Jaji Eliezer Mbuki Feleshi anafaa kuwa AG

Jaji Eliezer Mbuki Feleshi anafaa kuwa AG

Wanasahau kama DPP ni taasisi na pale kuna wakurugenzi wasaidizi kila kitengo na bado kuna wanasheria wa kanda ambao malanyingi ndo hufanya hizo kazi baada ya kumshauri DPP umuhimu wa kufanya hivyo, na mala nyingi huwa kuna kuwa na umuhimu wa kitechnique kufanya hivyo au wakati mwingine hakuna ushahidi na hata wakati mwingine kwa usalama wa nchi ambapo ushauri unatoka TISS na kwa Rais mwenyewe ambaye kumbuka ndo mteuzi wake.

Kama alikuwa na support yite hii ina maana kweli alikosa ushahidi unaodai ulikaliwa na PCCB, yaani walitunia TISS na Rais pia. Hapa sasa unaanza kuongea kuwa kama angetaka ushahidi angepata!!!

He was weak or compromised???!!!
 
wewe umekuwa naye kazini wapi, humu mitandaoni?

Mi napendekeza Mwanasheria mKuu awe yule Mhindi mzalendo kutoka Iringa Bw Sethi Singh wa Escrow. Nia ni kubalance viongozi, walio na wasio waaminifu. Itapendeza eeeh!
 
Kwa heshima na taadhima nampendekeza Dr Harrison Mwakyembe. Ningependa kuona AG wa style na personality ya Mwakyembe. Siasa anaijua, historia anaijua, kuongea anaweza na sheria ndiyo imelala pale.
 
Naona wafaidika wa Escrow bado mnaendeleza mtandao wa ulinzi; ebu tujikumbushe malalamiko ya bosi wa TAKUKURU (kama tulivyojulishwa katika wikiliks) juu ya rushwa kubwa kubwa kwamba DPP wa wakati huo wa EPA and co alifanya nini juu ya mashitaka ya watuhumiwa?
kwa bahati mbaya sana, watz wengi hawana information na kesi za epa. watu kadhaa walioshitakiwa walipatikana na hatia pale kisutu na walifungwa vifungo wengine wanatumia vifungo hadi sasa, na wengine bado kesi zao zinaendelea. akina maranda na wenzie walishafungwa tayari na bado wana kesi nyingine za kujibu. cha kujiuliza ni kwamba, kuna mhindi mmoja alifungwa miaka 2 akaambiwa alipe mamia ya mamilioni, alipoenda ndani hata mwaka haukuisha akatolewa kwa msamaha wa rais. ajabu yake watu hawaoni hilo kama dpp feleshi alifanya kazi hiyo na wale madogo masikini mawakili wa serikali pale kisutu,wanaona tu mengine. think twice.

binafsi sidhani kama feleshi atakubali kurudi kwenye shuruba za kulitumikia taifa kama hizo, ila kama angeteuliwa, hakika yake ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali ndio ingeboreshwa sana. waliofanya kazi na feleshi ndio wanaomjua alivyo. watu wa nje ambao wengine nimesikia wanasema chenge alikuwa dpp...hahaha, hata hawajui kinachoendelea hapa duniani. wana comment kwasababu wameona magazeti yamesema kitu.
 
Kwahiyo tulidanganywa pesa za EPA zilirudishwa?

kama zilirudishwa hiyo siyo water tight evidence siyo?
When the right does not read the left it is so difficult to lie!
mtu kama wewe ambaye hajui sheria na hajawahi kwenda mahakamani haupaswi kujadili naye, utapoteza muda. kwa hiyo wewe ulitaka feleshi awashitaki wale wahindi ambao Rais aliwapa amnesty? kwani yeye ndiye anaye arrest? kwa kukufahamisha, dpp hawezi kuvamia tu mtu na kumshitaki, anatakiwa kuletewa mtuhumiwa na watu wawili (polisi au pccb). hao wanawakamata, wanakusanya ushahidi, wanaleta jalada la ushahidi kwa dpp, kama hakuna ushahidi si utatia aibu mahakamani? ulishawahi kufika walau mahakamani mzee au mpo tu hapa mjini..
 
Kama alikuwa na support yite hii ina maana kweli alikosa ushahidi unaodai ulikaliwa na PCCB, yaani walitunia TISS na Rais pia. Hapa sasa unaanza kuongea kuwa kama angetaka ushahidi angepata!!!

He was weak or compromised???!!!
dpp hana uwezo kupeleleza, mawakili wake hawana hata uwezo wa kutumia bunduki wala kufanya upelelezi, hiyo ni kazi ya polisi na pccb. wanaokusanya ushahidi yaani wale wanaoenda battle ground sio dpp/mawakili wa serikali, ni polisi na pccb. polisi wakikusanya ushahidi ndio wanauleta kwa dpp pamoja na mtuhumiwa ili dpp amshitaki yule mtuhumiwa kwa kutumia ule ushahidi. kuna mgawanyo wa kazi hapo, na kati ya watu waliomwangusha sana dpp feleshi ni hosea ambaye haelezeki kwa kiswahili ila kwa lugha ya kihindi ningemweleza. ...ni mzigo wa taifa. ushahidi ni kesi ya UDA aliyochakachua jalada akapeleka jalada na watuhumiwa nusu kwa dpp, akamchukua mtuhumiwa mkuu awe shahidi...wote tulishuhudia pale kesi haiendesheki hadi dpp aliamua kuiondoa kwa aibu kwasababu ushahidi hauunganishiki na mpelelezi ambaye ni pccb ametengeneza mbinu za kumsaidia simon group.kisena...ni kama mtu anapeleleza kesi ovyo halafu anakurushia mpira kesi ikafie kwako, akiona haiendi vizuri anaenda kwenye vyombo vya habari anajipendekeza ili aonekana anfanya kazi kumbe bure kabisa.
 
Uliwahi kuiona profile ya Dr. Balali!?
..na je uliwahi kufuatilia alichodeliver BoT!

Uliwahi kuiona profile ya Prof. Anna Tibaijuka!?
..na je uliwahi kufuatilia alichodeliver wizarani!

Pamoja na ubunifu + compitence, ndio maana Mzee warioba kaja na wazo jipya nalo sio kuangalia watu bali kuangalia mfumo wa ni jinsi gani wanaingia pale.
Wabunge iwe 50/50 lakini kutoka kwa wananchi moja kwa moja sio uteuzi wa kishikaji.
Akina AG, CAG, CJ, mawaziri, wakurugenzi wasiteuliwe na mtu kirafiki bali wateuliwe na taasisi na terms of references zinazoeleweka ili kujua pale watakapoharibu na wakaweza kuwajibika. Yaani vetting iwe ya kihaki zaidi na hapo hata ukipewa wewe hiyo nafasi utaweza kudeliver maana utakaposhindwa utakuwa muungwana na kuuliza wanaojua wakushauri.

Wewe fikiria kauli ya huyu aliyetoka kuwa 'ushauri wangu haukueleweka' na mkuu wake anamshukuru kwa 'utumishi uliotukuka' wakati wananchi wote wanajua pesa za umma zimeliwa kwa makusudi na wala sio bahati mbaya! Hapo hata ukimshusha malaika hawezi kubadilisha chochote kwa mfumo huu!



mkuu umenena, njia peke ya kumpata MTU sahihi ni by vetting..LA sivyo watazidi kupeana kishikaji tu.mwisho wa siku tutapewa MTU hivyo mwenye kiburi na aliyejawa na majivuno Kama huyu alietoka.
 
Kwanza Feleshi ashitakiwe kwa kupokea rushwa kutoka kwa Iddi Simba na Simon Kisena aliyopokea kwa ajili ya kuondoa kesi ya UDA
watanzania 100 wakiwa wapumbavu kama wewe nchi hii itakuwa kama choo. kwa kifupi, ile kesi ya uda, aliyeharibu ni HOSEA. alikula rushwa ya mil.300 toka kwa Robert kisena wa simon group, badala ya kumweka kisena kuwa mtuhumiwa, akamuweka kuwa shahidi na anaharibu ushahidi wake ili asishitakike. kesi ikapelekwa kwa dpp, dpp akaendelea na kesi dhidi ya kina iddi simba, baadaye kuja kustuka akaona mtuhumiwa mkuu mmoja wapo ni yule aliyeletewa kama shahidi, robert kisena wa UDA. akamkamata na kumuunganisha. wakati kesi inaendelea akaomba ushirikiano na HOSEA kwamba walete ushahidi fulani dhidi ya kisena, hosea akagoma. ndio dili likabumbuluka kuwa kumbe dili lilishatengenezwa tangu awali. ili kesi isiharibikie kwenye acquittal ya no case to answer ambayo hatashitakiwa tena kwa facts zilezile, busara pekee ikawa kesi iondolewe, jalada lirudishwe kwa HOSEA ili hosea akakamilishe upelelezi na alete vielelezo vyote, akikamilisha hata kesho anaweza kupeleka lile jalada kwa dpp huyo mpya na idi simba na wenzie pamoja na kisena wakafunguliwa kesi upya kwasababu nolle waliotoa inaruhusu kushitakiwa upya. ila wangesubiri mahakama iwatoe wasingeshitakika tena wangekuwa na kinga. ajabu yake , inasemekana hadi leo hii tunapoongea HOSEA lile jalada ameliweka kapuni, na UDA ndio hiyooo inapaaa na kuongeza mabasi na kuingia partnership na wakubwa....hakuna mtu aliyepata shida kama feleshi.
 
Tunkamanini: Sitaki kuingia kwenye mabishano yako na AME. Lakini kwa faida wa wasomaji naomba kuweka jambo hili sawasawa

Kulingana na katiba yetu RAIS anayo mamlaka ya kumsaheme mtu/mfungwa yeyote aliyeapatikana na kosa mbele ya mahakama wakati wowote na hakuna chombo au mtu yeyote anayeweza kuhoji.

Lakini pia kulingana na katiba yetu, Rais hana mamlaka ya KUMSAMEHE mtuhumiwa yeyote wa makosa anayetarajiwa/aliyefikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Hivyo Rais kuwasamehe wezi wa EPA waliorudisha pesa wizi kwa hiari yao ilikuwa ni kuvunja katiba ya JMT.

Kama Rais alikuwa anawapenda sana hao watuhumiwa EPA, angesubiri kwanza wapatikane na kosa mbele ya mahakama halafu ndio awasamehe, hakuna mtu/chombo chochote kingehoji kwani mamlaka hayo amepewe na katiba ya JMT
unajua maana ya amnesty? kama rais ametoa amnesty unafikiri mtu mdogo kama feleshi angeenda mtaani kukamata watu awapeleke mahakamani? kama polisi na pccb wenye mamlaka ya kukamata na kumpelekea feleshi ashitaki na hawakufanya hivyo, inakuwaje lawama zinaenda kwa feleshi?
 
Kwa heshima na taadhima nampendekeza Dr Harrison Mwakyembe. Ningependa kuona AG wa style na personality ya Mwakyembe. Siasa anaijua, historia anaijua, kuongea anaweza na sheria ndiyo imelala pale.
anahitajika mtu ambaye alishawahi kufanya kazi ya wakili wa serikali, huwezi kumweka mtu ambaye haijui ofisi kabisa. ile sio ofisi ya mchezo.
 
X-DPP Dr. Feleshi ni mzigo kuliko Chenge na werema pamoja. Kumbukeni ushauri wake kwa rais in the EPA scandal.
 
wangempa hata Tundu Lissu kuwa mwanasheria wa serikali ndani ya ccm bado sijaona anafaa kumrithi tumbili werema
 
Yaani watu wahuni na walevi Kama Feleshi awe AG....

Ila yote yanawezekana maana alipoteuliwa kuwa DPP wengi hatukuamini na alipopewa ujaji tukapigwa na butwaa ngoja tusubiri ajabu lingine....
felshi hanywi pombe kabisa aisee. labda haumjui.
 
X-DPP Dr. Feleshi ni mzigo kuliko Chenge na werema pamoja. Kumbukeni ushauri wake kwa rais in the EPA scandal.
feleshi hajawahi kutoa ushauri kwa rais hata siku moja, ila aliletewa kesi za kushitaki na watu walishitakiwa na wapo ndani hadi leo.
 
Hii ni hati inayotolewa na DPP yenye nguvu ya kumwondolea mashitaka mtuhumiwa.
Wakati wa DPP Feleshi hati za aina hii zilitolewa kwa watuhumiwa hasa wa mauaji ikiwamo ile ya mtuhumiwa wa mauaji ya Bilionea wa Arusha Erasto Msuya aitwaye Joseph Damas(Chusa).Pamoja na watuhumiwa wengine kumtaja kama mhusika mkuu lakini DPP alimfutia mashitaka kwa kasi ya ajabu..
unajua kuwa katika kila mkoa kuna muwakilishi wa dpp anayefanya yote hayo? ni sawa na wewe ukienda kenya ukajisaidia barabarani, rais kikwete akaenda kutembelea kenya watu wakamlaumu rais kuwa amefanya jambo hilo kumbe yeye alikuwa ame delegate power kwa wakili wa serikali mfawidhi wa mkoa. hauijui hiyo ofisi, bora unyamaze kimyaaa.
 
Back
Top Bottom