Kawaida Judge wakati case inaanza anatunga maswali. Kwa mfano:
1. Hivi kwa aina ya case ya ugaidi kunahitajika vikao vingapi kupanga kufanya ugaidi? Je prosecution walileta ushahidi usio na shaka?
2.Kunahitajika idadi ya wataalam wangapi na watu wangapi wanaoweza kufanya Tanzania isitawalike kuanzia Kagera, Mtwara, Mbeya na Arusha? Je ushahidi uliwaonyesha?
3. Kwa aina ya case ya ugaidi na ukubwa wa Tanzania ili kufanikisha inahitajika vilipuzi, silaha na watendaji wangapi kufanikisha? Je ushahidi wa prosection wa basola moja na risasi tatu uma m move judge au mtu wa kawaida kuamini hivyo?
4. Kama walipanga kukata miti kuanzia Morogoro mpaka Mbeya, je kuna vifaa vya aina hiyo na watu walotayarishwa na ushahidi kuonekana?
5. Taarifa ya kumwambia Rais kama kiongozi wa nchi kwamba Mbowe alitoroka nchi na kwamba wenziwe tayari walishahukumiwa kifungo, lengo la kumdanganya Rais na kumdhalilisha dunia nzima lilikuwa nini? Bahati mbaya wakiomdanganya ndio haohao waliotakiwa kuleta ushahidi.
6. Je nini kilikuwa nyuma ya kufungua jalada la upelelezi la Mbowe bila kwanza kupokea maelezo ya DCI kama mlalamikaji mkuu?
7. Nini kimemuogopesha mlalamikaji mkuu DCI kutoa ushahidi mahakamani?
8. Kwa nini kuna inconsistencies, mfano wapo waliosema watuhumiwa walikamatwa saa 5 na wapo wanaosema saa 7 mchana...
9. Kitu gani kilifanya zoezi hili zima kuwahusisha kabila za rais JPM au wasukuma dhidi ya kabila rais alilolichukia la wachagga?
10. Kwa nini Kingai aliyekuwa Arusha ndie aliyeshughulika na jambo hili ambapo hata wapelelezi walikuwa wanapokea maagizo toka kwake bila wao kuwa na independent verification...kwamba Kingai ndie alisema.
11. Credibility na sincerity ya mashahidi kama Jumanne ambaye alikuwa na tuhuma za kumbanbikia case ya meno ya Tembo Mzee wa miaka 80 Maeda kule Arusha ambaye alikuwa mshauri wa mwalimu Nyerere wa mambo ya siasa na kumuibia mamilioni ya pesa! Huyo Urio je yuko detension na ndiko anakotokea?
12. Wote walioshughulika na hii case ya Mbowe walipewa vyeo kwa maana ya promortion. Je ni kweli wao pekee walistahili au walikuwa wamelipwa na Rais kwa kazi nzuri ya kum fix mpinzani mkuu wa chama cha rais? TISS walisaidia kiasi gani na wao walizawadiwa nini?
13. Mashahidi wengi ni polisi. Je sifa ya jeshi hilo inamfanya judge awaamini moja kwa moja wanachosema hata kama kuna mikanganyiko ya kutosha?
14. Sabaya factor: Kina Mbowe walituhumiwa kutaka kudhuru viongozi wa serikali. Akiyetajwa pekee ni Sabaya. Yeye alikuwa na significance gani katika viongozi wakuu ukizingatia ni DC tu! Bahati mbaya mwenyewe alikuja kupatikana na hatia za ki criminal nyingi zaidi ya nyingi. Kwa hiyo ushahidi wake haupo na ni muhalifu mkuu. Nini role ya Sabaya angekuwepo kutoa ushahidi? Jambo gani lilikuwa nyuma?
15. Mwisho, ni nini kimefanya madhahidi wa Jamhuri kuwa 13 badala ya 24? Je kuna uasi umetokea chini kwa chini? Je kufariki kwa JPM kumewarudisha watu kwenye UKWELI? Je kufungwa Sabaya kumetisha waongo? Je yanayomzunguka Makonda yameleta kusita kukuu kwa mashahidi ? ...na MENGINE MENGI. .ambayo hata Judge hatayakimbia maana naye ni mwanadamu, ana mwili na roho, ana watoto na pengine wajukuu na zaidi atakuwa anajua ana kesho yake mbele za Mungu kwa imani yake. Siamini kama atafanya mambo kumfurahisha yoyote kama alivyofanya JPM, Makonda, Sabaya , yule DC aliyeharibu mazao ya Mbowe Hai au yule m TRA aliyechoma vifaranga toka Kenya kwa petrolo...kuwataja hao wachache.
16. Nini kitajiri ikiwa kina Mbowe watatakiwa kutoa ushahidi waziwazi na consequences zake locally-hasa vyombo vitukufu vya serikali kama majeshi yetu nk and internationally na tayari tumeambiwa jinsi watuhumiwa walivyoshindia uji tu siku zote waliookuwa mahakamani na bado mkuu wa magereza yuko kazini? MUNGU IBARIKI TANZANIA.