Jacqueline Mengi aendelea kudondokea pua rufaa, mahakama yaondoa maombi yake ya kutaka kuurudisha wosia

Jacqueline Mengi aendelea kudondokea pua rufaa, mahakama yaondoa maombi yake ya kutaka kuurudisha wosia

Kuna wanawake na majini, Ingawa mi ni mwanamke but I can't do that kwa visivyo halali yangu.. dada mbona mrembo tu.. angekomaa tu walau apate hata tumilioni milioni tu jamani na wale watoto.

Au ndo anataka awe first woman billionaire in Tanzania?!! Daaah

Alafu bado kijana, atafute bilionea lingine alikwide walahi[emoji23]
 
1. Hivi wanaume kwanini mnaendaga kuoa vibinti teke mkiwa kwenye seventies huko? Mnadhani kabisa wanawapenda? Yani watoto wako ambao wamesota na wewe mmeinuka wote wanakuja kugombea mali na kimwanamke ambacho hata hakijui bei ya glass hapo nyumbani ni sh ngapi?

2. Jacky anajikuta nani kudai mali kibabe hivyo? Shame on her. Mashume wenzie wanatetea eti ooh ni mke. Mke my foot. Ndo utake wingi wa mali hivyo? Wewe kama nani? Jacky doesn’t deserve hivyo. Bora afanyiwe child support ya mwezi na ada aende. Hakuna cha kampuni wala nini. Kampuni alianzisha nae?


I hate gold diggers
Kama Hela ipo unatakiwa utafute kabinti kadogo ambako bado inabana ili ukumbushie enzi za ujana.Mambo ya Jacky mwachieni Jacky na kwakuwa sheria na mahakama vipo kila upande utapata haki yake.Wanawake msitupangie sisi waume zenu tumuoe nani na tuoe wangapi.Acha tuoshe rungu kwenye tushimo mabwawa yanachosha.
 
Huyu dada tamaa ya pesa itamfanya apoteze uhai. Amuulize yule mama aliyefariki juzi na wanae kwenye ajali ya gari.Infwakti Yule mama Immaculata Byemerwa kabla ya kuolewa na Engneer alikuwa na yuho mwanae Albert ambae ndo alikuwa dereva. Kaolewa kazaa Janet na Jolister.Na kumbuka kwamba alimkuta Josepahat ana watoto wakubwa .Sasa yule mama kapata ajali na kafariki na uzao wake wote. Kaacha watoto wa mzee wafaidi vizuri mali za baba na mama yao mzazi.
Jack acha tamaa.
Aiseee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mengi mara baada ya uchaguzi wa 2015, ule mwaka wa 2016 aliugua sana na hata uwezo wake kiakili ulipungua. Mengi alikuwa siyo mtu wa kujirekodi clip za video na kurusha kwenye mitandao eti akijiapiza kuwa anampenda sana huyo mwanamke.
Kwani mkuu ulikuwa unamjua kiundani kabisa ?
 
Mkuu uzuri watoto watakuwa watu wazima watajiunga na ndugu zao. Hao watoto kwa wachagga hawataachwa na urithi watapewa kabisa maana hata shule walikuwa wanasomeshwa vizuri? Alipotaka kwenda kuishi Dubai kwa lile Danga lake ndiyo akaleta bill ya Ada ya kutupwa na familia Ika stop ushenzi huo. Yaani kukekule alikofia Baba yao na kulekule ambako walimkuta hayuko na mgonjwa!!!! Ndiko huko alipanga kupeleka watoto na yeye kuishi huko.
Sawa watoto watajiunga na ndugu zao, je yeye muda aliokaa naye huyo babu utarudi? Hivi kuolewa na mzee unazani ni kazi ndogo? Basi ndugu zake wangemzuia asioe akae tu mwenyewe, hata Jack asiolewa na huyo mzee angekuwa na maisha mengine, msimfanyie hivyo jamani
 
Alijitoa mwili wake utumike kwa manufaa ya baadae lazima uwe na master plan km wewe ni mwanamke mwenye akili, Jana niliwaeleza watu kua ukiona mtu anamtafuta mtu wa kuanzisha nae mahusiano ujue yupo kwenye mission maalum ila wapo waliopuuza, Jack kuingia kwenye mahusiano na babu Mengi ilikua ni special mission
Wanawake wa kinywanda, Nigeria, Kenya ni hatari sana kwenye pesa
 
Muwe mnashauriana jamani. Ni mateso kwa wake zenu na watoto wanaobaki. Na unakuta mzee amezaa nje kama fungo. Yani kila Kijiji ana mtoto na hivyo sheria imetoka kwamba hata watoto wa michepuko wana haki. Yaani nyumba ya mzee itapigwa bei wagawane watoto wote. Ni mateso
Mateso vipi wakati nawaachia nyumba wanagawana? Kama vipi nao watafute vyao kwani hata Mimi nilikuwa na baba.
 

Jumamosi, Desemba 3 , 2022

Muhtasari:

Mjane wa aliyekuwa mfanyabiashara maarufu nchini, Reginald Mengi, Jacquiline Ntuyabaliwe na wanawe, wamekwama kutetea wosia ulioachwa na marehemu baada ya Mahakama ya Rufani kutupa shauri lake la kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu.


Dar es Salaam. Mjane wa aliyekuwa mfanyabiashara maarufu nchini, Reginald Mengi, Jacquiline Ntuyabaliwe na wanawe, wamekwama kutetea wosia ulioachwa na marehemu baada ya Mahakama ya Rufani kutupa shauri lake la kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu.

Jacquiline alifungua shauri mahakamani hapo la mapitio kufuatia hukumu ya Mahakama Kuu, iliyokataa wosia uliodaiwa kuachwa na Mengi.
Shauri hilo la mirathi namba 39 ya mwaka 2019, lilifunguliwa na watu wanne, wakiwemo ndugu wa marehemu Mengi.

Mahakama hiyo katika uamuzi wake uliotolewa juzi na jopo la majaji watatu, Rehema Mkuye (kiongozi), Dk Paul Kihwelu na Panterine Kente lilitupa shauri hilo kutokana na kasoro mbili zilizoonekana kwenye kiapo cha Jacquiline na cha wakili wake, Audax Kahendaguza vilivyoambatanishwa katika maombi hayo.

Kasoro hizo ambazo mahakama imekubaliana nazo ni viapo kuwa na maelezo yasiyopaswa kuwemo kwa hoja zinazohitaji ushahidi, maoni, mapendekezo na hitimisho na nyingine ni kutokubainisha chanzo cha taarifa ziliozokuwemo kwenye viapo hivyo.

Mahakama hiyo ilifikia uamuzi huo kutokana na pingamizi la awali lililowekwa na wasimamizi wa mirathi hiyo walioteuliwa na Mahakama Kuu ambao ni Abdiel Reginald Mengi akishirikiana na mdogo wake marehemu Mengi, Benjamin Abrahamu Mengi, kupitia kwa mawakili wao, Michael Ngalo na Roman Masumbuko.

Katika uamuzi huo, mahakama imesema kiapo kinapokuwa na kasoro kama hizo, aya zenye kasoro huondolewa kwenye kiapo na kuendelea na aya nyingine zisizo na kasoro.
Hata hivyo, imesema aya zenye kasoro ndizo msingi wa shauri hilo na kwamba, baada ya kuziondoa zinazobaki haziwezi kusimama zenyewe.
“Kasoro hizo zinayafanya maombi haya kutoweza kusimama, hivyo tunayatupilia mbali. Kwa kuwa shauri linatokana na mirathi hatutoi amri yoyote kuhusu gharama,” imesema mahakama hiyo katika uamuzi huo.

Awali, watu wanne, Benson Benjamini Mengi, William Onesmo Mushi, Zoebu Hassuji na Sylvia Novatus Mushi walifungua shauri la msingi la mirathi Mahakama Kuu wakiomba kuteuliwa kuwa wasimamizi wa mirathi hiyo, kwa mujibu wa wosia ulioachwa na Mengi.
Hata hivyo, Abdiel na Benjamini waliweka pingamizi dhidi ya wosia huo unaompa Jacquiline na wanawe haki ya urithi wa mali za Mengi, wakipinga uhalali wake huku wakiwasilisha jumla ya sababu nne za kuupinga.
Mahakama Kuu baada ya kusikiliza hoja za pande zote ilikubaliana na hoja za pingamizi dhidi ya wosia huo na kuikataa kuwa ni batili.

Jaji Yose Mlyambina alikubaliana na sababu hizo za pingamizi huku akisema unawanyima urithi wanawe wengine (wakubwa, Abdiel na ndugu yake) bila kutoa sababu.

Pia Jaji Mlyambina katika hukumu yake hiyo ya Machi 18, 2021, aliukataa wosia huo akieleza kuwa ziliiingizwa mali za mke wake mkubwa na kwamba nakala yake alikuwa nayo mwenyewe Jacguiline Mengi ambaye alikuwa mnufaika.
Hivyo Jaji Mlyambina aliwateua Abdiel na Benjamini kuwa wasimamizi wa mirathi na akaelekeza mali za marehemu zigawiwe warithi wanaostahili kwa utaratibu wa kawaida kama wa mtu ambaye hakuacha wosia.

Mwananchi
 
Back
Top Bottom