Msajili wa milele wa vyama vya siasa Tanzania , Francis Mutungi amekubali kutumika hadharani na ccm baada ya kutoa Tangazo la kukataza makongamano ya vyama vya siasa , kwa maelezo kwamba wanasiasa wasubiri kwanza kikao na IGP katika tarehe isiyojulikana .
Kwa wasiojua katiba ya nchi , Francis Mutungi kama mtu binafsi au kama Msajili wa vyama vya siasa HANA , HAJAWAHI KUWA NA HATOKUJA KUWA NA MAMLAKA YA KUZUIA MIKUTANO YA KISIASA WALA MAKONGAMANO , hili si jukumu lake
----
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Jaji Francis Mutungi, amevitaka vyama vya siasa nchini kusimamisha makongamano na mikutano ya kisiasa kwa muda ili kupisha mazungumzo baina ya vyama vya Siasa, Polisi na Ofisi ya Msajili ili kutafuta suluhu ya mikutano na makongamano.
Jaji Mutungi ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam na kwamba katika kipindi hiki cha kuelekea mazungumzo hayo ni vyema vyama vikasitisha makongamano na mikutano ya kisiasa mpaka hapo mazungumzo yatakapo fanyika ili kuondoa sintofahamu iliyoibuka baada ya polisi kudaiwa kuingilia mikutano ya kisiasa.
Hatua hiyo imekuja baada ya siku za hivi karibuni Chama cha NCCR- Mageuzi kilinukuliwa kikilalamikia kuzuiwa na Jeshi la Polisi kufanya mkutano wa Kamati Kuu katika eneo la Msimbazi baada ya Polisi hao kuvamia mkutano huo.
PIA SOMA
1.
Polisi wasambaratisha kikao cha Kamati Kuu ya NCCR-Mageuzi
2.
ACT Wazalendo: Tunalaani vikali kitendo cha Jeshi la Polisi kuvamia na kuzuia Kikao cha Kamati Kuu ya NCCR Mageuzi
3.
Kyela: Polisi wazuia kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa Chadema
4.
Musoma: Polisi Wazingira ofisi ya CHADEMA kulikopangwa kufanyika kongamano la Katiba Mpya