..Jaji Mkuu hatakiwi kuwashinikiza majaji na mahakimu ktk maamuzi yao.
..lakini pia Jaji Mkuu aliwahi kutoa kauli kuwa Mahakama haitatoa ushirikiano kwa wanaharakati.
..Sasa hoja hii ya kupinga wananchi kuwekwa mahabusu muda mrefu huku upelelezi haujakamilika ni hoja ya muda mrefu wa wanaharakati.
..kwa hiyo inafurahisha kwamba Jaji Mkuu ameona mantiki ktk hoja hiyo na ameamua kuiunga mkono.
..Lakini itapendeza na itakuwa jambo la kiungwana kama ataomba radhi kwa kauli zisizopendeza alizowahi kutoa dhidi ya wanaharakati.
Mkuu hoja hii tumeiongelea hapa JF miaka mingi.
Si hivyo tu, tulihoji kwanini watu wakamatwe weekend bila kufikishwa mahakamani katika masaa 24.
Tulihoji sana hivi Polisi inamkataje mtu bila ushahidi wa kutosha?
Kwamba mtu anakamatwa, ushahidi unatafutwa! wapi hili linatokea kwingine
Pili, Jaji aliwahi kusema suala la TL uchunguzi lazima ufanywe na vyombo vya ndani.
Sijui wakati BoT ikiungua alikuwa nchini au nje ya nchi.
Hili lilikuja baada ya shinikizo la wachunguzi wa nje, naye akaingia
Tatu, Jaji anapolalamika inasikitisha. Yeye ni mhimili, hivi amekaa na Wenzake na kutafuta suluhu ya tatizo? Kinachoonekana ni kusema ''mimi sihusiki'' kama Mwana jf yoyote.
Nne, Sugu alipomkataa hakimu hivi haikuwa haki yake?
Jaji alikaa kimya. Nadhani alipaswa atoe neno kuondoa utata, hakutoa.
Yapo mengi inatosha kusema, nafasi si kama ilivyokuwa! viatu ni vikubwa