MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
Hii ninashauri ili kupunguza tatizo la ajira na pia kusaidia kupunguza migogoro kati ya serikali na wafanyabiashara. Kuna kutokuelewana pakubwa kati ya serikali na wafanyabiashara kwenye hesabu zao. Mamlaka zinaona wafanyabiashara wanakwepa kodi huku nao wakiona mamlaka wanawaonea. Kupunguza tatizo kila mfanyabiashara awe na kijana mwenye elimu ya uhasibu atakayeweza kuondoa utata wa hapa na pale. Mfanyabiashara mwenye turnover ya zaidi ya 400m hashindwi kuajiri kijana akamlipa 400k kila mwezi ili mahesabu yake yakae sawa.
Natumaini huu uzi utafanyiwa kazi na mamlaka husika haraka iwezekanavyo.
Natumaini huu uzi utafanyiwa kazi na mamlaka husika haraka iwezekanavyo.