Jaji Warioba: Miaka yote watu wanaelewa kujaza fomu, lakini 2020 ghafla hawajui. Siasa inataka kuingia kwenye Dini

Jaji Warioba: Miaka yote watu wanaelewa kujaza fomu, lakini 2020 ghafla hawajui. Siasa inataka kuingia kwenye Dini

U
Zaidi ya Nusu za kata nchi nzima CCM ilipita bila kupingwa sasa mahakamani unaenda kufungua kesi Gani wakati hata uchaguzi haukufanyika?

NEC watu walipeleka rufaa zilikaa zaidi ya wiki 2 mpaka 3 huku CCM ilishaanza kampeni ghafla unaambiwa rufaa Yako imefeli!!! Then what?? Hiyo kesi mpaka iishe si inabaki wiki moja kwenda uchaguzi!!!

Nmefurahi kusikia Kinana anakiri kuwa Haki na Demokrasia havikuwepo, na ndio mwanzo mzuri kupata chaguzi zenye matakwa ya wananchi Ili kuleta viongozi wenye tija kwenye maendeleo yao
Uvumilivu ulikosekana wakati huo,, walipigwa kwenye chama tuu walikuwa wengi sana. 2025 wajiandae kisaikolojia, mhenza, kawe, bariadi.. Daaa yule kijana wa kawe nusu aanzee kutembelea v8 lake ndoto ikayeyuka paaaaaaa
 
Kwanini hawakuenda mahakamani?

Kubaki unalialia umeonewa wakati hakuna kesi hata moja mahakamani ya kupinga uchaguzi ni upuuzi na kupoteza muda.
Jaji gani angesikiliza kesi hiyo? Hao hao waliokuwa wanasikiliza kesi ya Mbowe?
 
Jaji Warioba akichangia kwenye mkutano wa TCD leo Dodoma, amenena haya

Miaka yote watu wanaelewa na wanajaza fomu vizuri lakini Mwaka 2020, ghafla watu hawajui kujaza fomu (wanaenguliwa). Hapa lazima kuna namna

Msitazame Wajumbe wa Tume pekee, angalieni Mfumo mzima wa Uchaguzi. Wizi wa kura unaanzia mbali. Unaanzia kwenye Kuandikisha wapiga kura, wakati wa kupiga kura na kutangaza matokeo

Siasa inataka kuingia kwenye dini, zamani viongozi tulikuwa tunakwenda kwenye vyumba vya ibada kama waumini, unasikiliza neno la Mungu. Siku hizi viongozi wakienda wanaombwa kutoa salamu za kisiasa, hii inaweza iingiza siasa katika dini tukapata matatizo

Vyama vingi vimekuwa kama makabila, vinaanza kugawa wananchi. Wananchi walikuwa kama jumuiya lakini siku hizi mambo mengi ya kijamii tunaingiza siasa, mfano msiba ni wa jamii lakini baadhi ya misiba unakuta sare za vyama,"

Katika vyama jumuiya zetu nazo zinakuwa kama za uhasama, badala ya kutuleta pamoja. Hali tuliyo nayo sasa utamaduni umetikiswa kidogo na tunapozungumzia maridhiano, nia yake kuturudisha kwenye utamaduni tuliokuwa nao


Viongozi wa kisiasa wangehubiri amani kama walivyofanya viongozi wa dini miaka michache iliyopita, nchi isingekuwa na malalamiko yanayolalamikiwa hivi sasa “kama wangetenda kama viongozi wa dini, nadhani matatizo haya tunayozungumza tusingekuwa nayo.

Sawa, lkn kwani kwakati wa Uchaguzi ulisafiri kwenda Brunei? Au ? Hukusema kitu.
 
Kipindi Cha Kinana CCM waliiba kura ila kwa aligorithm yaani Gap iwe 60-40% kuanzia Kata hadi Urais. Ila kwa JPM aisee hakuna Cha formula yeye alizoa kila kitu kuanzia vijiji hadi Urais 84%+

Yaani mpaka Pemba eti CCM ilishinda majimbo karibu yote!! Seriously?
Kwahiyo mnataka ile ya kuibiwa kidogo na kuachiwa kidogo,

Basi sawa, kinana ndio huyo sasa atawaibia kidogo

Sent from my SM-T295 using JamiiForums mobile app
 
Kwanini hawakuenda mahakamani?

Kubaki unalialia umeonewa wakati hakuna kesi hata moja mahakamani ya kupinga uchaguzi ni upuuzi na kupoteza muda.
Hao majaji wameteuliwa ujaji na mwenyekiti wa ccm halafu atende tofauti na ccm you guy waza sawasawa tumia akili yako kwa matumizi sahihi...
 
Kwanini hawakuenda mahakamani?

Kubaki unalialia umeonewa wakati hakuna kesi hata moja mahakamani ya kupinga uchaguzi ni upuuzi na kupoteza muda.
we unazani kwa udikteta ule ungenda mahakamani ungeshinda? alishasema mkurugenz nakuteua alafu utangaze mpinzani huna kazi,na ww na akili yako fupi kama ya pimbi unaona sawa kutetea uovu
 
Naunga mkono hoja ya mh.Jaji Warioba kuwa :-

1)Tukomeshe tabia za wanasiasa kutoa salamu za kisiasa/kuomba kura wakiwa katika mahali patakatifu katika nyumba za ibada....tabia hii imefurutu ADA hata kwa wanasiasa wa vyama vya upinzani.....

2)Tabia ya kwenda misibani huku tukiwa na sare za vyama vyetu si AFYA KWA JAMII

#Siempre JMT🙏
#Nchi Kwanza 🙏

Hata Kwenye shughuli za kiserikali unakuta Masare ya ccm.
 
Kwanini hawakuenda mahakamani?

Kubaki unalialia umeonewa wakati hakuna kesi hata moja mahakamani ya kupinga uchaguzi ni upuuzi na kupoteza muda.
Ngoja nimalize kula ndo nikujib, ww subiria hapo pembeni tu!

Screenshot_20220310-174730.jpg
 
Back
Top Bottom