Pulchra Animo
JF-Expert Member
- Jun 16, 2016
- 3,718
- 3,465
10 September 2021
Mahabusu na wafungwa wamuelezea Jaji M.M. Siyani
Source: Mubashara Studio
Kwa nini wanafunzi wa elimu ya msingi wanavaa sale?Kwanini majaji wa Tanzania wanavaa kama majaji wa enzi za ukoloni? Sasa utakuta USA jaji anavaa suti tu.
Lunatic [emoji2957][emoji2957][emoji2957]
mmeanza WANGA
Kwa ufupi sana Jaji huyu Mustapha Mohamed Siyani aliapishwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu kanda ya Dodoma siku ya Ijumaa tarehe 20 April 2018, na Aliyekuwa Rais wa Tanzania wa awamu ya 5 Dr John Magufuli, Baada ya kuteuliwa kushika nafasi hiyo tarehe 15 April 2018 .
Pia amewahi kuwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma.
NOTE : Jaji wa Mahakama Kuu ni mtumishi wa Umma, kumfahamu haijawahi kuwa kosa kisheria
Kwa ufupi sana Jaji huyu Mustapha Mohamed Siyani aliapishwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu kanda ya Dodoma siku ya Ijumaa tarehe 20 April 2018, na Aliyekuwa Rais wa Tanzania wa awamu ya 5 Dr John Magufuli, Baada ya kuteuliwa kushika nafasi hiyo tarehe 15 April 2018 .
Pia amewahi kuwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma.
NOTE : Jaji wa Mahakama Kuu ni mtumishi wa Umma, kumfahamu haijawahi kuwa kosa kisheria
Tusaidie jaji anateuliwa vipi?Tatizo sio judge kwamba ni muadilifu au sio, tatizo ni mfumo unatumika kumchagua na kumuapisha huyo judge..mfumo ndio root of all evil...huyu na aliepita wote wamechaguliwa na mfumo ule ule....as a person anaweza akawa mtu muadilifu kweli anaependa haki na kuona haki inatendeka...but kwa mfumo ulipo sasa na kwa uzito wa case kama hii....the only way forward ni mfumo mpya utakaoletwa na katiba mpya..
Siyo kweli mzee; majaji wa Marekani wanavaa majoho pia. Kila nchi ina staili ya majoho ya majaji wake kama ambavyo kila shule ina uniforms zake tofauti na kwinginekoKwanini majaji wa Tanzania wanavaa kama majaji wa enzi za ukoloni? Sasa utakuta USA jaji anavaa suti tu.
Lunatic [emoji2957][emoji2957][emoji2957]
Acha ujinga hakuna rais anamchagua mtu bila kwanza kujua ni mtiifu kwake. Upende usipende hakuna rais aliyependa haki nchi hii kuondoa nyerere kama magufuli. Alipenda haki tofauti na marais wengine aliwadhibiti kisawasawa fisadi na adui wa haki wote. Ndio wale waliyoonyesha furaha alipoaga dunia.Majaji wote walioteuliwa na marehemu siyo wa kuwaamini. Labda jaji kama alikuwa anafanya matendo anayotaka marehemu ili ateuliwe kuwa jaji.
Marehemu hakuwahi kumpenda mtu anayependa haki. Kigezo chake kikuu kwa uteuzi wowote, ni mteuliwa kumsujudia yeye na kumkubalia yeye kwa kila jambo hata kama jambo hilo ni hovyo kiasi gani.
uongo utakusaidia nini ? mpenda haki anawezaje kula hela ya tetemeko ?Acha ujinga hakuna rais anamchagua mtu bila kwanza kujua ni mtiifu kwake. Upende usipende hakuna rais aliyependa haki nchi hii kuondoa nyerere kama magufuli. Alipenda haki tofauti na marais wengine aliwadhibiti kisawasawa fisadi na adui wa haki wote. Ndio wale waliyoonyesha furaha alipoaga dunia.
Tabia ya CHADEMA ya kuwasemasema vibaya mahakimu na majaji ina gharama zake. Hao mahakimu na majaji sio artificial intelligence; ni binadamu wenye feelings kama binadamu wengine. Endeleeni; mtakipata mnachokitafuta!
Anasema wanasheria wanahisi mchakato huo umeingiliwa na watu wenye ushawishi.“Ninajua kwamba majaji wa Mahakama ya Juu hawafurahishwi na kuhangaishwa kwa Naibu Jaji Mkuu Mwilu. Wanaamini madai yote dhidi yake yalilenga kumzuia asiwe Jaji Mkuu,” asema.
Siyo kweli mzee; majaji wa Marekani wanavaa majoho pia. Kila nchi ina staili ya majoho ya majaji wake kama ambavyo kila shule ina uniforms zake tofauti na kwingineko
View attachment 1931746
Majaji wa Tanzania huteuliwa kwa usiri mkubwa bila uwazi. Hivyo ni jambo jema wananchi na vyombo vya media, asasi za kiraia, na wadau mbalimbali kuanza kuwajadili baada ya uteuzi maana kabla ya teuzi wananchi au chombo kingine huru hakihusishwi wala zoezi kuwa la wazi ili raia kuwajua wateuliwa wa nafasi hizi za kutoa hukumu. Mfano nchi za Marekani na Kenya kwa kutaja kwa uchache huwajadili mienendo ya majaji
.................................................................
Mfano:
Nairobi, Kenya
- Apr 15, 2019
Majaji 14 Motoni Akiwamo David Maraga
Na RICHARD MUNGUTI
CHUMA ki motoni kwa majaji 14 wa Mahakama ya Juu na Mahakama Kuu ambao huenda wakatimuliwa kazini kwa madai ya ufisadi na ukiukaji wa maadili ya kazi.
Wakipatikana na hatia, majaji hawa hawatakuwa na budi ila kufurushwa kazini kwa kuletea Idara ya Mahakama fedheha.
Kesi dhidi ya majaji hawa zinaendelea kusikizwa na majopo mawili ya Tume ya Kuajiri Watumishi Idara ya Mahakama (JSC).
Majopo haya yanaendelea kupokea ushahidi dhidi ya majaji hao katika Mahakama ya Juu na Jengo la Kenya R, Nairobi.
Majaji walioshtakiwa katika JSC wanawajumuisha majaji watano wa Mahakama ya Juu na majaji wanane wa Mahakama Kuu.
Walioshtakiwa ni Jaji Mkuu David Maraga, Jaji Mohammed Ibrahim, Jaji Smokin Wanjala, Jaji Njoki Ndung’u na Jaji Jackton Ojwang ambaye wiki iliyopita alisimamishwa kazi na Rais Uhuru Kenyatta.
Mwingine aliyewatangulia hawa ni naibu wa Jaji Mkuu Philomena Mwilu. Kusimamishwa kazi kwa Jaji Ojwang kumeyumbisha utendakazi katika mahakama hiyo ya upeo.
Rais Kenyatta aliteua jopo lenye wanachama watano kuamua hatma ya Jaji Ojwang. Mwenyekiti wa jopo hilo ni Jaji Alnashir Visram wa Mahakama ya Rufaa.
Jaji Smokin Wanjala. Picha/ Richard Munguti
Mashtaka dhidi ya CJ Maraga ni kuwa ni mbaguzi, mwenye ukabila na mkaidi wa maadili ya mahakama kwa kuhudhuria mikutano ya kisiasa Kisii na Nyamira.
Pia inadaiwa Jaji Maraga alinukuu uamuzi ambao haukuwa umesomwa wa Wajir katika kesi dhidi ya Gavana wa Laikipia.
Madai dhidi ya Majaji Ibrahim, Wanjala na Ndung’u ni ufisadi na ukiukaji wa maadili ya kazi.
Watatu hawa pamoja na Jaji Ojwang wanadaiwa walipokea hongo na kuidhinisha ushindi wa Gavana wa Wajir Mohamed Abdi Mohamud.
JSC inaombwa na walalamishi zaidi ya 600 kutoka kaunti ya Wajir wawatimue majaji hao watatu kazini kwa kupotoka katika uamuzi kwamba Bw Mohamud anahitimu kuwa Gavana.
Majaji wa mahakama kuu ni Majaji D.K Njagi, Edward Muriithi, Martin Muya, Thripsisa Cherere, Lucy Waithaka na Amin Farah. Wengine ni Richard Mwongo na James Wakiaga.
Baadhi ya malalamishi ambayo JSC imepokea ni pamoja na kucheleweshwa kutolewa kwa maamuzi, mapendeleo na muinguliano wa kimaslahi.
Majaji hawa wameandikia JSC na kueleza watawaita baadhi ya majaji wenzao kuwa mashahidi wao na walalamishi waliowasilisha kesi dhidi yao kujitetea wakiwekwa vizimbani.
JSC linaloongozwa na naibu wa mwenyekiti Mercy Deche linaendeleza vikao vyake katika Jengo la Kenya-Re.
Source : Majaji 14 motoni akiwamo David Maraga – Taifa Leo
Walipita huko na ndiyo maana katiba mpya ikapatikana, na siyo mwiko kujadili mwenendo wa jaji pia uteuzi wa majaji upo ktk hali ya uwazi na wanafanyiwa usaili ktk uwazi na umma mpana wanapata nafasi ya uelewa weledi, uzoefu, maadili na muegamio wa jaji upo wapi ktk masuala Kadhaa yenye manufaa kwa jamii kupata haki yao wanayostahili.Mijadala yao sio ya aina ya mijadala wanayoendesha CHADEMA!
Katiba haitaondoa matatizo yote. Bado hata tukipata katiba kuna cgamoto zingine, na hazitaepukika. Mfano huko Marekani kunakosifika kuwa na katiba nzuri, bado kuna changamoto za uteuzi wa majaji. Kama kutakuwa na raisi na awe nna chama chake kina maseneta wengi, basi hao masenata watahakikisha uteuzi wa majaji unapita bila shida. Sasa ile koti kuu ya USA ina majority ya majaji (7) ambao ni conservatives. TZ tukisema majaji wapendekezwe na raisi na kuteuliwa na bunge, matatizo yatakuwa palepale. Kama CCM ndiyo majority bungeni, itateua wale wenye mwelekeo wa CCM, na kama upinzani utakuwa na wabunge wengi na raisi pia uteuzi utakuwa ni wa wale wenye mwelekeo wa upinzani. Na hii itakuwa hata kwenye tume mbalimbali. Wajumbe, makamishina, na wakuu wa tume, kamisheni, na bodi mbali mbali watateuliwa na kupata support ya bunge kufuatana na ni nani mwenye majority bungeni.Uwepo wa mhimili uliojichimbia zaidi kwa mujibu wa katiba ya Tanzania kunatia ukakasi sana:
1. Hawa ni sehemu ya vigogo wanufaika wa lile saga la kutolipa kodi kwa mujibu wa katiba.
2. Hawa hawawajibiki kwa lolote katika maamuzi yao.
3. Hawa ni wateuliwa wa ule mhimili ule wenyewe.
Salama zaidi ya haki kutendeka ilikuwa kwenye kuonyeshwa kwa jitihada za kudai katiba mpya kwa ari zaidi.
Kusikia miito tu kwa masikio yakiwa makavu hakujawahi kuwa uwezekano kwenye dunia yetu.
Dini zote zinataka uadilifu.EeeenHeeee!
Yaleyale ya siku zote. Imani na mtu ni vitu mbalimbali kabisa. Sijui kwa nini watu huwa hawapendi kuamini hili!
Mahakama hiyo chini ya jaji Mustapher Siyani imekubali pia ombi la upande wa utetezi unaoongozwa na wakili Peter Kibatala kuwa upande wa utetezi una mashahidi wake kadhaa na kuiomba Mahakama Kuu kuwa miongoni mwao mashahidi hao, wapo mashahidi 4 walindwe na Mahakama wasitangazwe anuani zao wala majina yao kwa kuhofia kufuatwa na vyombo vya serikali.
Mheshimiwa jaji aliitazama sheria ya Uhujumu Uchumi na kukubaliana na upande wa utetezi juu ya ulinzi wa mashahidi hoja ambayo upande wa serikali / mashtaka waliipinga mashahidi kupewa ulinzi.24 Juni 2016 Makala ya mtandao (online document) parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1468490491-24JUNI,2016.pdf