanzo wa Taarifa hii Potofu. (Fungua hapa kutazama Video hio)

Ukitazama video hiyo utaona nyoka huyo alikuwa amegandamizwa na ubao kwenye mwili wake hali iliyomfanya ashambulie nyanya zilizokuwa mbele yake sababu ya maumivu ya kugandamizwa na ubao na si kwa sababu yeye anakula nyanya au amedhamiria kutoboa nyanya.

Baada ya Video hiyo, Septemba 22, 2024 lilifanyika Jaribio la kuonesha kwa nini nyoka huyo alishambulia nyanya.

Kupitia Mtandao wa Youtube, Kwenye akaunti ya Jamal Al-Imwase alipost video ya jaribio la Nyoka aliyewekewa Nyanya mbele na kisha kugandamizwa ili kuona nini kitatokea, matokeo yalikuwa ni nyoka kuishambulia nyanya kama ilivyotokea kwenye video ya nyoka wa kwanza na kubainisha uhalisia kuwa Nyoka hali nyanya isipokuwa aling'ata nyanya kama sehemu ya kujilinda baada ya kugandamizwa na kuhisi maumivu. (Fungua kutazama video hiyo)

Aidha, Picha inayoonekana hapo Juu, ikimuonesha nyoka kang'ata nyanya kama ilivyowasilishwa na Mtoa mada ni Picha kutoka kwenye video hiyo ya jaribio ambalo lilifanyika ili kukanusha upotoshaji wa video ya awali kama ilivyoelezewa hapo juu.

Ambapo wapotoshaji walichukua Picha kutoka kwenye video hiyo na kuanza kusambaza tena upotoshaji kuwa Nyoka hung'ata nyanya na kucha sumu inayoweza kudhuru mtu akila kitu ambacho Si kweli. Aidha, Matundu kwenye nyanya husababishwa na wadudu, minyoo na magonjwa baadhi ya nyanya.

1732958829483-png.3165692

1732958842808-png.3165693

1732958803258-png.3165690

Uhalisia ni upi kuhusu Popo kula nyanya?
Popo ni wanyama aina ya mamalia ambao hutoka kwenye familia ya Pteropodidae ambapo chakula chao ni matunda, hasa yale yenye asili ya utamu kama vile mapera, nk. Kwa kawaida Popo hawawezi kula nyanya kwa sababu sio aina ya matunda ambayo popo hula.
1732961926658-png.3165730
Popo wanapenda matunda yenye juisi nyingi na ladha tamu, kwa hivyo nyanya sio miongoni mwa chakula chao cha kawaida.
Last edited:
Kwa uelewa wangu mdogo..kuhusu hilinyoka ni hapana....
Nyoka hutumia sumu yake katika madhumuni makuu mawili,1..kuwinda na 2.ni kumdhuru adui....
Sasa hili la nyanya ni ukakasi kwa sababu...nyoka pia sio vegetarian.
Nimekupata mkuu... 👍
 
SIYO KWELI. Kwa muonekano wa tunda no2 tyr limeshapona na halina shida kabisa.Nyoka hawezi tumia sumu yake ovyo ovyo tu mwenye tabia hiyo ni swila pekee lkn huyo kifutu hadi umkanyage ama umchokoze na hutoa sumu kwa kujihami tu pia kwa sumu ya nyoka tunda lazima liharike papo hapo!
Hapa umeshindwa, kutuelewesha sisi tunao soma coment.
Kwanza mimi nilivyoelewa hiyo picha ya nyoka imetumika kama mfano, maana siyo lazima awe aina hiyo.
Ila kwakua unaamini swila anaweza kuigonga nyanya, basi kuna haja ya kutilia shaka nyanya za namna hiyo, maana isije kuwa imetobolewa na swila.
 
Ukinywa sumu ya nyoka haufi labda uwe na vidonda mdomoni au tumboni kwasababa sumu ya nyoka ni venom na sio poison
Ni sawa ukinywa mtori haufi ila tukichukua mtori tukauweka direct kwenye blood stream hauchukui sekunde
 
Sumu ya nyoka ikishaingia kwenye tunda hilo tunda lazima liharibike mkuu. haliwezi kubaki kama lilivyo na hadi kupona
Hapo hata waje na majibu vipi ni ngumu kuwa elewa. mfano koboko akikung'ata muda sio mrefu utakufa na kuanza kuharibika haraka. vilevile aking'ata hata lile bapa la mkonge{katani} hukauka ama kunyauka kwa muda ule ule.

Kwa maelezo mengine naweza kusema kwamba hiyo picha kwa sisi wakulima huwa ni funza fln {caterpilar} huwa wanaingia kwenye tunda ukiwahi kumthibiti kwa sumu atakufa na tunda litapona na kuonyesha hali hiyo mkuu
 
Sumu ya nyoka au nge au tandu (venom) ina madhara ikiingizwa kwenye mfumo wa damu. Vinginevyo, haina madhara.
 
Bila shida yoyote. Nyoka vile anavyotembea tu na kula Hana sumu. Hata Maji akiyanywa kwenye chombo chako wewe kunywa tu. Ndivyo tulivyoishi siku zote maisha ya Kitanzania kwa ambao hatujazaliwa magorofani. Nyoka sumu yake anaitoa kwa kazi maalumu tu kama vile kujihami au wakati wa mawindo yake magumu tu inayomlazimu kutumika sumu yake Ili kushinda.

Vile anaringa wakati anatembea anaweza kukupiga denda mdomoni bila shida yoyote.

Pia kumbuka siyo nyoka wote Wana sumu.
Inategemea na aina nyoka, kuna baadhi wana sumu kali wakikatiza juu ya kitu ukashika kuna namna unadhurika.
 
SIYO KWELI. Kwa muonekano wa tunda no2 tyr limeshapona na halina shida kabisa.Nyoka hawezi tumia sumu yake ovyo ovyo tu mwenye tabia hiyo ni swila pekee lkn huyo kifutu hadi umkanyage ama umchokoze na hutoa sumu kwa kujihami tu pia kwa sumu ya nyoka tunda lazima liharike papo hapo!
Kimtazamo huwa nafikiria kuwa meno ya nyoka ndo yana sumu, kumbe ipo ndani ya mwili wake... Au hii imekaaje mkuu??
 
Ukinywa sumu ya nyoka haufi labda uwe na vidonda mdomoni au tumboni kwasababa sumu ya nyoka ni venom na sio poison
Ni sawa ukinywa mtori haufi ila tukichukua mtori tukauweka direct kwenye blood stream hauchukui sekunde
Duh hapo kwenye mtori sasa ni mpya hii.. Kwamba mtori unaweza kusababisha blood clot??
 
Kimtazamo huwa nafikiria kuwa meno ya nyoka ndo yana sumu, kumbe ipo ndani ya mwili wake... Au hii imekaaje mkuu??
Sumu haipo kwenye meno. Sijui inakuwaje hapo lkn Sumu Huwa ni option ya mwisho kabisa ya kujirinda ama kuwinda. Haitumii ovyo tu. Ndio maana ukutanapo na nyoka lazima atajitahidi akimbie iwapo ataona Bado una mfuata basi lazima ajihami kutumia siraha yake hiyo kama swila atatema mate kwanza Ili usione akimbie au vyote viwili
 
Umeeleweka mkuu 👍👍👍
 
Kazi kuu ya jamiicheck ni kupembua maada tatanishi au zile zinazosambaza taarifa za uongo ili kuhakikisha kuwa taarifa au jambo limetolewa majibu kwa ufasaha , sasa nashangaa kwa nini hii thread imefutwa " katika pita pita zangu, nimekutana na maada inayosema kwamba matunda kama nyanya (pichani) yanaweza kushambuliwa na popo, au yoka, endapo binadamu atalitumia likiwa mbichi, afya yake inaweza kuathirika na sumu ya viumbe hao"

Sasa najiuliza:-
1. Je mmekosa majibu sahihi ya swali hili ??

2. Au moderator umeamua tu kufuta hii thread bila sababu maalum ??

3. Na je Kama majibu yamekosekana kwa nini msiache hii thread kama NADHARIA??
 
Wamefuta sababu wenyewe wamechoka kutafuta majibu au wamekutana na majibu wasiyokubariana nayo
 
Kazi kuu ya jamiicheck ni kupembua maada tatanishi au zile zinazosambaza taarifa za uongo ili kuhakikisha kuwa taarifa au jambo limetolewa majibu kwa ufasaha , sasa nashangaa kwa nini hii thread imefutwa " katika pita pita zangu, nimekutana na maada inayosema kwamba matunda kama nyanya (pichani) yanaweza kushambuliwa na popo, au yoka, endapo binadamu atalitumia likiwa mbichi, afya yake inaweza kuathirika na sumu ya viumbe hao"

Sasa najiuliza:-
1. Je mmekosa majibu sahihi ya swali hili ??

2. Au moderator umeamua tu kufuta hii thread bila sababu maalum ??

3. Na je Kama majibu yamekosekana kwa nini msiache hii thread kama NADHARIA??
Habari Nyafwili,

Mada hii inafanyiwa kazi, utapatiwa majibu hivi punde.
 
Back
Top Bottom