Jacqueline Mengi aendelea kudondokea pua rufaa, mahakama yaondoa maombi yake ya kutaka kuurudisha wosia

Jacqueline Mengi aendelea kudondokea pua rufaa, mahakama yaondoa maombi yake ya kutaka kuurudisha wosia

Ni ujinga wake Mengi kama wachaga mna akili kwa nini Mengi akamatwe mpaka amalizwe na Jackline?
Tafadhali futa hii kauli.
Wanaume wote ni wajinga linapokuja swala la tekwa na sauti nyororo.

Kwa wale wanaoamini kwa Mungu wa yakobo, tumesoma jinsi Adam alivyodanganywa na Eva.

Samsoni na minguvu yake hakupona mbere ya Delila.

Daud akaona amuue mpiganaji wake Ili aweze kujimilikisha mke wake.

Tuachane na hizo Hadithi , tujikumbushe Monica Luinsick ,huyu alimkamata Raisi wa USA. Kumbuka hao wote sio Wachaga.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Danga limeangukia tena pua. Yaani Mali amezikuta anataka kufilisi familia,,? Haiwezekani kabisa. Amejenga uadui na hii familia kizembe Sana. Yaani mchagga ukishampeleka Mahakamani hamtakaa mkae meza Moja milele. Kwa Heri Gold Digger. Kwa Heri International Danga. Kaendelee tu kudanga maana ndicho unachofahamu. Na Ile kampuni Amorate Furniture uliua ukijua kuna pesa ya wosia fake. Swine mkubwa wewe. Ulitumalizia kipenzi cha watanzania. Yaani wale wamama,vijana na walemavu alikuwa anasaidia watakulaani wewe Danga Jack Ntubaliwe. Watanzania tuna hasira na hili Danga. Mzee Mengi amechangia Uchumi wa hii nchi halafu anaenda kufia ugenini kwa utata. Ndiyo maana hukudondosha hata chozi Moja. Yaani anaingizwa kaburini hata kope hukukunja Danga. Mnaomfamu mfikishieni hizi salamu.
Huyu mwanamke alishindwa kula na kipofu
 
Mke wa bilionea, marehemu Reginald Mengi ameendelea kukumbana na vigingi vya sheria baada ya mahakama ya rufaa kuondoa maombi yake ya kupinga uamuzi uliobatilisha wosia wa mwisho wa marehemu Reginald Mengi.

Mahakama imekubali hoja za upande wa watoto wakubwa wa marehemu na kubaini viapo vilivyoletwa na Jacquline Mengi na wakili wake vina makosa.

May mwaka huu Jaji Yose Mlyambina wa mahakama kuu aliukataa wosia unaodaiwa kuandikwa na Reginald Mengi kwa madai haukufata misingi ya kisheria.

Watoto wakubwa wa Reginald Mengi walipinga wosia huo wakisema baba yao hakuwa kwenye nafasi ya kuandika wosia kwasababu alikuwa anakabiliwa na matatizo makubwa ya kiafya tangu 2016.

Familia ya Dkt. Mengi ipo kwenye mgogoro mkubwa wa kisheria juu ya mirathi ya marehemu ambao ulianza punde baada ya kifo chake huku ndugu zake wakitaka kuteuliwa wasimamizi wa mirathi.

Hukumu iliyopita, jisomee=> HAPA


Samahani, hukumu ilitoka lini? Naweza kuipata? Ahsante.
 
Back
Top Bottom