Jaji Mgeta: Niliumizwa na Waziri Mkuu kuchana Hukumu ya kesi niliyotoa kuwa kashindwa

Umeshapanic 😂😂
 
KATIBA TU. MHIMILI MMOJA UMEJICHIMBIA ZAIDI UFUKULIWE NA KUNG'OLEWA NDIPO MAMBO YATAKUWA SAWIA. HAPA MAMBO YOTE LAZIMA YASUJUDU MHIMILI ULIOJICHIMBIA. Mfano: Ni dharau kubwa kujipanga msululu kumchagua mgombea na mnauhakika ameshinda halafu anapinduliwa na kuwekwa ambaye MHIMILI uliojichimbia unamtaka sio wananchi. Maneno ya Jaji yanatoa ushahidi WA umuhimu WA mfumo/katiba kuundwa Upya ili mihimili iheshimiane na kudhibitiana.
 
halafu umri wa kustaafu majaji ni miaka mingapi? inaonekana majaji wanao staafu wamezeeka sana!!! Kwa Nini umri wa kustaafu majaji usipunguzwe?!!! maana wamechoka sana!!!
Inaonekana wengi wao umri umesonga sana.

Wanadanganyaga umri
 
Alimchongea kwa prezdaa amle kichwa ili wamwonyeshe kazi, au kama vipi angemchongea kwa mheshimiwa chupika walale naye mbele kule mjengoni......wakishamwondolea cheo basi kwishaaa...
 
Huyu jaji mstaafu kaishi na nyongo kali muda mrefu, amepata nafasi ya kuitema ndio kaitema kwa kumsema huyo waziri mkuua akijua hayupo madarakani na hataweza kumjibu
 
Kwa nini kichwa ni waziri mkuu huku habari inasema ni kigogo aliyechana hukumu. Kama ni waziri mkuu mbona habari haimtaji jina. Tutajie alikua nani?
 
Kumbuka aliyefanya hivyo alikuwa kigogo wa serikali[emoji848]aliwaza mafao yake na penshen yake ya uzeen akaamua kutumia busara kuliacha lipite[emoji1787]he knows the court system is somehow fu.ck.e.d up[emoji1733]
Inasikitisha sana
 
Naomba kutofautiana na wewe..

Kwa maoni yangu naona ni vyema kwanza ingejulikana kama ni kweli kuna huyo kigogo( Waziri mkuu) alichana hukumu ya mahakama? au jaji amejitungia stori?

Jambo la pili tujiulize,kama ni kweli alichana hiyo hukumu,ni jambo sahihi kwa kiongozi yoyote wa serikali kuchana hukumu kama hizo?

Jambo la tatu ni tujiulize,kuchana hiyo hukumu,kiongozi huyo aliidharau Mahakama kama mhimili au alimdharau Jaji husika? ( Maana tunaona aliyeumia ni jaji binafsi na wala siyo mahakama)

Kama hayo yote hapo juu ni kweli,je viongozi uliowaorodhesha hapo juu ukiwa na hofu kuwa iko siku nao watatuhumiwa, je wanayo haki ya kuchana hukumu iliyotolewa na viongozi wa mhimili mwingine?

La mwisho ni kuwa,maoni yako japo nayaheshimu, bali yamejaa ukale wa kuwatukuza viongozi uliowaita wa juu hata kama wakifanya makosa ya wazi,watu wakae kimya tu
 
Tuache kumlaumu jaji mstaafu kutotaja jina la waziri mkuu mstaafu.

Waandishi wa habari za kiuchunguzi wa magazeti na mitandao na raia wenye uchungu Mahakama kutishwa na wanasiasa wa chama tawala CCM waingie mtandaoni ili waweze kupata maamuzi ya kesi husika : Home | Tanzlii


Image

Karibu kwenye Tanzania Legal Information Institute​

TanzLII ni tovuti ya Mahakama ya Tanzania inayochapisha maamuzi, Sheria na Kanuni kwa ufikiaji bure Mtandaoni. TanzLII provides free access to the law of Tanzania and is a member of the African LII community

Judgement database:

Source : Judgments | Tanzlii
 
Hayo maswali yote uliyo yauliza hayana maana kwa wakati huu.

Yalikuwa maswali ya msingi wakati tukio lilipo tokea tu sio sasa.

Jaji alikuwa na malaka ya kisheria ya kuchukua hatua lkn akashindwa kuyatumia!! na kuachilia uhuru wake kuingiliwa na kudharauliwa kama ni kweli!!!! Hii ni stori ya kipuuzi kabisa na inalengo la kumdhalilisha kiongozi aliye tuhumiwa.

Kama alishindwa kuchukua hatua kipindi kile basi ni Bora angeendelea kukaa kimya kuliko alivyo onyesha udhaifu wake leo hii!!!!
 
Hapana. Jata sasa ina msaada. Kama ni Majaliwa, basi hii ni kashfa kubwa kwake, hastahili hata kuwa Waziri Mkuu.
 
Mahakama inahitaji utulivu wa kichwa.

Watu wazima akili zao ziko settled kuliko vijana wenye matamanio ya mambo mengi.

Mgeta alikua poa sana.

Sasa hivi Kuna mahakimu na majaji wadogo ila bado hawajaiva vizuri
Wale walioteuluwa na marehemu, wengi wao hawafai kwa sababu waliteuliwa kwa lengo maalum la kwenda kuua uhuru wa mahakama. Karibia wote walikuwa maafisa wa TISS.

Hata simba, siyo jaji yule. Fikiria afisa wa TISSS anapokuwa msajili.wa mahakama. Yeye ndiye anayepanga kesi gani isikilizwe na jaji gani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…