Jaji Elinaza Luvanda ajiondoa kuendesha kesi ya Mbowe na wenzake baada ya washtakiwa kudai hawana imani naye

Mkuu.. Jaji Mkuu ndio tatizo kubwa..
Nimeshalisema sana hili..
Hatuna CJ hapa Tz..
Ni sanamu tu yule..
Amekubali kuwa zezeta wa serikali..
Shame.
Hii inaonyesha Jaji Luvanda alikua anafanya chini ya shinikizo, ndiyo maana alipopata huu upenyo wa kukaa pembeni ameamua kuliacha shauri washughulike nalo wengine.
 
sio lazima Mawakili waombe, mahakama ipo pale kuhakikisha haki inatendeka kwa pande zote mbili; yaani mtuhumiwa na hata upande wa Jamuhuri, hivyo Jaji yuko sahihi kabisa kutoa maelekezo kwa upande wa Jamuhuri kwenda kurekebisha hati ya mashitaka hata kama wao hawajaomba.
 
Angekuwa baba ako yupo mahabusu sijui kama ungeongea huu utumbo
 
ameshalkubali kujitoa sasa, wewe na hao mawakili nani kaonekana mpuuzi?
 
Asante sana.

Hii inaonyesha Jaji Luvanda alikua anafanya chini ya shinikizo, ndiyo maana alipopata huu upenyo wa kukaa pembeni ameamua kuliacha shauri washughulike nalo wengine.

Unaonaje hilo mkuu?
Tuna majaji wa hovyo kabisa
 
Washenzi sana hawa, hawajui huyo Jaji ataepangiwa hiyo kesi hatokuwa na huruma yeyote, na kwa ushahidi uliopo Jaji akiamua kutenda haki Mbowe anaenda Jail, jinai sio ya kuchezea, kosa dogo tu umenitukana na niko na ushahidi bila huruma ya hakimu unaenda Jail na unalipa faini, wacha wajitekenye watacheka wenyewe baadae, bahati mbaya sana ndo anaichukuwa JK Feleshi mwenyewe asojua kupindisha sheria watafurahi.
 
Kwa nini upande wa mashitaka uliokosea kuandaa hati usubiri Jaji awape maelekezo ya kurekebisha makosa? Wewe uliyekosea ndiye unakua mwepesi kugundua ulipokosea (kama uko kihaki) na kuomba ufanye hayo marekebisho. Mkuu jaribu kuwa neutral na kuliona hilo.
 
Hakuna kitakachobadilika pamoja na jaji kujitoa kulinda tu taaluma na heshima ya nafasi yake'mark my words' matokeo ni yaleyale
 
Mahakama ziache kutumika,ndio mhimili pekee unaoweza kuwaokoa Watanzania,mihimili mingine inapwaya sana.
 
Hii haimanishi judge anaingilia mwenendo wa kesi..na anatoa maelekezo nini cha kufanya..ili iweje..hiyo ni kazi ya judge??kwakuwaambia wakairekebishe inamaana anakubali imekosewa..and what does the law say hati inapokosewa..na ombi la kina kibatala lilikuwa ni nini kuhusiana na hati??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…