Baadhi yetu tumekosa mwelekeo kabisa! Nilisikiliza press conference ya Jaji Warioba, na sikuona sehemu yoyote ya kusema labda kasema uwongo. Kwa bahati mbaya na kama kawaida yetu, badala ya kujibu hoja zake, baadhi yetu tumeanza kumshambulia, wengine wakisema "astaafu siasa." Natoa maoni yangu katika muktadha wa Ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (kama ilivyofanyiwa marekebisho hadi mwaka 2005). Ibara 18(a) inasema "Kila mtu ana uhuru wa maoni na kueleza mawazo yake." Ibara hii haisemi mtu akistaafu au akiwa mzee, anakosa huo uhuru au kwamba hana haki ya kutoa maoni na kueleza mawazo yake. Je, ni nani anayemnyima huo uhuru na kwa mujibu wa sheria gani? Je, mtu akistaafu au akiwa mzee, hana haki ya kutoa maoni kuhusu mambo anayoyaona kwa masilahi ya nchi? Kwa mantiki hii naona tumekosa mwelekeo. Some of us no longer have good judgement, and so our ability to distinguish between good and bad or right and wrong is blurred. Why have we reached this stage?