Jaji Eliezer Mbuki Feleshi anafaa kuwa AG

Jaji Eliezer Mbuki Feleshi anafaa kuwa AG

Acha upumba.vu, samahani kama nimekuwa mkali kwa hili, mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni, kama humfahamu mtu ni bora ukakaa kimya, nimefanya kazi na huyu jamaa na nakuhakikishia sidhani hata kama anajua radha ya pombe ikoje, jamaa ni mcha Mungu na muadilifu hasa, kama kuna mengine yaseme lakini kuhusu uadilifu Feleshi ni miungoni mwa watu wachache sana walobakia Tanzania, uliza wanasheria wa serikali watakuambia.


Mimi NADHANI TATIZO LETU SI TU UADILIFU KAMA WENGI TUNAVYOTAKA KUAMINISHWA.TUNAHITAJI KIONGOZI/VIONGOZI 'COMPETENT NA CREATIVE'SINA HAKIKA KAWA FELESHI ANAO UWEZO WA KUTOSHA MANA HATA AKIWA DPP AMEKUWA AKITILIWA SHAKA NA WADAU KIUWEZO JAPO N MSOMI MWENYE VYETI.
 
Mpeni toto tundu, ANTIPAS TUNDU LISU, hapo nchi itakuwa imepata mtaalamu hao wengine ni wababaishaji tu
 
Mimi NADHANI TATIZO LETU SI TU UADILIFU KAMA WENGI TUNAVYOTAKA KUAMINISHWA.TUNAHITAJI KIONGOZI/VIONGOZI 'COMPETENT NA CREATIVE'SINA HAKIKA KAWA FELESHI ANAO UWEZO WA KUTOSHA MANA HATA AKIWA DPP AMEKUWA AKITILIWA SHAKA NA WADAU KIUWEZO JAPO N MSOMI MWENYE VYETI.

Kutiliwa shaka na wadau wa jamiiforums wanaookota taarifa magazetini na kwa wanasiasa? Hizo rushwa kubwa zipi ambazo alipelekewa ushahidi akaacha kushtaki? Dr. Slaa aliwahi sema anao ushahidi akaambiwa apeleke akalala mbele, yule kijana wa Kagoda naye vilevile, TAKUKURU walipolalamika akawahoji waseme ni faili gani hajalishughulikia wakakaa kimya, acheni kutuka mtu kwa vitu msivyovijua.
 
Wewe Laki si pesa utaishia pabaya maana unajiongelesha kama vile unatekenywa unawaza kwa kutumia nini? ??,naona unatumia kinyeo ndo maana maandishi yako yana kichefuchefu, shame on you
 
Unadhani anafanya hivyo kwa kukurupuka tu? ni lazima uamuzi wake ubase kwenye ushahidi na pia maslahi ya umma, kama DCI kawasilisha kwa DPP ushahidi wa kumsafisha mtuhumiwa unadhani DPP atafanya nini zaidi ya kuiondoa kesi? DPP sio chombo chunguzi kumbuka.

Wewe NAWE USIWE -----,DPP KUTOKUWA CHOMBO CHA UCHUNGUZI HAINA MAANA KWAMBA YEYE HAWEZI KUHOJI CIRCUMSTANCE NA BADALA YAKE AKAE AKIMSUBIRI DCI.ANAO UWEZO WA KUAGIZA UCHUNGUZI UFANYIKE NA ANAO MAAFISA WA KUSHIRIKIANA NA DCI.
 
tatizo hujiheshimu na unaleta mizaha kwenye mambo ya msingi, hilo la uda wala halihitaji uwe na cheti cha form four kuzitambua rangi zake, hossea kampeleka kwa dpp kisena kama shahidi, dpp kapitia faili la ushahidi toka pccb akagundua kisena pia kahusika na akamjumuisha na watuhumiwa wengine, hossea kwa kuwa pccb ndio chombo chunguzi kwa hilo swala ili kumuokoa kisena akavuruga ushahidi, na kumbuka kesi ni ushahidi ulitaka kesi ikae mahakamani wakati takukuru wamehold na kuhujumu ushahidi?


alafu wewe jamaa ni mtu flani hv wa pahala flani hivi wanapenda sana kujipendekezapendekeza.tuondolee fenes wako hapa.jamaa hawezi hata ku-argue.kuna wakati flani manfred alimwalika kwenye kipimajoto,dah aibu tupu.nilijiuliza huyu mwanasheria au vitu gani, utadhani katoka nyakahako leo?anaweza jibu hoja hata moja bungeni huyo?muhurumie ndugu yako, atakufa kwa presha akikutana na vchwa vya cdm kama lisu.nafuu awe hata jaji mkuu kuliko ag.hyo nafasi lazima ate na sifa za mwanasiasa,aweze ku_argue.
 
alafu wewe jamaa ni mtu flani hv wa pahala flani hivi wanapenda sana kujipendekezapendekeza.tuondolee fenes wako hapa.jamaa hawezi hata ku-argue.kuna wakati flani manfred alimwalika kwenye kipimajoto,dah aibu tupu.nilijiuliza huyu mwanasheria au vitu gani, utadhani katoka nyakahako leo?anaweza jibu hoja hata moja bungeni huyo?muhurumie ndugu yako, atakufa kwa presha akikutana na vchwa vya cdm kama lisu.nafuu awe hata jaji mkuu kuliko ag.hyo nafasi lazima ate na sifa za mwanasiasa,aweze ku_argue.

Usione nimekaa kimya ukadhani unayoandika yana maana, nimeamua kukupuuza, we hapa sasa ndo unaona unaweza kuargue yeye hawezi? kwanza unatukana na kuleta midhaha kwenye issue ambayo ni sensitive hii pekee ni sababu tosha ya mtu kupuuza unachoandika, tulikuwa tukimuongelea Jaji Feleshi wewe unamzungumzia "fenes, nakusihi anzisha uzi kumuhusu.

Hoja zako ni za kipuuzi kabisa, eti AG anafaa kuwa mwanasiasa, you can't be serious, hao waliopoliticise uAG huoni walipo sasa?!!!
 
Hakuna mtakatifu ndani ya nchi yetu kwa sasa 'the Country is corrupt', tutalszimika kuwateua wale wale kati ya wachafu sababu hatuna la kufanya. Hakuna atakaeniaminisha kuwa X-DPP ni mtakatifu, kesi ngapi zimepigwa zengwe hatujui zilipoishia hasa za wakubwa na matajiri!?

hatuwezi kubinafsisha cheo cha AG tukampa Mchina, Mmarekani au Mkaburu?
 
Mimi NADHANI TATIZO LETU SI TU UADILIFU KAMA WENGI TUNAVYOTAKA KUAMINISHWA.TUNAHITAJI KIONGOZI/VIONGOZI 'COMPETENT NA CREATIVE'SINA HAKIKA KAWA FELESHI ANAO UWEZO WA KUTOSHA MANA HATA AKIWA DPP AMEKUWA AKITILIWA SHAKA NA WADAU KIUWEZO JAPO N MSOMI MWENYE VYETI.
Uliwahi kuiona profile ya Dr. Balali!?
..na je uliwahi kufuatilia alichodeliver BoT!

Uliwahi kuiona profile ya Prof. Anna Tibaijuka!?
..na je uliwahi kufuatilia alichodeliver wizarani!

Pamoja na ubunifu + compitence, ndio maana Mzee warioba kaja na wazo jipya nalo sio kuangalia watu bali kuangalia mfumo wa ni jinsi gani wanaingia pale.
Wabunge iwe 50/50 lakini kutoka kwa wananchi moja kwa moja sio uteuzi wa kishikaji.
Akina AG, CAG, CJ, mawaziri, wakurugenzi wasiteuliwe na mtu kirafiki bali wateuliwe na taasisi na terms of references zinazoeleweka ili kujua pale watakapoharibu na wakaweza kuwajibika. Yaani vetting iwe ya kihaki zaidi na hapo hata ukipewa wewe hiyo nafasi utaweza kudeliver maana utakaposhindwa utakuwa muungwana na kuuliza wanaojua wakushauri.

Wewe fikiria kauli ya huyu aliyetoka kuwa 'ushauri wangu haukueleweka' na mkuu wake anamshukuru kwa 'utumishi uliotukuka' wakati wananchi wote wanajua pesa za umma zimeliwa kwa makusudi na wala sio bahati mbaya! Hapo hata ukimshusha malaika hawezi kubadilisha chochote kwa mfumo huu!


 
Tatizo sio nani anafaa kuwa pale tatizo lipo kwenye msingi na mfumo mbovu mfano ulio hai tunaiona wenyewe kulikuwa na watu tuliwaamini lakini leo mmejionea wenyewe walivyotusaliti na kuwa sikio la kufa ndani ya ccm hakuna atakae kaa ndani ya mwaka na akitoka lazima awe na skendo.
 
Kutokana na kujiuzulu kwa aliyekuwa mwanasheria mkuu wa serikali Jaji Werema ni wazi sasa nafasi hiyo inabaki wazi.

Kwa walio wadau wa tasnia hii ya sheria nadhani wataungana nami pasina shaka lolote kuwa kutokana na nafasi hiyo kuwa nyeti kwa ustawi wa Taifa lolote lile duniani, inahitaji kushikiliwa na mtu mwenye nidhamu, weredi na mwenye uadilifu wa hali ya juu.

Kwa wasomi na wanataaluma wa sheria nchini wenye sifa hitajika ni adimu sasa kwa taifa letu hili kwa sasa, binafsi namfahamu vyema Mhe. Jaji Feleshi licha ya kufanya nae kazi kwa muda wa miaka michache lakini ni mtu ambaye ukimweka na viongozi waandamizi wenye hadhi yake ni kama mtu aliyeshushwa toka peponi.

Hakuna mtu wa kada yeyote anaeza ongea swala la hongo kwa Mhe. Jaji Feleshi, kwa kipindi chote nlichofanya kazi pale Sukari sijawahi ona mfanyakazi wa kawaida akimtangulia kufika ofisini na akimuwahi kutoka ofisini, sikuelewa nia ya Mhe Rais kumtoa kwenye uDPP lakini huenda alikuwa akiandaliwa kushika nyazifa za juu katika muhimili huo muhimu ili kuusuka upya lakini kutokana na ombwe hili katika nafasi ya AG bado sijaona mtu mbadala.

Safari hii tujaribu mwanamke tuone, wanaume huwa wanatutoa mswaki kila siku. Angela Kairuki je? Kwa wanaume Tundu Lissu angetufaa kama lengo letu lingekuwa kuleta utengamano wa kitaifa.
 
Huyo mnyaruanda tumpeleka wapi! Keshaharibu toka alipokua DPP

I don't think you guys know this Fella Dr. Feleshi, ni mchapakazi mno . Anajali wafanyakazi siyo hao akina Werema bora ameondoka. Jamaa alikuwa anawazidi akili akina Werema, Masaju na Hosseah na hakutaka wan wamwingilie katika kazi zake. Wakajenga fallacy kwamba anawachia wala rushwa na hashirikiani na wenzake wakati siyo kweli.
Hata hivyo sipendi mleta mada alivyoileta kwani inaweza kuchangia hata asifikiriwe kwa post hiyo.
 
Hawa unaowataja ni mtazamo ule ule wa siku nyingi kuwa Ukimuelimisha mtu asiye mwaminifu kutunza pesa ni kumpa njia zaidi za kukuibia! Na mtubutu kufanya hivyo muone, mtu ana billion 10 kwenye account na kwa vile alizipata kwa njia isiyo halali anapigana ziwe billion 100 kwa njia zile zile!
Andrew Chenge nae aliimudu vyema hiyo nafasi. Chenge ni msomi mzuri tu wa Havard na ana ushawishi mkubwa kwa jamii
Nimrod Mkono anafaa sana kuwa mwanasheria mkuu wa serikali
Nimemsikia Prof. Lipumba kwenye Nipashe asubuhi (R1) anesema yale maneno ya "rais atumie busara" hayaamini tema na haziamini busara za rais tangu alipopindua mawazo ya Jaji Warioba
Tumuachie MH Rais atamchagua mtu mzuri mwenye busara lkn tukubali tukatae rushwa ipo pale pale
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Una uhakika anajua kazi yake kweli? angekuwa anajua kazi yake angeshindwa vipi kuchukulia hatua za kinidhamu wateule wake badala yake ni mpaka kapata shinikizo la nje?

Mtu kajiuzulu kutokana na matumizi mabovu ya ofisi na yenye harufu ya kijinai then Raisi anampongeza na kumpamba eti uongozi wake ulitukuka na ulisheheni uadilifu!!??? Shame, shame shame...only in Tanzania.

Hivi hakuna kipenngele chochote kikatiba kinachoruhusu Rais kuzodolewa? Maaana kuna kitu kinapanda kooni nakosa pa kutemea....msaada please kwa 'wasomi'!
 
Safari hii tujaribu mwanamke tuone, wanaume huwa wanatutoa mswaki kila siku. Angela Kairuki je? Kwa wanaume Tundu Lissu angetufaa kama lengo letu lingekuwa kuleta utengamano wa kitaifa.

Kavulata nimekupa like ya Tundu Lisu, huyo mwingine simfahamu na ni kama vile ametokea ukoo wa maza?
 
Hivi hakuna kipenngele chochote kikatiba kinachoruhusu Rais kuzodolewa? Maaana kuna kitu kinapanda kooni nakosa pa kutemea....msaada please kwa 'wasomi'!

Katiba mpya inaruhusu, ila maccm walibaka haipo tena meza wembe aina topaz hiyo kitu kitashuka fasta....
By the way maoni ya wananchi yako mbioni ila yatasimamiwa na madc, ded, nk
 
Naona wafaidika wa Escrow bado mnaendeleza mtandao wa ulinzi; ebu tujikumbushe malalamiko ya bosi wa TAKUKURU (kama tulivyojulishwa katika wikiliks) juu ya rushwa kubwa kubwa kwamba DPP wa wakati huo wa EPA and co alifanya nini juu ya mashitaka ya watuhumiwa?

Feleshi ni mmoja wa watu wanaowalinda mafisadi. Kumbuka vita kati ya Feleshi na Hosea katika sakata la EPA. Jamaa hafai kabisa huyu.
 
Nafasi ya AG ni mhimu na nyeti. Itangazwe ili walio na sifa waombe na waweze kuhojiwa pamoja na jamii kuwajua vizuri na kwa kina
 
Back
Top Bottom