Jacqueline Mengi aendelea kudondokea pua rufaa, mahakama yaondoa maombi yake ya kutaka kuurudisha wosia

Jacqueline Mengi aendelea kudondokea pua rufaa, mahakama yaondoa maombi yake ya kutaka kuurudisha wosia

Sawa.nielimishe sasa.familia ya mengi inamkwepa vipi jack.na ukimbuke kuwa jack kaolewa na ndoa ya kanisani na hawakuachana na watoto wamezaa na mengi.
Familia ya Mengi Wala haikwepi Jack ila tatizo Jack anataka kuchukua Mali kuliko familia ya mengi isitoshe Mali pia ya mama yao marehemu ndio chanzo utajiri wote

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
 
Dunia ya ajabu sana yaani marehemu kasahaulika watu wanagombana huku.
Ndio maana tunaambiwa tumtumikie Mungu na sio mali, utadhulumu watu, utauwa watu, utaibia watu ili tu upate hizo mali lakini siku ukifa unaacha kila kitu, na sio mali tu unaacha mpaka nguo zako za kuvaa unaondoka uchi kama ulivyokuja.
Nawaza tu-Malori ya mafuta 200, nyumba 80, mabasi 50, hoteli za five star 30, gari za kifahari hapa sizungumzii vi IST nazungumzia gari za kuanzia Milioni 100 unakuwa nazo 20, lakini siku ukizimika tu vinakuwa sio vyako tena watu wanajibebea...
 
Family ya mengi Wala haikwepi jack ila tatizo jack anataka kuchukua Mali kuliko family ya mengi isitoche Mali pia ya mama yao marehemu ndio chanzo utajiri wote

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
Mbona inasemekana huyo Mama marehemu waligawana kabla kila mtu akabaki na chake? Huyo Jack mkumbuke alimpa mzee raha mpaka akasahau uzee wake, kwani yeye hakuwaona wazee wenzie mpaka kumuoa msanii wetu Jack?
 
Kama Hela ipo unatakiwa utafute kabinti kadogo ambako bado inabana ili ukumbushie enzi za ujana.Mambo ya Jacky mwachieni Jacky na kwakuwa sheria na mahakama vipo kila upande utapata haki yake.Wanawake msitupangie sisi waume zenu tumuoe nani na tuoe wangapi.Acha tuoshe rungu kwenye tushimo mabwawa yanachosha.
Ebooo! Ndo maana mnakufa mapema maana wanafuata mali wakiona unachelewa kufa wanawaua.
 

Jumamosi, Desemba 3 , 2022

Muhtasari:

Mjane wa aliyekuwa mfanyabiashara maarufu nchini, Reginald Mengi, Jacquiline Ntuyabaliwe na wanawe, wamekwama kutetea wosia ulioachwa na marehemu baada ya Mahakama ya Rufani kutupa shauri lake la kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu.


Dar es Salaam. Mjane wa aliyekuwa mfanyabiashara maarufu nchini, Reginald Mengi, Jacquiline Ntuyabaliwe na wanawe, wamekwama kutetea wosia ulioachwa na marehemu baada ya Mahakama ya Rufani kutupa shauri lake la kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu.

Jacquiline alifungua shauri mahakamani hapo la mapitio kufuatia hukumu ya Mahakama Kuu, iliyokataa wosia uliodaiwa kuachwa na Mengi.
Shauri hilo la mirathi namba 39 ya mwaka 2019, lilifunguliwa na watu wanne, wakiwemo ndugu wa marehemu Mengi.

Mahakama hiyo katika uamuzi wake uliotolewa juzi na jopo la majaji watatu, Rehema Mkuye (kiongozi), Dk Paul Kihwelu na Panterine Kente lilitupa shauri hilo kutokana na kasoro mbili zilizoonekana kwenye kiapo cha Jacquiline na cha wakili wake, Audax Kahendaguza vilivyoambatanishwa katika maombi hayo.

Kasoro hizo ambazo mahakama imekubaliana nazo ni viapo kuwa na maelezo yasiyopaswa kuwemo kwa hoja zinazohitaji ushahidi, maoni, mapendekezo na hitimisho na nyingine ni kutokubainisha chanzo cha taarifa ziliozokuwemo kwenye viapo hivyo.

Mahakama hiyo ilifikia uamuzi huo kutokana na pingamizi la awali lililowekwa na wasimamizi wa mirathi hiyo walioteuliwa na Mahakama Kuu ambao ni Abdiel Reginald Mengi akishirikiana na mdogo wake marehemu Mengi, Benjamin Abrahamu Mengi, kupitia kwa mawakili wao, Michael Ngalo na Roman Masumbuko.

Katika uamuzi huo, mahakama imesema kiapo kinapokuwa na kasoro kama hizo, aya zenye kasoro huondolewa kwenye kiapo na kuendelea na aya nyingine zisizo na kasoro.
Hata hivyo, imesema aya zenye kasoro ndizo msingi wa shauri hilo na kwamba, baada ya kuziondoa zinazobaki haziwezi kusimama zenyewe.
“Kasoro hizo zinayafanya maombi haya kutoweza kusimama, hivyo tunayatupilia mbali. Kwa kuwa shauri linatokana na mirathi hatutoi amri yoyote kuhusu gharama,” imesema mahakama hiyo katika uamuzi huo.

Awali, watu wanne, Benson Benjamini Mengi, William Onesmo Mushi, Zoebu Hassuji na Sylvia Novatus Mushi walifungua shauri la msingi la mirathi Mahakama Kuu wakiomba kuteuliwa kuwa wasimamizi wa mirathi hiyo, kwa mujibu wa wosia ulioachwa na Mengi.
Hata hivyo, Abdiel na Benjamini waliweka pingamizi dhidi ya wosia huo unaompa Jacquiline na wanawe haki ya urithi wa mali za Mengi, wakipinga uhalali wake huku wakiwasilisha jumla ya sababu nne za kuupinga.
Mahakama Kuu baada ya kusikiliza hoja za pande zote ilikubaliana na hoja za pingamizi dhidi ya wosia huo na kuikataa kuwa ni batili.

Jaji Yose Mlyambina alikubaliana na sababu hizo za pingamizi huku akisema unawanyima urithi wanawe wengine (wakubwa, Abdiel na ndugu yake) bila kutoa sababu.

Pia Jaji Mlyambina katika hukumu yake hiyo ya Machi 18, 2021, aliukataa wosia huo akieleza kuwa ziliiingizwa mali za mke wake mkubwa na kwamba nakala yake alikuwa nayo mwenyewe Jacguiline Mengi ambaye alikuwa mnufaika.
Hivyo Jaji Mlyambina aliwateua Abdiel na Benjamini kuwa wasimamizi wa mirathi na akaelekeza mali za marehemu zigawiwe warithi wanaostahili kwa utaratibu wa kawaida kama wa mtu ambaye hakuacha wosia.

Mwananchi
Huyu binti sijui nani alikuwa mshauri wake!! Hata Kama kweli mzee Mengi aliandika usia ule na kumpatia yeye, angejiongeza kwa kutouonyesha hadharani pengine hata kuuchana angeweza uchana!!! maana kwa mtu yeyote mwenye akili timamu hawezi muelewa kwa akili za kibinadamu hata kisheria pia!! hakimu yeyote au Jaji mwenye utu ndani yake hawezi kuwa upande wake kwa namna yoyote ile!!
 
Huyu binti sijui nani alikuwa mshauri wake!! Hata Kama kweli mzee Mengi aliandika usia ule na kumpatia yeye, angejiongeza kwa kutouonyesha hadharani pengine hata kuuchana angeweza uchana!!! maana kwa mtu yeyote mwenye akili timamu hawezi muelewa kwa akili za kibinadamu hata kisheria pia!! hakimu yeyote au Jaji mwenye utu ndani yake hawezi kuwa upande wake kwa namna yoyote ile!!

Angepata mgao wake kama Mke mwenye watoto ktk familia.

Wachagga cyo wandengereko linapokija suala la mali.
 
Mbona inasemekana huyo Mama marehemu waligawana kabla kila mtu akabaki na chake? Huyo jack mkumbuke alimpa mzee raha mpaka akasahau uzee wake, kwani yeye hakuwaona wazee wenzie mpaka kumuoa msanii wetu Jack?
Walienda mahakamani wakataka kugawana wakaambiwa warudi ili mali igawanywe ndio hakuna aliyerudi mpaka wote wakakumbwa na mauti.
 
Walienda mahakamani wakataka kugawana wakaambiwa warudi ili mali igawanywe ndio akuna aliyerudi paka wote wakakumbwa na mauti
Itakuwa walielewana nyumbani na wakayamaliza, sasa sisi huku nje tunataka kujua kila kitu cha ndani [emoji3][emoji3][emoji3]
 
Hata akiacha mali zigawanywe kwa usawa atapata share kubwa tu ukizingatia kamkuta mengi tayari ni tajiri.. anachozingua huyu dada anataka kupiga kila kitu kama vile wamehustle pamoja na mengi kutafuta izo mali
Huyo dada hana akili
 
Huyu dada tamaa ya pesa itamfanya apoteze uhai. Amuulize yule mama aliyefariki juzi na wanae kwenye ajali ya gari.Infwakti Yule mama Immaculata Byemerwa kabla ya kuolewa na Engneer alikuwa na yuho mwanae Albert ambae ndo alikuwa dereva. Kaolewa kazaa Janet na Jolister.Na kumbuka kwamba alimkuta Josepahat ana watoto wakubwa .Sasa yule mama kapata ajali na kafariki na uzao wake wote. Kaacha watoto wa mzee wafaidi vizuri mali za baba na mama yao mzazi.
Jack acha tamaa.
Hii story ipo wapi tz au uganda
 
Ndio maana tunaambiwa tumtumikie Mungu na sio mali, utadhulumu watu, utauwa watu, utaibia watu ili tu upate hizo mali lakini siku ukifa unaacha kila kitu, na sio mali tu unaacha mpaka nguo zako za kuvaa unaondoka uchi kama ulivyokuja.
Nawaza tu-Malori ya mafuta 200, nyumba 80, mabasi 50, hoteli za five star 30, gari za kifahari hapa sizungumzii vi IST nazungumzia gari za kuanzia Milioni 100 unakuwa nazo 20, lakini siku ukizimika tu vinakuwa sio vyako tena watu wanajibebea...
Acha maneno mengi hizo mali ni bora kuliko kufa njaa.

Watumishi wenu tuu wanamapesa mengi mnawapa na hamsemi
 
Back
Top Bottom