Jaji Mkuu achukizwa na wapelelezi wanaokamata mtuhumiwa kabla ya kukamilisha upelelezi

Jaji Mkuu achukizwa na wapelelezi wanaokamata mtuhumiwa kabla ya kukamilisha upelelezi

Jaji mkuu wa Tanzania ameshauri wapelezi wa kesi kuharakisha upelelezi wa kesi ndipo mtu akamatwe "Mahakama hazipaswi kulaumiwa kwa msongamano wa watu magerezani bali wapelelezi wa kesi, wapelelezi huchukua muda mrefu kukamilisha upelelezi na sababu wao kuchukua muda mrefu wakati mwingine hazina mashiko" Jaji Mkuu
Kama wangelifanyia kazi hilo invekuwa njema sana. Maana akina malinzi waliingia ndani 2017 miezi ya tano au sita, ila upelelezi umekamilika katikati ya mwaka huu. Sasa kama mkigundua kwamba hana hatia mtamlipa kwa muda mwingi mliomkalisha mahabusu mtuhumiwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kazungumza maneno ya kwenye majukwaa na sio hali halisi.Kama anadhamira na kweli anasali aanzishe mchakato wa kubadili baadhi ya sheria za kikoloni.Nchi zote isipokuwa za kidikteta kesi zote zinadhaminika isipokuwa murder.
Uhujumu uchumi ni fimbo ya kuwatesea wasio na chapa kwenye paji la uso.Ila Maisha ni upepo milango ya jela watakayotokea wenzao ndio watakayoingilia maana jela haina mwenyewe.
 
Tatizo mhimili huu wa Mahakama umepotezwa na mhimili wa dola.

Nchi zilizo na mihimili huru, Mahakama ikitoa dhamana kwa mtuhumiwa inatakiwa vyombo kama Polisi, TAKUKURU kuheshimu uamuzi wa Mahakama. Sana sana Polisi wanaweza kumtaka mtuhumiwa kuripoti Polisi kila mara kusaidia upelelezi ukamilike na siyo kumrundika mahabusu mtuhumiwa.

Mahakama kupitia kwa Jaji Mkuu watakuwa watu wa kulalamika mpaka lini juu ya suala hili la kikatiba?

Jaji Mkuu wa Tanzania aige wenziwe wa nchi za Jumuiya ya Madola kukataa kuburuzwa au kuomba Hisani na kusimama kidete kama Prof. Assad Mussa GAG au Jaji Mkuu wa Kenya Mh. David Maraga kuonesha kwa Vivendi kusimamia utawala wa sheria na Katiba

Jamhuri Day 12. December 2019
Jaji Mkuu Kenya akataa unyonge

Jaji Mkuu David Maraga asusia hafla kuonesha kuchoshwa na vitendo vya dola / serikali kubinya bajeti za Mahakama na uingiliaji wa shughuli za mhimili huu unaofanywa na watendaji wa serikali.

November 4, 2019

Ati mwasema Kumbe Kenya ina wenyewe ?
- Jaji David Maraga aidindia serikali na Bunge

Oktoba 28, 2019
Mahakama nchini Kenya zachechemea kwa kubinywa bajeti yake, huku idara zingine za serikali hazipitiwi na panga la kupunguza bajeti. Hii ni jinsi msuguano kati ya mhimili wa Mahakama na mhimili wa dola ilivyo, ila kuna nchi mhimili wa Mahakama haukubali kuwa nyonge mbele ya mhimili wa dola au Bunge.

August 20, 2019
Mahakama yaitaka mihimili ya Bunge na Dola kuongeza pesa za Mahakama

Mahakama yaitaka serikali kuongeza bajeti ya Idara hiyo muhimu ya kuamua haki nchini Kenya

July 30, 2019
Chama cha Mahakimu na Majaji nchini Kenya chaja juu kutokana na mwenendo wa mhimili wa dola / serikali kuu kuiburuza Idara hiyo nyeti inayounda Mihimili muhimu ya uendeshaji nchi. Hii ni kufuatia mihimili ya Bunge na Dola / Serikali kushutumiwa vikali na Jaji Mkuu wa Kenya Mh. David Maraga kutokana na 'njama' zao kutaka kudhoofisha mhimili wa Mahakama
 
Kazungumza maneno ya kwenye majukwaa na sio hali halisi.Kama anadhamira na kweli anasali aanzishe mchakato wa kubadili baadhi ya sheria za kikoloni.Nchi zote isipokuwa za kidikteta kesi zote zinadhaminika isipokuwa murder.
Uhujumu uchumi ni fimbo ya kuwatesea wasio na chapa kwenye paji la uso.Ila Maisha ni upepo milango ya jela watakayotokea wenzao ndio watakayoingilia maana jela haina mwenyewe.
awamu hii alama kwenye paji la uso ni muhimu sana kama hutaki shida
 
Kama wangelifanyia kazi hilo invekuwa njema sana. Maana akina malinzi waliingia ndani 2017 miezi ya tano au sita, ila upelelezi umekamilika katikati ya mwaka huu. Sasa kama mkigundua kwamba hana hatia mtamlipa kwa muda mwingi mliomkalisha mahabusu mtuhumiwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Uliona wapi kesi za kubambikwa ushahidi ukakamilika kwa wakati?
Lengo la kukaa ndani bila ushahidi eti unanyooshwa then ukishanyooshwa what next,tupo sawa na uncivilized and uneducated japo tumepita shule
 
Jaji mkuu wa Tanzania ameshauri wapelezi wa kesi kuharakisha upelelezi wa kesi ndipo mtu akamatwe "Mahakama hazipaswi kulaumiwa kwa msongamano wa watu magerezani bali wapelelezi wa kesi, wapelelezi huchukua muda mrefu kukamilisha upelelezi na sababu wao kuchukua muda mrefu wakati mwingine hazina mashiko" Jaji Mkuu
Waambie jeshi la polisi wanaotupeleka lockup week nzima na kutuachia bila kosa.
Je? Huo muda tulioupoteza wataufidia vipi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tujifunze kwa wenzetu ushahidi kwanza unakamilishwa ndipo ukamatwa mtu haizidi mwezi anahukumiwa.Kwetu wawezakaa mahabusi hata miaka 7 easy tu then hukumu ikitoka unafungwa let say miaka 2 tena.Kwann usiachiwe huru sababu ushatumikia mahabusu miaka saba?.Maana kama lengo ni kumyoosha si tayari ashakaa mahabusi.Yapaswa tufanye mambo kama watu walioelimika na kustaarabika hata umkomoe vipi mwenzie aitokuongezea siku za kuishi.
 
Kuna wachache wanatuharibia ustawi na umoja wa taifa letu. Kuna wajinga walitamani Mbowe na wenzake wawe jela wasishiriki hata chaguzi za ndani ya chama chao kwa kesi na shauri tata.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jaji mkuu wa Tanzania ameshauri wapelezi wa kesi kuharakisha upelelezi wa kesi ndipo mtu akamatwe "Mahakama hazipaswi kulaumiwa kwa msongamano wa watu magerezani bali wapelelezi wa kesi, wapelelezi huchukua muda mrefu kukamilisha upelelezi na sababu wao kuchukua muda mrefu wakati mwingine hazina mashiko" Jaji Mkuu

Jaji mkuu wewe ni mwanasheria nguli. Haki za msingi za watuhumiwa zinapaswa kulindwa. Yaondolewe mazingira yanayotia shaka kuwa pana kukomoana. Wewe ni mkuu wa Mahakama. Tendea haki ukuu wa mhimili kwako - hii kwa mujibu wa Katiba.
 
Kama jaji mkuu anaburuzwa kila hafla ya rais hata kuzindua kisima cha maji, ataweza kusimamia haki kweli? Yeye kashakubali kuburuzwa atii tu ili mlo wake ujae vizuri kwenye sahani. Hii kauli yake ni furahisha genge.

Mfano muafaka kabisa wa kuonesha unyonge wa Mhimili wa Mahakama. Jaji Mkuu wa Tanzania aache kuomba hisani au kulalama bali awachukulie hatua maafisa wanaokiuka haki za msingi za watuhumiwa kwa kuwafunga maafisa wakaidi wa idara ya polisi.
 
Back
Top Bottom