Jaji Warioba: Dkt. Bashiru ajibiwe kwa hoja, hajafanya kosa lolote acheni kumshambulia

Jaji Warioba: Dkt. Bashiru ajibiwe kwa hoja, hajafanya kosa lolote acheni kumshambulia

Hapa ndipo unapotofautisha maoni ya msomi, na mashabiki wanaotafuta madaraka na vyeo kwa kumshambulia Bashiru kwa ajili ya matumbo yao.

Utashangaa mpaka kina Msukuma na Lusinde leo wanaonekana wa maana kisa wanamshambulia Bashiru, tuna taifa la mihemko sana, ambalo kila siku linazidi kupoteza muelekeo.

..wakati Dr.Bashiru akiwa Katibu Mkuu aliwatumia kundi la wasiojulikana, Musiba, Musukuma, Kibajaji, kuwatukana na kuwashambulia wakosoaji wa serikali ya awamu ya 5.

..Dr.Bashiru ajilaumu mwenyewe kwasababu hawa wanaomsuta na kumbeza yeye ndiye aliyekuwa akiwatunza alipokuwa Katibu Mkuu wa Ccm.
 
Mzee maisha yamempiga, anahaha tu kutafuta ajira kupitia wapiga debe wa katiba mpya.

Huyu alikaa na Nyerere kwa miongo kadhaa, hakumshauri kuhusu katiba, na aliiacha nchi imefilisika, kwa Sasa hivi hana la kutushauri, ni mtu wa hovyo tu, na pia alikula Hela katika kashfa ya meremeta.

Matapeli wa kisiasa waliobaki
Hivi hapo ulipo unajiona unafanana kwa lolote na warioba
 
WAZIRI Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Sinde Warioba, ameeleza kuwa Balozi Bashiru Ally, hajafanya kosa lolote hakustahili kushambuliwa. Amesema, watu wajibu hoja badala ya kumshambulia yeye binafsi.[emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116]View attachment 2423226
ccm kwa maigizo
 
Hebu tupe mfano wa mtu mmoja toka CCM, au wale wengine mashabiki wa walamba asali aliyejibu hoja za Dr. Bashiru ukiondoa hizo kelele za kina Lusinde na wenzake.

Halafu unawaingiza wakina Lissu na wengine sijui wanahusiana nini kwenye kujibu hoja za Dr. Bashiru, naona ndio unataka apuuzwe kisa historia yake.

Mtambue whatever Dr. Bashiru alifanya kabla, hakumuondolei haki yake ya kuzungumza na hoja zake kujibiwa.

Hiki mnacholazimisha kuleta ndicho kinawakuta nanyi halafu mnalalamika, ndio maana mikutano ya siasa mmezuiwa japo ni haki yenu, amkeni; msiwe wabinafsi, haki haichagui rangi, historia, wala chochote..

Ukimnyima haki mwenzio mjue nanyi mtamyimwa, mjifunze kuihubiri demokrasia na kuitenda, sio mnaishia kuihubiri pekee, hii demokrasia yenu unayoileta ina exceptions, hamtaki fulani asikilizwe kisa historia yake, hii kitu haipo hapa duniani.

..unachozungumza kiko kinadharia zaidi.

..huwezi kuwa mbinya haki za wenzako halafu ghafla unataka wale uliokuwa ukiwadhulumu wakutetee.

..Dr.Bashiru awe muungwana kwa kuomba radhi kwa kusimamia na kutetea udhalimu wakati akiwa Katibu Mkuu wa Ccm.
 
Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Sinde Warioba, ameeleza kuwa Balozi Bashiru Ally, hajafanya kosa lolote hakustahili kushambuliwa. Amesema, watu wajibu hoja badala ya kumshambulia yeye binafsi.

View attachment 2423235

Chanzo: Mwanahalisi
Muda si mrefu na yeye ataanza kushambuliwa! Shauri yake. Chawa hawataki kabisa bosi wao kuguswa.
 
Pia ajibiwe na aliowasema sio chawa wao.

Bashiru kamsema Samia Ila ajabu anajibiwa na wakina Kigwangala.

Kigwangala ana cheo gani serikalini Cha kumjibia Samia

Samia atoke ajibu hoja za bashiru mwenyewe sio kuwatuma mawakala wa unaupiga mwingi[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
Unadhani hata mama kawatuma basi. Watu wanasaka uteuzi hao. Kigwangala kuna hoja iliyowahi kutokea inayomgusa Rais kuanzia JPM then akakaa kimya. Anasaka Uwaziri bado

Sent from my CPH2219 using JamiiForums mobile app
 
..wakati Dr.Bashiru akiwa Katibu Mkuu aliwatumia kundi la wasiojulikana, Musiba, Musukuma, Kibajaji, kuwatukana na kuwashambulia wakosoaji wa serikali ya awamu ya 5.

..Dr.Bashiru ajilaumu mwenyewe kwasababu hawa wanaomsuta na kumbeza yeye ndiye aliyekuwa akiwatunza alipokuwa Katibu Mkuu wa Ccm.
Bado hamjitambui kabisa, bado wachanga sana kidemokrasia, demokrasia haina exceptions, eti itakupa haki yako kama hauna historia mbaya ya yaliyopita!.

Halafu mnaonesha dhahiri kumbe hata huwa hamumuelewi Mbowe akisema hana visasi, nyie bado wachanga sana.

Kama mkianza kuleta habari hizo, hata huko ulipo nanyi kuna madudu mlifanya yanayostahili msisikilizwe, na tukianza kutazamana kwa jicho hilo, mwishowe hili taifa litakuwa la mabubu CCM wafanye wanavyotaka, usimfunge mdomo mwenzio ili nawe ukisema upate wa kukusikiliza.
 
..wakati Dr.Bashiru akiwa Katibu Mkuu aliwatumia kundi la wasiojulikana, Musiba, Musukuma, Kibajaji, kuwatukana na kuwashambulia wakosoaji wa serikali ya awamu ya 5.

..Dr.Bashiru ajilaumu mwenyewe kwasababu hawa wanaomsuta na kumbeza yeye ndiye aliyekuwa akiwatunza alipokuwa Katibu Mkuu wa Ccm.
JIBU HOJA, Bashiru wa enzi ya Magu alikuwa Mlevi!!!

Mlevi hujibiwa akiwa POMBE imekata, na Si wakati amelewa.

Bashiru huyu ndiye Bashiru halisi, Ajibiwe Kwa hoja.
 
Kwa mwenye akili timamu, hashambulii, hujibu kwa hoja , kwa weledi wa hali ya juu. Naona ambao kwao shule ni shida wana taabu ya kuelewa.
 
..unachozungumza kiko kinadharia zaidi.

..huwezi kuwa mbinya haki za wenzako halafu ghafla unataka wale uliokuwa ukiwadhulumu wakutetee.

..Dr.Bashiru awe muungwana kwa kuomba radhi kwa kusimamia na kutetea udhalimu wakati akiwa Katibu Mkuu wa Ccm.
Mimi nazungumzia sheria zilizoandikwa vitabuni tunazotakiwa kuzifuata, ajabu wewe unasema niko kinadharia zaidi!.

Utambue haki haihitaji hisani yako wala ya mwingine yeyote, na usitumie hisia kuhukumu jambo linalohitaji kutendwa kisheria, tambua sheria haina hisani.

Lazima uifuate sheria, kama hutaki kuifuata kisa historia ya mtu, basi utambue nawe ni mvunja sheria tu kama walivyo CCM, nyie hamchekani.
 
ccm kwa maigizo
Akili za ccm ni kudhalilisha dada zetu na kushindwa kujibu hoja[emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji41][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116]
FB_IMG_1668933224377.jpg
 
Hapa ndipo unapotofautisha maoni ya msomi, na mashabiki wanaotafuta madaraka na vyeo kwa kumshambulia Bashiru kwa ajili ya matumbo yao.

Utashangaa mpaka kina Msukuma na Lusinde leo wanaonekana wa maana kisa wanamshambulia Bashiru, tuna taifa la mihemko sana, ambalo kila siku linazidi kupoteza muelekeo.
Loud and clear
 
Mzee maisha yamempiga, anahaha tu kutafuta ajira kupitia wapiga debe wa katiba mpya.

Huyu alikaa na Nyerere kwa miongo kadhaa, hakumshauri kuhusu katiba, na aliiacha nchi imefilisika, kwa Sasa hivi hana la kutushauri, ni mtu wa hovyo tu, na pia alikula Hela katika kashfa ya meremeta.

Matapeli wa kisiasa waliobaki
Shame on you
 
Back
Top Bottom