Jaji Warioba: Miaka yote watu wanaelewa kujaza fomu, lakini 2020 ghafla hawajui. Siasa inataka kuingia kwenye Dini

Ilishangaza ccm ndo inawenyeviti na vitongo na wajumbe wa mitaa na vijiji hawajui kusoma na kuandika wengi nchini lakini wao tume haikuwaona [emoji38][emoji38][emoji38]
 
Hawa wazee wakae kimya sasa, wakati yanatokea walikuwepo wakakaa kimya hawakusema leo wanasema...
Unawaonea hawa si waliongea ila tatizo waliongea gizani...Tusiwe wazuri wakulaumu, hawa ni wahanga wakuongea yaliyokuwa yanawasibu
 
Mfuasi wake mmoja tokea jalalani alimuita Mheshimiwa Mungu siyo??😆
Ile ilikuwa ni kilele cha kujipendekeza. Japokuwa ilikuwa ni kuteleza kwa ulimi lakini mara nyingi mambo haya yanatokana na vitu vilivyojificha kwenye ubongo.
 
Kwanini hawakuenda mahakamani?

Kubaki unalialia umeonewa wakati hakuna kesi hata moja mahakamani ya kupinga uchaguzi ni upuuzi na kupoteza muda.
Wewe nadhani unaishi kama shetani, mtu asiye na haki!
 
Kwanini hawakuenda mahakamani?

Kubaki unalialia umeonewa wakati hakuna kesi hata moja mahakamani ya kupinga uchaguzi ni upuuzi na kupoteza muda.
Waende mahakamani, mahakama ambazo majaji wote wameteuliwa na mwenyekiti wa CCM.
Halafu tena hapohapo unaenda kuwastaki tume ya viongozi walioteuliwa na mwenyekiti wa CCM!
 
msingi wa kujaza fomu ni sheria- hizo hufuta kesi mahakamani zikikosewa- ila kwenye uchaguzi mnataka ichukuliwe poa- ni sheria au mapenzi /husuda? Acheni unafiki
 
Waasisi wakuu
Waasisi wengi ninaowajua kwenye nyanja za siasa duniani hapa walikuwa wanatembea na punda hata ng'ombe! Wapuuzwe?

Ushawahi kuona picha ya Mwalimu J.K anaendesha baisikeli? Alikuwa mjanja?
 
Hawa wazee wakae kimya sasa, wakati yanatokea walikuwepo wakakaa kimya hawakusema leo wanasema...
Hata Mh. Hapi aliyanena hayo hayo leo hii anasulubiwa. J.K(mrisho) ameingia madarakani kwa gia hizo hizo na hata kumwachia Makonda batoni.
Mh. Suluhu ameruhusu 'uhuru' 'anasifiwa' ma amekubali kwa kinywa chake kuwa ni ngumu kwa CCM ya sasa kuingia katika mchakato wa vinyang'anyiro vya uongozi bila rushwa kidogo. Msikilize akiiwa anapokea ripoti za "Domo-krasia" ikulu
 
Ni ujumbe mzuri sana, Mzee jaji Warioba Mungu aendelee kukujalia Afya njema, nasi tuendelee kufaidi busara zako
 
Uko sahihi ni ccm wote, ila kwa Magufuli it was even worse.
Kuna ukweli na hilo la "even worse" amekipatia CCM jeuri maradufu na kilivyokuwa huko nyuma+"mabilonea" na hata kuhalilisha vitega uchumi vyake ambavyo vilisikika kua na udhalimu ndani yake-mfano kujilimbikisha ardhi n.k
 
Kwa Ulimwengu wa Sasa kwani ishu ya kuchukua fomu na kurudisha zifanyike physically? Kwann watu wasipakue fomu online then wajaze alafu waaplod. Ni uhuni tu, mgombea anachukua fomu mara mkurugenzi hayupo ofisini mwisho wa siku anarudi saa 10 alafu ndio deadline. Mgombea anajaza fomu ikifikia mezani kwa wahuni kama aliandika anamiaka 35 wahuni wanaongezea 1 nyuma then inasomeka ana miaka 135 na anakosa sifa ya kugombea. Kurudisha fomu mara mpokeaji hayupo au mgombea anatekwa njiani mpaka muda wa mwisho unafika yaaan ni maigizo ya kijinga sana. Kwakweli Jiwe sipati picha alikuwa anataka nn na hii nchi.
 
Kikubwa hapa ni kutafakari.
Nimekuwa nasema mara nyingi kuhusu matabaka mapya yanayojengeka, na hata kusema kabila wanalolijenga. Kuna kila aina ya vigezo la kuwa sasa CCM ni kabila.
...na hata kusema kuwa bila ya Demokrasia ya kweli(kama ipo) ndani ya CCM hawawezi kutulaghai kuwa kuna Demokrasia katika mchakato wa siasa Tanzania. Juzi kati nguli wao Jemedari Kinana ameligusia hilo.

CCM wabadilike, Wananchi tubadilike na Tabia nchi. Tusibuluzane.
 
Ile ilikuwa ni kilele cha kujipendekeza. Japokuwa ilikuwa ni kuteleza kwa ulimi lakini mara nyingi mambo haya yanatokana na vitu vilivyojificha kwenye ubongo.
Kabisaaaah, linalotokea mdomoni ni jambo ambalo unalifikiria, lipo kichwani na kwenye nafasi na moyoni mwako!
 
Haumtendei haki Hayati Raisi JPM. Ukweli ni kuwa "CCM ina wenyewe" ili kuwaridhisha "Kabila" lao na kutekeleza "malani"(ilani) kulikuwa na ulazimu wa Kuteka uchaguzi wao-ni CCM wote hao

Nadharia wanayojenga kuwa ni yalikuwa ya Hayati JPM, rest in peace Comrade, ni mazingaombwe Kamati kuu, na wajumbe ni CCM na alikaa na "Wenyewe" Aisee
Kuna umuhimu wa kutenganisha kofia zao mbili mbili na hilo wanalijua. Kuna umuhimu wa kuangalia tena mchakato huo wa kujaza fomu-elektroniki inaweza ikawa suluhisho zuri lakini kama CCM ndio ihusike pekee na mchakato huo tutarudi pale pale. I Second ushauri wako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…