Jaji Francis Mutungi atangaza kuzuia Mikutano na Makongamano ya Vyama vya Siasa kwa muda kutafuta suluhu

Jaji Francis Mutungi atangaza kuzuia Mikutano na Makongamano ya Vyama vya Siasa kwa muda kutafuta suluhu

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Msajili wa milele wa vyama vya siasa Tanzania,

Francis Mutungi amekubali kutumika hadharani na CCM baada ya kutoa Tangazo la kukataza makongamano ya vyama vya siasa , kwa maelezo kwamba wanasiasa wasubiri kwanza kikao na IGP katika tarehe isiyojulikana.

Kwa wasiojua katiba ya nchi, Francis Mutungi kama mtu binafsi au kama Msajili wa vyama vya siasa HANA, HAJAWAHI KUWA NA HATOKUJA KUWA NA MAMLAKA YA KUZUIA MIKUTANO YA KISIASA WALA MAKONGAMANO, hili si jukumu lake

----
Mutungi.jpg

PICHA: Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Jaji Francis Mutungi, amevitaka vyama vya siasa nchini kusimamisha makongamano na mikutano ya kisiasa kwa muda ili kupisha mazungumzo baina ya vyama vya Siasa, Polisi na Ofisi ya Msajili ili kutafuta suluhu ya mikutano na makongamano.

Jaji Mutungi ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam na kwamba katika kipindi hiki cha kuelekea mazungumzo hayo ni vyema vyama vikasitisha makongamano na mikutano ya kisiasa mpaka hapo mazungumzo yatakapo fanyika ili kuondoa sintofahamu iliyoibuka baada ya polisi kudaiwa kuingilia mikutano ya kisiasa.

Hatua hiyo imekuja baada ya siku za hivi karibuni Chama cha NCCR- Mageuzi kilinukuliwa kikilalamikia kuzuiwa na Jeshi la Polisi kufanya mkutano wa Kamati Kuu katika eneo la Msimbazi baada ya Polisi hao kuvamia mkutano huo.

PIA SOMA
1. Polisi wasambaratisha kikao cha Kamati Kuu ya NCCR-Mageuzi
2. ACT Wazalendo: Tunalaani vikali kitendo cha Jeshi la Polisi kuvamia na kuzuia Kikao cha Kamati Kuu ya NCCR Mageuzi
3. Kyela: Polisi wazuia kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa Chadema
4. Musoma: Polisi Wazingira ofisi ya CHADEMA kulikopangwa kufanyika kongamano la Katiba Mpya
 
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Jaji Francis Mutungi, amevitaka vyama vya siasa nchini kusimamisha makongamano na mikutano ya kisiasa kwa muda ili kupisha mazungumzo baina ya vyama vya Siasa, Polisi na Ofisi ya Msajili ili kutafuta suluhu ya mikutano na makongamano.

Jaji Mutungi ameeleza kushtushwa na kitendo cha polisi kujazana na mabomu katika kila mkutano wa chama cha siasa nchini jambo linaloleta taswira hasi kuwa hali ya kisiasa nchini si shwari wakati si kweli.

Chanzo: ITV
 
Tunajenga uchumi kwanza kwa sasa, kipindi hiki kigumu ambapo uchumi wa dunia nzima umeshuka! Hivi saa hizi uene nchi kama India au USA uwaambie kipaumbele chako ni katiba mpya si watakuona chizi!!

Dunia nzima inahangaika inajikomboa vipi na hili janga nyie mnataka kipaumbele cha taifa kiwe katiba mpya! Kila jambo litafanyika, ila kwa wakati muafaka, muwe mnajua kusoma alama za nyakati na kubadilika
 
Suluhu ipi? Kwani vyama vya siasa kuna sheria au katiba wamevunja? Kama Polisi wanavunja katiba si washughulikiwe kwa mujibu wa sheria?Yaani Polisi wakivunja sheria au katiba dawa ni kutafuta suluhu?

Halafu huyo msajili wa vyama vya siasa anaongea kama NANI akitumia SHERIA ipi? This man is a professional fool!
 
Kwani nyie bavicha mnataka makongamano ya nini wakati kuna corona?
 
Tamko hili likapingwe mahakamani ni kinyume na katiba.

Cc;
- Mkiti wa TCD Zitto Kabwe.
- Rais TLS
- Mawakili wa Chadema
 
Msajili wa milele wa vyama vya siasa Tanzania , Francis Mutungi amekubali kutumika hadharani na ccm baada ya kutoa Tangazo la kukataza makongamano ya vyama vya siasa , kwa maelezo kwamba wanasiasa wasubiri kwanza kikao na IGP katika tarehe isiyojulikana .

Kwa wasiojua katiba ya nchi , Francis Mutungi kama mtu binafsi au kama Msajili wa vyama vya siasa HANA , HAJAWAHI KUWA NA HATOKUJA KUWA NA MAMLAKA YA KUZUIA MIKUTANO YA KISIASA WALA MAKONGAMANO , hili si jukumu lake

----
View attachment 1926218
Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Jaji Francis Mutungi, amevitaka vyama vya siasa nchini kusimamisha makongamano na mikutano ya kisiasa kwa muda ili kupisha mazungumzo baina ya vyama vya Siasa, Polisi na Ofisi ya Msajili ili kutafuta suluhu ya mikutano na makongamano.

Jaji Mutungi ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam na kwamba katika kipindi hiki cha kuelekea mazungumzo hayo ni vyema vyama vikasitisha makongamano na mikutano ya kisiasa mpaka hapo mazungumzo yatakapo fanyika ili kuondoa sintofahamu iliyoibuka baada ya polisi kudaiwa kuingilia mikutano ya kisiasa.

Hatua hiyo imekuja baada ya siku za hivi karibuni Chama cha NCCR- Mageuzi kilinukuliwa kikilalamikia kuzuiwa na Jeshi la Polisi kufanya mkutano wa Kamati Kuu katika eneo la Msimbazi baada ya Polisi hao kuvamia mkutano huo
Hii kwa kinyakyusa tunaita Herding behavior, an occurrence of thoughtful people suspending their individual reason, because of a self-Absorbed group or fear. Ni tabia ya kikundi fulani kudhani wanaweza kufikiri vizuri kuliko wanao waongoza
 
Back
Top Bottom