The Sunk Cost Fallacy 2
JF-Expert Member
- Nov 8, 2022
- 9,436
- 10,944
Swali.
Kama hivi ndivyo,Kwa nini CCM mnakuwa wadogo wa madaraka wakati kiuhalisia Wapinzani hawana uwezo wa kushindana na kushinda?
My Take
Ni vyema CCM ikajifunza Namibia sio lazima ushinde Kila pointi ndio uhasabiwe umeshinda.
Wapinzani wakishinda watangazwe Ili kuepusha chuki na sintofahamu kwenye jamii.
=====
"Mimi ninazungumza na vyama vyote na viongozi wao, si muda mrefu umepita, ilikuwa kama miezi sita hivi, nilimuuliza kiongozi mmoja wa upinzani, je, kweli mnategemea nini?
Akaniambia walikuwa wamefanya utafiti waone hali itakavyokuwa, alisema matokeo yaliyotoka kwamba tukijitahidi sana upinzani kwenye uchaguzi wowote unaokuja hatutazidi 25% wakijua kwamba wao kwa wakati huu hawana uwezo wa kuweza kutoa ushindani mkubwa, nikawauliza kwanini?
Wakasema ‘kwa miaka 6 shughuli za siasa zilikuwa zimesimamishwa, sisi hatukufanya kazi, sasa ndiyo tunaanza kufanya kazi, hatujasambaa hata kwenda chini, kwahiyo ukija uchaguzi kuna mahali hata hatutaweza kusimamisha wagombea’, na ndilo hilo ambalo limetokea.
Walikuwa wanasema asilimia 25, lakini hawakufika hata 1 kwasababu walijua hawana uwezo wa kuweka wagombea kila mahali, lakini hata walipokuwa na uwezo wa kuweka wagombea, wameenguliwa"- Jaji Warioba.
Waziri Mkuu mstaafu wa Tanzania Jaji Joseph Sinde Warioba akizungumza na wanahabari siku ya Jumatano Desemba 04, 2024 mkoani Dar es Salaam kuhusu uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika Novemba 27, 2024.