Jaji Mkuu achukizwa na wapelelezi wanaokamata mtuhumiwa kabla ya kukamilisha upelelezi

Huyu anasema tu, kwa mini asiwaagize mahakimu na majaji kutupilia mbali mikesi isiyoisha

..Jaji Mkuu hatakiwi kuwashinikiza majaji na mahakimu ktk maamuzi yao.

..lakini pia Jaji Mkuu aliwahi kutoa kauli kuwa Mahakama haitatoa ushirikiano kwa wanaharakati.

..Sasa hoja hii ya kupinga wananchi kuwekwa mahabusu muda mrefu huku upelelezi haujakamilika ni hoja ya muda mrefu wa wanaharakati.

..kwa hiyo inafurahisha kwamba Jaji Mkuu ameona mantiki ktk hoja hiyo na ameamua kuiunga mkono.

..Lakini itapendeza na itakuwa jambo la kiungwana kama ataomba radhi kwa kauli zisizopendeza alizowahi kutoa dhidi ya wanaharakati.
 
Yaani uuwe Leo uachwe tu mpaka upelelezi ukamilike mwezi septemba,2019 na wewe unasubiri upelelezi? Utakuwa siyo mtanzania labda.
Na kama una uhakika kauwa sasa unampeleka mahakamani kufanya nini?
 
Huyu Jaji ni mnafiki, na ataingia kwenye vitabu vya historia ya Tanzania kama Jaji ambaye amekuwa 'highly compromised by the exexutive'.

Wananchi tunashangaa kwa nini Polisi wanakamata watu na kuwapeleka Mahakamani wakati upelelezi bado haujakamilika, naye Jaji Mkuu Profesa Juma anashangaa kama wananchi mbali na nguvu za kikatiba alizonazo

Mhimili wake una nguvu kikatiba ya siyo tu kuzifuta kesi hizo bali kuwachukulia hatua Polisi ambao wanakiuka maagizo hayo.
 
Toka sirikale hii imeingia imehakikisha kila ateuliwaye kwenye nafasi nyeti ana utaalamu wa kucheza rhumba hili. Ni kampeni tuuuu kila siku kwenye media jinsi walivyo watakatifu
 
Huyu jamaa ndio jaji mkuu wa kiwango cha chini zaidi kuwahi kutokea nchi hii tangu ipate uhuru
Naheshimu sana mawazo yako!

Naamini wewe pia ni mtu mwenye IQ ya chini kuliko watanzania wote.
Hayo ni maoni yangu,na yametokana na maoni yako.
 
Huyo jaji mkuu ndio msimamizi uovu ili kulinda maslahi yake.
 
Kama DPP alitoa tangazo hilo tangu 2012 mh. Jaji utasemaje ni"bahati mbaya" watu kupelekwa mahakamani kabla ya upelelezi kukamilika?? Huo ni moja ya mifumo iliyotengenezwa makusudi
 
Sasa Jaji Mkuu amechukua hatua gani? Ama ameishia kulalamika tu?
 
unakamatwa kwa shutuma za Uraia unakaa ndani.., wanaona upo safi.., wanaleta shutuma za kutakatisha fedha...., Hii wazee wa zamani wa magharibi ya mbali walikuwa wanaiita witch hunt.....
 
Jaji mkuu hasemi kweli. Kwa sababu mahakama inayo mamlaka kufuta kesi ambazo watuhumiwa wanateseka jela kwa isingizio cha ushahidi unaendelea. Tunafahamu Polisi wanaweza mkamata mtu kwa kumkomoa na kumuweka ndani muda mrefu kwa kisingizio upelelezi haujakamilika. Je mpaka sasa mahakama imeshafuta kesi za namna hii ngapi? Hapa sio polisi wa kulaumiwa bali mahakama
 
Anatakiwa atoe way forward na sio kulalamika. Anamiliki mhimili muhimu

Nionavyo Mimi.
 
Sasa siwawe wanawaachia mpaka waletwe ushahidi ukiwa umekamilika wanashindwa nini? Yeye si ndio mkuu wa mhimili atoe agizo au anaogopa maagizo toka juu.
 
Mahakama kikiwa na mwelekeo huu watanzania wengi watakuja na imani nayo
 
Anatakiwa atoe way forward na sio kulalamika. Anamiliki mhimili muhimu

Nionavyo Mimi.
Dalili ya mvua ni mawingu alichozungumza ni kitu muhumu sana kama ni kweli kinatoka chini ya uvungu wa moyo wa mahakama
 
Jaji mkuu eti naye analalamika tu kwani hajui kuwa kwenye vyesi vya sasa vya uhujumu uchumi, utakatishaji fedha na vinavyohusu wapinzani lengo ni ukomoaji na wala sio kukidhi matakwa ya kisheria.

Kwa ina maana hajui nani yuko nyuma ya hivyo vyesi.
Kwa kusema tu hivyo ni Dira kwa muhimili mzima tena kwa tanzania ya sasa huyu jaji kama kweli anamaanisha anachokisema basi huyu ndio mtu wa kuanza kuombewa na watanzania wote maana kifuatacho ni kuwaachia wote walioshtakiwa kinyume na sheria,ambao kesi zao ni za mda mrefu uchunguzi haujakamilika,kwa kutengenezewa kesi kama mashekhe wa Zanzibar, kabendera,kesi ya kina mbowe,figisu za lisu na ubunge wake n.k binafsi namuona huyu jaji kama ametangaza Vita !!!!!
 
mpaka james Rugemalira na Harbinder Sethi? ina mana hata kina Kitillya pia haikujuzu kukaa ndani kwa muda wote wakati upepelezi unaendelea?
kukaa ndani wakati uchunguzi unaendelea una mantiki gani kwa mtuhumiwa? Kwani akiwa nje uchunguzi hauendi kuendelea? na kama akikaa ndani na mwisho wa siku hana hatia itakuwaje? Tusiwe wepesi kuangalia upande mmoja wa shillingi tuigeuze na kuiangalia upande wa pili unasomekaje, usiombee ovu kwa mwenzio kwani hakuna mwanadamu aliyekamilika chini ya jua sote ni wakosefu
 
Yaani uuwe Leo uachwe tu mpaka upelelezi ukamilike mwezi septemba,2019 na wewe unasubiri upelelezi? Utakuwa siyo mtanzania labda.

Maoni binafsi usiyashabihishe na uraia wa mtu. Gharama za kumtunza 'mtuhumiwa' huko mahabusu nani anazibeba? Niko pale pale...haraka ya nini kama upepelezi haujakamilika?
 
Jaji mkuu wa Tanzania ameshauri wapelezi wa kesi kuharakisha upelelezi wa kesi ndipo mtu akamatwe "Mahakama hazipaswi kulaumiwa kwa msongamano wa watu magerezani bali wapelelezi wa kesi, wapelelezi huchukua muda mrefu kukamilisha upelelezi na sababu wao kuchukua muda mrefu wakati mwingine hazina mashiko" Jaji Mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…