Jaji kufanya uchambuzi wa kurasa 1,500 ukaweza kutoa hukumu kwa siku mbili ni jambo lisilowezekana

Hakuna unalolijua dada/bro . Bora kuwa na mwenyekiti Mbowe kuliko waunga juhudi mkono.

Chacha wangwe alipata ajali , vinginevyo isaidie polisi kwa vile jinai haifi. Zito ndiyo huyo anampiganie Mbowe na kumlilia kama kaka mlezi. Kifupi huna hoja. Umekaririshwa propaganda za lumumba. Huku family za watawala humo wanajirundikia vyeo na mamlaka.

Kama huwezi kusoma hata kuona huwezi ?!
 
Wasiwasi wako tu. Labda angesema Kilatini "prima facie" ungeelewa zaidi. Hii ni kesi ya ugaidi si ya uzururaji au kuiba kuku wa Mpare.
So kama ya ugaidi, inamaana anayehisiwa ni kusulubiwa TU bila kujali haki ilipo sio au yapi mawazo wako . 🤔.
 
Hata wewe ulitetewa Ile awamu uliyokuwa mwimba panbio nashuhuri, Leo hii unajidai kusahau.
 
Hiyo ni dhahiri Jaji amepewa maagizo hiyo kesi aifute!!!
Hivi jaji ana mamlaka ya kufuta kesi kweli?
Mbona mnaandika kishabiki sana,kwa nini msisubiri tu tamati ifike tujue mbivu na mbichi?
 
Mkuu aisee unafuatilia haswa..
kuna siku kulikuwa na case ndani ya case.. kuna swali Kibatala alimuuliza shahidi.., Mawakili wa Serikali wakajaribu kupiga kelele lisiulizwe.. ubishi ukatokea Jaji akawaita ofisini wakaongea kiutu uzima.
Waliporudi Kibatala akauliza mambo tofauti kabisa.. Sijui huko ofisini wanapatanishwa au kuna kitu gani
 
wafuasi wa Gaidi wao wanacho taka kusikia ni kuwa Gaidi yuko Huru basi hapo watafurahi na kumsifia Jaji kinafiki.

lkn endapo Gaidi atakutikana na Kesi ya kujibu wataanza kejeli zao na matusi juu!! hawa wafuasi hawana tofauti na "machokoraa" hawaamini wala sio watu wa kuwachekea au kuwafuatisha.

Nashauri Jaji afanye kazi yake bila kubabaishwa na hili kundi la kihuni la Mboe, asikubali kuyumbishwa na kejeli na matusi, kamwe hawezi kuwaridhisha "macholoraa"

Gaidi lazima ajibu kesi inayo mkabili, msaliti mkubwa huyu.
 
Mkuu hakimu/judge akisikiliza kesi na hasa hizo zenye interest huwa anaielewa kesi yote mwanzo mwisho. Hivyo majibu ya maamuzi madongo (ruling) anayajua hata kabla ya kulisoma jalada.
 
Anakuja tuu kusema maamuzi ila yashapangwa b4
 
Kwa taarifa yako uchomaji moto ni jinai ya kufungwa maisha. Hata mwanafunzi wa shule ya msingi aliyeshiriki kuchoma moto Kituo cha Polisi Sitaki Shari naye alifungwa maisha.
 
Hii kesi imefanya Tanzania iwe suspended kuhusiana na Special Drawing Rights hivyo ina athari kwa uchumi wa nchi ila wapumbavu hawalijui hilo.
 
Niliwahi kubadilisha kitabu cha Anson's Law of Contract kiwe cha sauti ili kumsaidia mtu mwenye changamoto ya kuona aweze kukisikiliza.

Kitabu hiki kina kurasa 800+
Nilipobadilisha kuwa audio kilikuwa na urefu wa masaa 23.
software nilizotumia ni ivona na pistonsoft.

Kwa hiyo kwa kusoma tuu kama kasuku mfululizo bila kupumzika page 1500 zitachukua kati ya masaa 44.
 
Hukumu ilishatolewa kwenye mahijiano ya BBC SWAHILI
 
Hivi ni kweli wewe hili shauri unahitaji muda mrefu kupitia makabrasha ya kesi??
Mashahidi wenyewe washakiri kuwa watuhumiwa hawakushuhudiwa wakipanga au wakifanya vitendo vya kigaidi?
Jaji kaombwa mwenendo wa kesi. Hataki! Jaji kaombwa basi utetezi wapewe nafasi wafanye wasilisho kwa mdomo. Hataki!
Badala yake kawaita mawakili faragha! Which means: Wanaficha aibu ya Jamhuri! In short
"There is No Case To Answer..."

NB: Labda wamfunge Mbowe kwa hila na ubabe.
 
Kawaida Judge wakati case inaanza anatunga maswali. Kwa mfano:
1. Hivi kwa aina ya case ya ugaidi kunahitajika vikao vingapi kupanga kufanya ugaidi? Je prosecution walileta ushahidi usio na shaka?
2.Kunahitajika idadi ya wataalam wangapi na watu wangapi wanaoweza kufanya Tanzania isitawalike kuanzia Kagera, Mtwara, Mbeya na Arusha? Je ushahidi uliwaonyesha?
3. Kwa aina ya case ya ugaidi na ukubwa wa Tanzania ili kufanikisha inahitajika vilipuzi, silaha na watendaji wangapi kufanikisha? Je ushahidi wa prosection wa basola moja na risasi tatu uma m move judge au mtu wa kawaida kuamini hivyo?
4. Kama walipanga kukata miti kuanzia Morogoro mpaka Mbeya, je kuna vifaa vya aina hiyo na watu walotayarishwa na ushahidi kuonekana?
5. Taarifa ya kumwambia Rais kama kiongozi wa nchi kwamba Mbowe alitoroka nchi na kwamba wenziwe tayari walishahukumiwa kifungo, lengo la kumdanganya Rais na kumdhalilisha dunia nzima lilikuwa nini? Bahati mbaya wakiomdanganya ndio haohao waliotakiwa kuleta ushahidi.
6. Je nini kilikuwa nyuma ya kufungua jalada la upelelezi la Mbowe bila kwanza kupokea maelezo ya DCI kama mlalamikaji mkuu?
7. Nini kimemuogopesha mlalamikaji mkuu DCI kutoa ushahidi mahakamani?
8. Kwa nini kuna inconsistencies, mfano wapo waliosema watuhumiwa walikamatwa saa 5 na wapo wanaosema saa 7 mchana...
9. Kitu gani kilifanya zoezi hili zima kuwahusisha kabila za rais JPM au wasukuma dhidi ya kabila rais alilolichukia la wachagga?
10. Kwa nini Kingai aliyekuwa Arusha ndie aliyeshughulika na jambo hili ambapo hata wapelelezi walikuwa wanapokea maagizo toka kwake bila wao kuwa na independent verification...kwamba Kingai ndie alisema.
11. Credibility na sincerity ya mashahidi kama Jumanne ambaye alikuwa na tuhuma za kumbanbikia case ya meno ya Tembo Mzee wa miaka 80 Maeda kule Arusha ambaye alikuwa mshauri wa mwalimu Nyerere wa mambo ya siasa na kumuibia mamilioni ya pesa! Huyo Urio je yuko detension na ndiko anakotokea?
12. Wote walioshughulika na hii case ya Mbowe walipewa vyeo kwa maana ya promortion. Je ni kweli wao pekee walistahili au walikuwa wamelipwa na Rais kwa kazi nzuri ya kum fix mpinzani mkuu wa chama cha rais? TISS walisaidia kiasi gani na wao walizawadiwa nini?
13. Mashahidi wengi ni polisi. Je sifa ya jeshi hilo inamfanya judge awaamini moja kwa moja wanachosema hata kama kuna mikanganyiko ya kutosha?
14. Sabaya factor: Kina Mbowe walituhumiwa kutaka kudhuru viongozi wa serikali. Akiyetajwa pekee ni Sabaya. Yeye alikuwa na significance gani katika viongozi wakuu ukizingatia ni DC tu! Bahati mbaya mwenyewe alikuja kupatikana na hatia za ki criminal nyingi zaidi ya nyingi. Kwa hiyo ushahidi wake haupo na ni muhalifu mkuu. Nini role ya Sabaya angekuwepo kutoa ushahidi? Jambo gani lilikuwa nyuma?
15. Mwisho, ni nini kimefanya madhahidi wa Jamhuri kuwa 13 badala ya 24? Je kuna uasi umetokea chini kwa chini? Je kufariki kwa JPM kumewarudisha watu kwenye UKWELI? Je kufungwa Sabaya kumetisha waongo? Je yanayomzunguka Makonda yameleta kusita kukuu kwa mashahidi ? ...na MENGINE MENGI. .ambayo hata Judge hatayakimbia maana naye ni mwanadamu, ana mwili na roho, ana watoto na pengine wajukuu na zaidi atakuwa anajua ana kesho yake mbele za Mungu kwa imani yake. Siamini kama atafanya mambo kumfurahisha yoyote kama alivyofanya JPM, Makonda, Sabaya , yule DC aliyeharibu mazao ya Mbowe Hai au yule m TRA aliyechoma vifaranga toka Kenya kwa petrolo...kuwataja hao wachache.
16. Nini kitajiri ikiwa kina Mbowe watatakiwa kutoa ushahidi waziwazi na consequences zake locally-hasa vyombo vitukufu vya serikali kama majeshi yetu nk and internationally na tayari tumeambiwa jinsi watuhumiwa walivyoshindia uji tu siku zote waliookuwa mahakamani na bado mkuu wa magereza yuko kazini? MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
A robotized human-being may be! To be one of the world-wonders.
 

..ndani ya ccm kuna hofu hakuna demokrasia.

..hakuna anayeweza kumchallenge mwenyekiti halafu vyombo vya dola visimshughulikie.
 
hukumu tayari anayo tangu day 1, mengine yote ni maigizo tupu, hawezi kupigana na wajiri wake Mbowe lazima afungwe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…