Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
"Wamesema vifo na vilitokea vipi... mimi naamini vifo vilikuwa vingi zaidi kuliko wanavyosema. Lakini wanasema kulikuwa na vitendo vya uvunjaji wa sheria, na wanapendekeza iundwe tume nyingine iende kuchunguza na wale ambao walitenda nje ya sheria wawe personally accountable. Maana yake wanasema uende utafute askari ambao wametenda nje ya sheria kisha uwashughulikie.
Nayo inanipa matatizo kidogo... inanipa matatizo kidogo kwa mambo mengi. Unakwenda kutafuta hawa waliotenda; walioagiza je? Na hii hapa tumekuwa na mifano. Mwaka 1976 serikali iliunda kikosi kazi cha wataalam, polisi na usalama. Tulikuwa na tatizo kama unakumbuka, tulikuwa na tatizo la vikongwe kuuawa Mwanza na Shinyanga. Wakawapeleka kule waende wakafanye uchunguzi. Tulichokuwa tunataka ni uchunguzi, kwa nini haya yanatokea? Kisha waje watoe taarifa kwa serikali ijue hatua za kuchukua.
Tatizo lilikuwa ni la uaji, mauaji ya wanawake wazee wakishukiwa kuwa ni wachawi. Wale, kile kikosi kazi, badala ya kwenda kufanya uchunguzi, kikaenda kuanzisha makambi kule na kutesa wananchi. Wengine wakafa, wengine wakapata vilema. Ilipogundulika ile, hatua zilizochukuliwa; ya kwanza ilikuwa ni kuwajibika. Hawakuwa kule, ndio unakumbuka Mwinyi ali-resign, Siyovelwa aliyekuwa Waziri wa Usalama ali-resign, Wakuu wa Mikoa Mwanza na Shinyanga, Mabawa na Kisumo, walire-resign. Ndio ikafuata hii sasa hatua ya pili kwenda kuona hawa walio... wakaenda, wakakamatwa, wakashtakiwa.
Sasa hapa haya yametokea. Hapa ni kama wanasema polisi walivunja sheria. Sasa unataka tume iende ikachunguze nani? Ichunguze taasisi ya polisi ama watu maalum? Mimi naona kama hii nayo ni kama kusibaziba mambo."