LGE2024 Jaji Warioba: Wapinzani Waliniambia Wangeweza Kupata Ushindi Kwa 25% tu

LGE2024 Jaji Warioba: Wapinzani Waliniambia Wangeweza Kupata Ushindi Kwa 25% tu

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Hii dhambi aliyofanya Mchengerwa malipo yake yatakuwa 2025, Mungu atawapiga kofi kubwa hawataamini macho yao.
Watanzania wengi huwa hawajitokezi kupiga kura. Wamekalia malalamiko tu. Acha CCM iendelee kututawala. Hiyo 2025 hakuna jipya litakalotokea mpaka siku CCM ipasuke vipande vipande yenyewe.
 
"Nilimuuliza kiongozi mmoja wa upinzani. Je, kweli mnategemea nini? Akaniambia walikuwa wamefanya utafiti. Matokeo yake tuliyoonyeshwa tukijitahidi sana upinzani kwenye uchaguzi wowote unaokuja hatutazidi asilimia 25"

Waziri Mkuu mstaafu Jaji Sinde Warioba.
Kwa mazingira yale wewe ulitegemea nini?
 
Unaengua nini kama wapinzani wenyewe hawakujipanga sio tu kwenye kampeni mpaka maandalizi ya kampeni yeyewe ovyo tu.
Kuengua mgombea kwasababu za kipuuzi ili chama kimoja kipate uhalali wakushinda peke yake hapo nani hakujipanga?.
 
Kulipaswa kuwe na haki na usawa kisha tuone je ni kweli hawakujipanga.tofauti na hapo nikutaka kulazimisha kuhalalisha ujinga uliofanyika.Warioba aache kumumunya maneno kwasababu wote tunajua kilichotokea.
 
"Nilimuuliza kiongozi mmoja wa upinzani. Je, kweli mnategemea nini? Akaniambia walikuwa wamefanya utafiti. Matokeo yake tuliyoonyeshwa tukijitahidi sana upinzani kwenye uchaguzi wowote unaokuja hatutazidi asilimia 25"

Waziri Mkuu mstaafu Jaji Sinde Warioba.
Ukitaka kuwa mjinga kwenye nchi hii kuwa mfuasi wa ccm
 
Hatutarajii wamgeuke Jaji Warioba kwa kukataa matokeo mwaka 2025, wameongea naye wakamwambia kama ni kushinda, basi ni asilimia 25, kwa hesabu rahisi, Samia atashinda kwa kishindo cha asilimia 75.

Mchezo umekwisha, tujadili 2030.
Screenshot_20241205-125023.jpg
 
Umeandika nini sasa?
Warioba katoa maangalizo na udhaifu wa ccm mbele ya wapinzani. Ni hoja, mtu mwenye akili angemjibu warioba kwa hoja si kwa viji maneno kama vya kwenye taarabu/khanga/kawa.
Alisema mnaingiza majeshi kwenye siasa siyo kweli? Rejea parade ya songwe
Alisema kura zilipigwa nje siyo kweli?
Alisema wapinzani walikatwa kwa hilarious na ghirba siyo kweli?
Alisema UCHAWA kama wa kwako unatengeneza udiktata siyo kweli?
 
Mimi namjadili kwa engo hiyo
 
Kabisa mkuu..najua hawawez kushinda kwa asilimia zote kutokana na mizizi ambayo ccm imejiwekea. Lakini angalau waachiwe hata hicho kidogo wanacho pata.
Unafikiri hata wakiachiwa hicho kidogo (japo sijapenda neno kuachiwa).. hiyo 25% wakishinda ambayo ndo ilikuwa haki yao kwa hesabu zao, kwa siasa za bongo na wapinzani hawa wangelalamika tu!.

Mi nafikiri siku kukipatikana upinzani utakaojitolesheza vyema ccm anatoka madarakani tena mapema mno!, wanalalamika wananunuliwa kwanini wasikatae kununuliwa...?

ukikubali kununuliwa sie tu aliekununua ndo anahatia hata wewe uliekubali unayo hatia!.
chengine wapinzani wamekuwa wanapinga kila kitu, hata vile ambavyo vinawaletea tija watu na wanaona moja kwa moja wao wanapinga!.. heri wangekuja na sera za uboreshaji kwa yale mazuri ambayo yameanzishwa na wengine ila wao wakianza kuisema Tanzania unaweza kusema ni jehanam ndogo..!!!
 
Hakuna sehemu Mzee Warioba amesema kuwa wapinzani hawajajipanga. Kama hawajajipanga wasingeweza basi kutoa tathmini ya matarajio yao, Mzee alieleza sababu alizopewa na wapinzani alioongea nao za kuwa na matarajio madogo kuwa ni kutokana kuminywa kwao na vyombo vya dola kutekeleza majukumu yao kwa amri haramu ya yule mwendawazimu wa Chato
 
Mimi nimemuelewa vizuri sana Mzee Warioba, sasa huo Uchaguzi Mkuu ujao tujizatiti na wakijifanya kuuchafuzi tunalianzisha Nguvu ya Umma✌️
 
Back
Top Bottom