Jaji Mutungi: Sijazuia mikutano ya ndani ya kisiasa ya vyama

Huyu Jaji alitakiwa kuwa upande wa vyama vya siasa! Sio upande wa Polisi kwa sababu anajua wazi kati ya hawa wawili mmoja hayuko sahihi.

Angeweza kutangaza kuwa vyama vina haki ya kufanya mikutano ya ndani kwani taarifa kwa polisi kisheria iko kwenye mikutano ya hadhara nje!!

Badala yake ombil lake linatumia ku-pacify walio na haki! Anafundisha “mwenye mabavu mpishe”!
 
Katiba na sheria za nchi zinasemaje?
 
Chama cha siasa kitakacho kubali kukutanishwa na polisi hakijitambui. Mutungi ndie msajiri, anazijua sheria. Amekubali kuna mapungufu, lakini hana ubavu wa kusimamia sheria, anajua serikali (polisi) ndio wenye makosa, lakini hawezi sema acheni kwa sababu hakuna sheria inayo waruhusu kufanya hivyo. Vyama vya siasa vingekuwa ndio vina vunja sheria angewaambia sheria namba fulani inawakataza. Mwafaka gani unautafuta kwa polisi wavunja sheria kwa kusimamiwa na CCM?

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Hivi Jaji, sheria ina semaje kuhusu mikutano ya vyama vya siada?

Kwanini wataalam mkisha pewa teuzi taaluma zenu mna waachia wake/ waume zenu wakandie unga wa chapati?

Mna aibisha mno. Sikutegenea Jaji kama wewe kutoa mawazo ya muuza togwa.
Wauza togwa au pombe?
Hulijui togwa wala mtungi wake!

Sent from my G80 using JamiiForums mobile app
 
Hi
Hivi Katiba haijatoa ufafanuzi wa kudumu wa vyama vya siasa kuhusu mikutano ya ndani au maelekezo ya katiba sio yenye tija. aisee Majaji wetu wanashida kabisa hivi elim zao walizipata wapi, lazima tuhoji kwa sababu wanavyo behave hata kwenye kesi ya mbowe inatufanya tutafakari upya kuhusu elimu waliyo nayo kama ni sahihi aula maana mtu akiona kuna mfumo umemkera kwa elimu yake huwa anajiuzulu
 
Eti Mvutano wa Polisi na vyama vya siasa, kwanza ni aibu Polisi kuwa na mvutano na vyama vya siasa aibu sana sana kwa sababu vyama vya siasa vinajua fika vinafanya shuguli kiseheria sasa polisi anaingiliaje kati kwenye maswala ya kisheria na kubatilisha kuwa sio kisheria, hivyo vyama ni vipi si angesema mvutano wa polisi na CDM, NCCR kwan lini wamewahi kuwa na mvutano na CCM huenda hiki kikao kitakuwa kati ya vyama na polisi kasoro CCM maana wao ndio hawahusiki
 
Polisi wana matatizo sana kwenye hii nchi. Wenzao wa JWTZ, JKT, Zima Moto, Mgambo, nk. Wametulia tu. Hawana shida na mtu. Ila siyo wao! Kutwa ni kutafuta tu kiki na kujitutumua.

..kuna wana-chadema walioko mkoa wa mara wanadai hivi majuzi, polisi, ffu, na jkt, wametumika kuzuia kongamano lao.
 
Notable quotes: "...tunajaribu kupata ufumbuzi...wajizuie kwa muda...waendelee kuwa wastahimilivu..."
"Anawashauri" vyama vya siasa, vipi! Na chake pia?! Wawe wastahimivu, hadi lini?
Kwa mtu mwenye CV kama yake, ni aibu kuja na maandiko kama haya, yanaonyesha kilichoko moyoni mwake. Kazi zao "mahakimu" ni kunukuu vifungu, sheria. Angenukuu vifungu polisi wanavyovivunja na kupendekeza adhabu inayowastahili. Mikutana ya maridhiano si yake, haimhusu.
Naona kaachia mambo yamefika kusiko, kachafuka, ananuka, anajaribu kuoga. Je, atatakata?
 
Baada ya kumkumbusha kuwa hana mamlaka ya kufanya hivyo naona akili zimemrudi
 
Nashangaa sana CCM na uongozi wa juu wa serikali kuwasikiliza wapinzani ambao ni vyama Maiti vinavyotembea.

Hamna kitu ndani ya hivi vyama ni kupoteza muda bure ambao ungetumika kufanya mambo mengine muhimu.

Ni madebe matupu hayaishi kutika. Ukiishi ndani ya hivi vyama ndio utajuwa vilivyo vyeupe, wale wanaotaka kufanya siasa na wana sifa za uana siasa hawa wezi kupoteza muda wao bure ndani ya hivi vyama.

Kueneza chuki ndio sera za chama. Mfyuuuuuuuuu.
 
Hakika
 
Anafikiri hatfahamu kuwa, wanafahamu kuwa wanakwenda UN na watakumbana na maswali magumu kujibu huko ndiyo maana anawaletea changa la macho ili katika kikao hicho wapitishe maazimio danganya toto kisha wakiulizwa huko waseme wamekaa wakakubaliana kidemokrasia. Siku zote ukiona mtu fedhuli anaitisha suluhu ogopa sana ujue kuna walakini. Huyu jaji amekuwa akikiuka katiba mchana peupe bila haya wala uoga na anajulikana kabisa ni kibaraka wa nani. Msitegemee jema lolote kutoka kwake
 
Ushauri wa bure kwa Msajili. Ongea na Waziri Simbachawene hata kwa simu na amtake waziri atoe amri kwa Siro na polisi wake waache upuuzi wanaofanya. Period.
 
Hivi Jaji, sheria ina semaje kuhusu mikutano ya vyama vya siada?

Kwanini wataalam mkisha pewa teuzi taaluma zenu mna waachia wake/ waume zenu wakandie unga wa chapati?

Mna aibisha mno. Sikutegenea Jaji kama wewe kutoa mawazo ya muuza togwa.
hahahahaaaaaaaaa umegonga aisee wee jamaa hufai daaa
 
Ushauri wa bure kwa Msajili. Ongea na Waziri Simbachawene hata kwa simu na amtake waziri atoe amri kwa Siro na polisi wake waache upuuzi wanaofanya. Period.
hao wote lao ni moja utasumbuka bure babangu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…