Jaji Elinaza Luvanda ajiondoa kuendesha kesi ya Mbowe na wenzake baada ya washtakiwa kudai hawana imani naye

Jaji Elinaza Luvanda ajiondoa kuendesha kesi ya Mbowe na wenzake baada ya washtakiwa kudai hawana imani naye

Baada ya Jaji Luvanda kutupa mapingamizi yote yaliyotolewa na Mawakili wanaomtetea Mbowe na wenzake, Mbowe amesimama na kumtaka Jaji Luvanda ajiondoe kuendesha kesi hiyo kwani ameonyesha upendeleo na taarifa zinasema ana maelekezo ya kupindisha sheria ili amfunge Mbowe na wenzake.

Jaji Luvanda amesema hati ya mashtaka ni batili amewashauri Mawakili wa serikali wakaibadilishe, Mawakili upande wa utetezi wamegoma wamemwambia kama hati ya mashtaka ni batili basi futa kesi Jaji akakataa ila amekubali kujiondoa kuendesha kesi.

====

Jaji Elinaza Luvanda wa Mahakama Kuu Divisheni ya Uhujumu Uchumi na Makosa ya Rushwa na aliyekuwa anaisikiliza kesi ya Uhujumu Uchumi namba 16/2021 yenye mashtaka sita yakiwemo ya Ugaidi, amejitoa kusikikiza kesi hiyo.

Sababu ya kujitoa katika kesi hiyo ni kutokana na mshtakiwa wa nne katika kesi hiyo, Freeman Mbowe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema Taifa, kuieleza mahakama hiyo kuwa yeye na washtakiwa wenzake watatu hawana imani na Jaji huyo katika kutenda haki dhidi ya kesi yao.

Kesi imehairishwa mpaka jaji mwingine atakapopatikana. Pia awali Jaji Elinaza Benjamin Luvanda alikataa kutoa uamuzi wake leo juu ya mapingamizi ya upande wa utetetezi mpaka atapopata hansard / kumbukumbu za majadiliano ya Bunge kuhusu sheria ya ugaidi.

Wote walikubaliana kuwa kesi hii ina masilahi mapana kwa umma wote waliopo ndani ya Mahakama na nje.

Hoja 3 za upande za upande wa utetezi zilikuwa zinashambulia madhaifu na kasoro ya hati ya mashtaka. Hoja ya kwanza ilikubaliwa na jaji wakati hoja ya pili ilikubaliwa kwa nusu yake na jaji wakati hoja ya tatu ya kutupiliwa mbali au kufutwa kesi, jaji aliikataa.

Na kwa msingi huo mtuhumiwa Freeman Mbowe kwa niaba ya wenzake akasimama na kusema hawana imani na Jaji Elinaza Benjamin Luvanda kuendelea kusikiliza kesi hiyo, na mheshimiwa Jaji E.B Luvanda akaafiki ombi hilo na kujiengua kusikiliza kesi hii.

Source : Mwananchi Digital

UPDATE: Jaji Luvanda akubali
Jaji Elinaza Luvanda aliyekuwa anaisikiliza kesi ya Uhujumu Uchumi nyenye mashtaka 6 yakiwemo ya ugaidi, amejitoa kusikiliza kesi hiyo, sababu ya kujitoa kwake, ni kutokana na mshtakiwa wa nne katika kesi hiyo, Mhe. Freeman Mbowe na wenzake kuwa hawana imani na Jaji huyo.

Pia soma >
Mahakama ya Uhujumu Uchumi: Mvutano mkali kesi ya Mbowe na wenzake. Hatma ya kesi kujulikana Septemba 6
. "Jaji Mwenzangu Luvanda" Machozi ya samaki majini hayatakufikia wewe na kizazi chako mpaka cha nne, tekeleza maagizo
. CHADEMA tusimpe vitisho Jaji Luvanda, mpaka sasa hajapendelea pande yoyote. Kibatala na jopo lake walichemka
Kuna msemo una kufa ila kufa kishujaa, thanks mwenyekiti wangu mh Mbowe umeitendea haki YAKO nafsi yako ,tz , na Dunia KWa ujumla, na Mungu anasema twende tu, usiogope asema bwana
 
Jaji asikubali upuuuzi na ushenzi huu wa Mawakili wa Mbowe na Mbowe mwenyewe.

Huko ni kumtusi Jaji na Mahakama,

Mbowe na mawakili wake hawana sababu ya msingi zaidi ya kutaka kumyumbisha Jaji, tuhuma wanazo zitoa dhidi ya Jaji ni za kipuuuzi na hazina uthibitisho wowote zaidi ya kudhania na kuhisia tu, hakuna hoja hapo, kwa hiyo anamtaka Jaji ambaye ni RAFIKI YAKE ili asikilize kesi yake.

kwa hiyo imefikia sasa Mtuhumiwa kuchagua Jaji wa kusikiliza kesi yake aisee! hata marekani hakuna kitu kama hicho.

ninacho sema Jaji angeweza kujitoa kama tuhuma zinazo tolewa na Mbowe zina uthibitisho la sivyo Jaji aendelee tu kungurumisha kesi.......asikubali kubabaishwa na hoja za kipuuzi na za kuokoteza na zenye lengo la kuchelewesha haki kutendeka.
Kiko wapi sasa
 
Kuna Jaji mmoja alishakiri kabisa na kusema "Jamani hizi kesi za kisiasa hizi na mimi nina watoto wadogo".

Tufika muda tuwaonee huruma hawa jamaa baadhi yao wanafanya kazi wa mashikinizo makubwa mno toka Serikali, ukifanya tofauti na wanavyotaka wao - Je mhimili wa mahakama unaweza kukupatia personal security ?
 
Jaji amekosea sana kujitoa ktk kesi.
Maana yake ni kwamba tuhuma alizo zitoa Mbowe dhidi ya Jaji ni za kweli.
Kabla ya kujitoa hizo tuhuma lazima kwanza zithibitishwe maaana sio tu kwamba zina mchafua Jaji/Majaji bali zinauchafua Muhimili wa Mahakama.
Jaji anajua sana kwa nini amejitoa ,ila wewe tu genge lako ndo hamjaelewa
 
Mkuu ninaheshimu mihimili ya nchi....

Binafsi mambo ya mahakamani huwa SIINGIZI mdomo wangu kwa kuchelea kuwa "pang'ang'a".....

Kesi iko mahakamani niongelee nini mimi muuza "gahwa" na Al Kasus huku kwa "Manjunju"?!!🤣🤣

Nisalimie "ufipa" hapo najua mkuu wangu mnamaliza makopo ya dawa za mbu tu tehe tehe tehe 🤣

#SiempreJMT
#NchiKwanza

Ila mkuu kipo mnachoweza kukataa kweli?

Nay wa Mitego naona aliwatendea haki sana.

Au nasema uongo ndugu yangu?
 
Jaji asikubali upuuuzi na ushenzi huu wa Mawakili wa Mbowe na Mbowe mwenyewe.

Huko ni kumtusi Jaji na Mahakama,

Mbowe na mawakili wake hawana sababu ya msingi zaidi ya kutaka kumyumbisha Jaji, tuhuma wanazo zitoa dhidi ya Jaji ni za kipuuuzi na hazina uthibitisho wowote zaidi ya kudhania na kuhisia tu, hakuna hoja hapo, kwa hiyo anamtaka Jaji ambaye ni RAFIKI YAKE ili asikilize kesi yake.

kwa hiyo imefikia sasa Mtuhumiwa kuchagua Jaji wa kusikiliza kesi yake aisee! hata marekani hakuna kitu kama hicho.

ninacho sema Jaji angeweza kujitoa kama tuhuma zinazo tolewa na Mbowe zina uthibitisho la sivyo Jaji aendelee tu kungurumisha kesi.......asikubali kubabaishwa na hoja za kipuuzi na za kuokoteza na zenye lengo la kuchelewesha haki kutendeka.
Unapokuwa na akili za namna hii ni kama upo kwenye kilevi fulani, hakuna jambo lolote nje ya kilevi chako linaloweza kubadili akili yako ione tofauti na unavyoona wewe ukiwa kwenye kilevi hicho.

Tatizo lako ni kwamba unataka wengine wote nao waonekane kuwa walevi kama ulivyo wewe!
 
Jaji asikubali upuuuzi na ushenzi huu wa Mawakili wa Mbowe na Mbowe mwenyewe.

Huko ni kumtusi Jaji na Mahakama,

Mbowe na mawakili wake hawana sababu ya msingi zaidi ya kutaka kumyumbisha Jaji, tuhuma wanazo zitoa dhidi ya Jaji ni za kipuuuzi na hazina uthibitisho wowote zaidi ya kudhania na kuhisia tu, hakuna hoja hapo, kwa hiyo anamtaka Jaji ambaye ni RAFIKI YAKE ili asikilize kesi yake.

kwa hiyo imefikia sasa Mtuhumiwa kuchagua Jaji wa kusikiliza kesi yake aisee! hata marekani hakuna kitu kama hicho.

ninacho sema Jaji angeweza kujitoa kama tuhuma zinazo tolewa na Mbowe zina uthibitisho la sivyo Jaji aendelee tu kungurumisha kesi.......asikubali kubabaishwa na hoja za kipuuzi na za kuokoteza na zenye lengo la kuchelewesha haki kutendeka.
Ww ni mpumbavu jaji anakiri hati ya mashtaka in shida kwa upeo wake pengine anaweza kujitoa kukwepa aibu anawezaje kung'ang'ania kesi ambayo kabaini ina makosa ktk ufunguaji wake?
 
Jaji asikubali upuuuzi na ushenzi huu wa Mawakili wa Mbowe na Mbowe mwenyewe.

Huko ni kumtusi Jaji na Mahakama,

Mbowe na mawakili wake hawana sababu ya msingi zaidi ya kutaka kumyumbisha Jaji, tuhuma wanazo zitoa dhidi ya Jaji ni za kipuuuzi na hazina uthibitisho wowote zaidi ya kudhania na kuhisia tu, hakuna hoja hapo, kwa hiyo anamtaka Jaji ambaye ni RAFIKI YAKE ili asikilize kesi yake.

kwa hiyo imefikia sasa Mtuhumiwa kuchagua Jaji wa kusikiliza kesi yake aisee! hata marekani hakuna kitu kama hicho.

ninacho sema Jaji angeweza kujitoa kama tuhuma zinazo tolewa na Mbowe zina uthibitisho la sivyo Jaji aendelee tu kungurumisha kesi.......asikubali kubabaishwa na hoja za kipuuzi na za kuokoteza na zenye lengo la kuchelewesha haki kutendeka.
Kuficha ujinga ni hekima!
 
...........................
ISSUE ambayo inatrend ni ile offer ya Mahakama kuwapatia upande wa Jamhuri kitu ambacho haikukiomba-to amend/recorrect/reconstruct the charge sheet' Republic hakiomba kitu kama hiki kabisa, kwa hiyo wamepewa zawadi ambayo pengine hawakustahili kuwa nayo.....kuna msemo wa Kisheria unaosema kuwa "Mahakama sio mama yako, akupatie kila unachohitaji pale unapolia" The court is not your motherwho grants things you have never asked for".

Kwa maana hiyo hili tu ndilo jambo ambalo kwa mtizamo wa wananchi kuwa mahakama imetoa kitu ambacho sio ombi la Jamhuri, kwa sababu Jamhuri iliamini kuwa charge sheet yao inajitosheleza kumbe ina matobotobo......kisheria charge sheet ndio inayomwezesha mtuhumiwa kuweza kujitetea......sasa kama kuna fabricated offenses (if any) inakuwa ngumu kwa accussed kujitetea; ndio maana Mawakili wa utetezi wameweka nguvu nyingi kwenye PO =Preliminary Objections.

jopo la Majaji 3 wa Mahakama ya Rufani mwaka 2020 Kwenye Kesi ya Ezekile Kwihuja vs Republic (2020) unreported, iliamuru washitakiwa watolewe magereza haraka iwezekanavyo baada ya kuonekana makosa ya hati ya mashitaka kwenye Kesi ya Mahakama Kuu chini ya Jaji Ruhangisa. Utamu na ubora wa sheria ni ule mwendelezo wa Rufaa kutoka mahakama moja kwenda nyingine; hata uamuzi huu wa leo ungeweza kukatiwa Rufaa hata kama Jaji angegoma kujitoa;

Itoshe kusema kuwa sheria ni uwanja wa kujifunza kila siku na ndio sababu mojawapo ya kusema Mawakili Wasomi

Kuanzia hapa, hii ndiyo sababu kuu ya Jaji Luvanda kuamua kukaa pembeni baada ya kuamliwa kufanya hivyo. Hili kosa sijui kwa nini alilifanya?
 
Kengeza la gaidi DJ haliwezi kumtisha jaji mpaka akubali kujitoa, gaidi ajiandae kula mvua za kutosha!. 🤣
Keshajitoa, ili na wewe usionekane makengeza yako ya akili, futa 🖕comenti yako hapo!
 
Jaji asikubali upuuuzi na ushenzi huu wa Mawakili wa Mbowe na Mbowe mwenyewe.

Huko ni kumtusi Jaji na Mahakama,

Mbowe na mawakili wake hawana sababu ya msingi zaidi ya kutaka kumyumbisha Jaji, tuhuma wanazo zitoa dhidi ya Jaji ni za kipuuuzi na hazina uthibitisho wowote zaidi ya kudhania na kuhisia tu, hakuna hoja hapo, kwa hiyo anamtaka Jaji ambaye ni RAFIKI YAKE ili asikilize kesi yake.

kwa hiyo imefikia sasa Mtuhumiwa kuchagua Jaji wa kusikiliza kesi yake aisee! hata marekani hakuna kitu kama hicho.

ninacho sema Jaji angeweza kujitoa kama tuhuma zinazo tolewa na Mbowe zina uthibitisho la sivyo Jaji aendelee tu kungurumisha kesi.......asikubali kubabaishwa na hoja za kipuuzi na za kuokoteza na zenye lengo la kuchelewesha haki kutendeka.
😀😃😄😄😄🤑👊
 
Baada ya Jaji Luvanda kutupa mapingamizi yote yaliyotolewa na Mawakili wanaomtetea Mbowe na wenzake, Mbowe amesimama na kumtaka Jaji Luvanda ajiondoe kuendesha kesi hiyo kwani ameonyesha upendeleo na taarifa zinasema ana maelekezo ya kupindisha sheria ili amfunge Mbowe na wenzake
Tukisema katiba mpya ccm wabeza, ila iwe wazi ,nchi ipo gizani ,ukiona mtumiwa anakataa jaji ambae kwa mjibu wa taratibu mtu muhim jiulize Mara mbili ,thanks my chair man
 
Makamanda tusilie bali tusonge mbele kwani mda si mwingi Mungu anaenda kutufurahisha tena 👋👋👋
 
Wew ni mjinga usio jielewa. Ushahidi gani unao taka zaidi ya huu jaji kakubali hati ya mashitaka ni batili halafu anakataa kufuta kesi? Upo ushahidi wa aaina nyingi wew Kibwetele kama hujui. Huu alio toa Mbowe ni ushahidi wa kimazi gira na unaweza kumtia MTU hatiani.

Mabishano ya Mawakili yalikuwa
kujua je Hati ya Mashitaka ni batili au sio batili? Mawakili wa utete walileta ushahidi kuonesha hati ni batili na wale wa serikari walileta vielelezo kuonesha hati hiyo ni halali. Baada ya kupitia hoja za pande zote mbli, Jaji kakubaliana na hoja za mawakili wa Mbowe kuwa hati ni batili hivyo kilicho kuwa kinafuata ni yeye kuifuta kesi.
 
Back
Top Bottom