Tatizo mhimili huu wa Mahakama umepotezwa na mhimili wa dola.
Nchi zilizo na mihimili huru, Mahakama ikitoa dhamana kwa mtuhumiwa inatakiwa vyombo kama Polisi, TAKUKURU kuheshimu uamuzi wa Mahakama. Sana sana Polisi wanaweza kumtaka mtuhumiwa kuripoti Polisi kila mara kusaidia upelelezi ukamilike na siyo kumrundika mahabusu mtuhumiwa.
Mahakama kupitia kwa Jaji Mkuu watakuwa watu wa kulalamika mpaka lini juu ya suala hili la kikatiba?
Jaji Mkuu wa Tanzania aige wenziwe wa nchi za Jumuiya ya Madola kukataa kuburuzwa au kuomba Hisani na kusimama kidete kama Prof. Assad Mussa GAG au Jaji Mkuu wa Kenya Mh. David Maraga kuonesha kwa Vivendi kusimamia utawala wa sheria na Katiba
Jamhuri Day 12. December 2019
Jaji Mkuu Kenya akataa unyonge
Jaji Mkuu David Maraga asusia hafla kuonesha kuchoshwa na vitendo vya dola / serikali kubinya bajeti za Mahakama na uingiliaji wa shughuli za mhimili huu unaofanywa na watendaji wa serikali.
November 4, 2019
Ati mwasema Kumbe Kenya ina wenyewe ? - Jaji David Maraga aidindia serikali na Bunge
Oktoba 28, 2019
Mahakama nchini Kenya zachechemea kwa kubinywa bajeti yake, huku idara zingine za serikali hazipitiwi na panga la kupunguza bajeti. Hii ni jinsi msuguano kati ya mhimili wa Mahakama na mhimili wa dola ilivyo, ila kuna nchi mhimili wa Mahakama haukubali kuwa nyonge mbele ya mhimili wa dola au Bunge.
August 20, 2019
Mahakama yaitaka mihimili ya Bunge na Dola kuongeza pesa za Mahakama
Mahakama yaitaka serikali kuongeza bajeti ya Idara hiyo muhimu ya kuamua haki nchini Kenya
July 30, 2019
Chama cha Mahakimu na Majaji nchini Kenya chaja juu kutokana na mwenendo wa mhimili wa dola / serikali kuu kuiburuza Idara hiyo nyeti inayounda Mihimili muhimu ya uendeshaji nchi. Hii ni kufuatia mihimili ya Bunge na Dola / Serikali kushutumiwa vikali na Jaji Mkuu wa Kenya Mh. David Maraga kutokana na 'njama' zao kutaka kudhoofisha mhimili wa Mahakama