GE2025 Jaji Hamidu Mwanga akataa kujitoa kwenye kesi ya CHADEMA

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Wahuni wanasema ..hata ukikaza kalio sindano ya dokta huingia hivyo hivyo😀, naye mwisho wake waja
 
Chadema wamecheza ngoma ambayo itawamaliza.Tatizo hawana dola
 
Sheria zetu zina mashimo mengi sana..
 
Mimi leo nina swali la kijinga jinga; kwa sababu sheria ekee ninayo ijuwa ni inayoitwa 'common sense'; hizi za vitabuni sizijui.

Kwa hiyo naomba wasomi wa sheria wanisaidie jibu hapa:

Hawa CHADEMA na viongozi wao walipewa "HUKUMU", (hata kabla ya kesi yao kusikilizwa na kuamliwa?)
kwamba wasijishughulishe na shughuli za chama?; au kisiasa? hadi kesi itakapo amriwa?
Haya niliyo andika haa ni sawa?

Kama ni sahihi, CHADEMA wanaokwenda mahakamani kushughulikia hizi kesi zao hawakiuki amri ya kutofanya shughuli za chama?
Kuwepo kwa kesi hii mahakamani; hii siyo kama CHADEMA wamefutwa kuwa chama cha siasa Tanzania?
Wakitaka kushiriki kwenye uchaguzi ujao, wataruhusiwa vipi iwapo wamefungwa na hii kamba ya Mheshimiwa Hamidu?

Naomba tu jibu kwa anayejuwa.
 
Uzoefu unaonesha kwamba ni majaji wachache sana ambao hukubali kujitoa. Mara nyingi majaji ambao wako inclined kujitoa huwa wana hulka ya kuwa very fair. Kwahiyo, hata huwa hakuna haja ya kuwataka wajitoe!
 
Hivi kwanini viongozi wa Chadema kila wakishindwa majukumu yao sababu ni Mbowe.
Kwani hii kesi inatokana na uongozi wa nani, siyo Mbowe?
Hizo mali kugawanywa haikuwa wakati wa Mbowe.

Viongozi wa CHADEMA tokea wachukue uongozi hawajashindwa majukumu yoyote, mbali ya kushindana na vikwazo wanavyo wekewa na huyo huyo Mbowe na washirika wake; halafu unakuja haPa na kudai "wakishindwa majukumu"!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…