tucker carlson
Senior Member
- Oct 5, 2025
- 182
- 759
Yaani kwa alichokisema huyu baba kwenye hii video na kinachoendelea ni kwamba TANZANIA HATUNA BUNGE
-----------------------------------
Aliyekuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Prof. John Ruhangisa, amesisitiza kuwa ni wajibu wa kisheria na kikatiba kwa wabunge kurudi kwa wananchi waliowatuma ili kushauriana nao kabla ya kuchangia au kupitisha sheria bungeni.
Akizungumza huku akionyesha kijitabu cha Katiba, Prof. Ruhangisa amefafanua kuwa mbunge hasimami bungeni kwa ajili ya mawazo yake binafsi, bali anawakilisha sauti na matakwa ya wananchi wa jimbo lake.
"Kuingia bungeni lazima uwe unaridhia ya wananchi, ili utakaposimama kusema, liwe kweli. Na kiuhalisia, wabunge wanatakiwa ku-consult, wanatakiwa kurejea kwenda kule kwa wananchi:
'Jamani, ninyi wananchi mlioruhusu mliolituma bungeni, kuna sheria hii na hii na hii inataka kufanya hivi na hivi, mnasemaje? Maoni yenu ni yapi?' Ili mimi nikienda kule, niongee mawazo yenu, kwa sababu hamtakuwa ninyi nyote ila mimi nitakuwepo kwa niaba yenu
Hapo sasa, swali lipo. Ndio utakalojiuliza wewe, je, wabunge wanaposimama kuongeea bungeni, wanakuwa kweli wametumwa waliyoyawaongea? Wanaoyofanya ni jambo moja, waliyotumwa au kwa mujibu wa sheria ni jambo jingine.
Wawe hawafanyi lakini wajibu ni huo, lazima wawe wanaridhia ya watu. Huwezi ukaongeea mambo ambayo hujawa-consult watu. Je, kama uliyoongea sio wanayotaka? Na wao hawana fursa ya kwenda pale, unakuwa umewa... sariti"