Jakaya Kikwete achaguliwa kuishinikiza Taliban kurudisha watoto wa kike shule

Kha! at mataifa makubwa kama US huwa wanaidharau UN, sijui ni nani aliyekudanganya kijana. Huyo US angekomaa na kura yake ya VETO, au angekuwa analipa mamilioni ya madola kuihudumia kama angekuwa anaidharau? Kuna post za UN hawezi kupewa raia wa nchi yo yote zaidi ya US, unadhani kwa nini?

Kwa sababu US inajua sana umuhimu wa UN na pale ndipo siasa na influence zinapopigwa.

Halafu enzi za JK si ndiyo alianzisha wanafunzi kupewa mikopo ya vyuo mpaka vile vyuo vya binafsi? Ama kweli tenda wema wende zako.
 
Halafu enzi za JK si ndiyo alianzisha wanafunzi kupewa mikopo ya vyuo mpaka vile vyuo vya binafsi? Ama kweli tenda wema wende zako.
Kwenye vyuo vikuu bado hatujaanza kuwa na tatizo la elite and prestigious schools ambazo wanyonge na watengwa hawakanyagi.

Tatizo liko shule za sekondari, msingi na awali.

Jakaya Kikwete hasomeshi watoto wake kwenye shule za makapuku, alisema mwenyewe kuhusu mwanae Mwanaasha kwenye hotuba ya mazishi ya Magufuli.

Unaendaje kuongoza juhudi za dunia kutoa fursa za elimu bora kwa wote kama nchini mwako ukiwa Rais hukuweza na hukujali chochote cha elimu bora isipokuwa ya watoto wako binafsi ????
 
Hapo huyo mzee kautafta yeye mwenyewe huo mchongo
 
Unaweza kuta na ww n Graduate wa Shule za Kata au UDOM. Toka Uhuru, hakuna awamu ambayo ilifanya mageuzi makubwa ya elimu kimiundombinu na uwezeshaji kama 2005-2015 chini ya JK. Kama hujasoma shule ya kata, kuna watu wako wa karibu wameganya hivyo. Hizi shule za kata na Chuo cha UDOM na makumi ya vyuo vya kati yaliopandishwa hadhi na kuwa vyuo vikuu na hata wapuuzi weny maks chache kuweza kujitapa na kjlujiona bira kuwa na Degree ni Legacy ya Jakaya Mrisho Kikwete, waliofuatia walipaswa kucement kile alichoasisi. Kaa tafakari, hakuna Rais wa Nchi au Serikali iliowahi kumaliza matatizo ya nchi yake. America kutoa msaada katika kusaidia kaya maskini, haimaanishi ndani ya US kila mtu anajimudu.

Rudi shule, fuatilia maisha ya JK na aina ya uongozi wake na mtazamo wake kuhusu Democracy, Maendeleo na Mifumo ya kitaasisi ndo utamuelewa kwanini bado anang'aa Duniani.
 
Wafuasi wa jiwe ni washamba kuliko hata jiwe lenyewe
 
Assume Sasa hapo mleta mada ndo kapigiwa simu na hao wateuzi kuulizia kama wamteue ama la.

MALAIKA: Omba lolote tutakupa ila jirani yako tutampa mara mbili ya ulichoomba.

JIBU: NATAKA CHONGO.
 
Muda mwingine tupunguze tabia ya kupinga kila kitu.Hivyo mtoa mada unaona waliomchagua JK ni wendawazimu.Mtoa mada anaonekana ni kijana ambae anaongozwa na emotions kuliko facts
 
Ni kweli kabisa,juzi juzi nimewasikia taliban eti wanazuga kuomba msaada kwa usa.nikacheka nikasema hawa watu wanajuana.
 
Shule za kata kamjengea nani asome ??????

Mwanaasha, mtoto wa JK aliyemtambulisha kwenye mazishi ya JPM, hasomi shule za kata! Kwa sababu shule za kata ni dreadful.

His work on quality education front was abysmal. The Jakaya Kikwete's of the third walikaa mbali na miundombinu ya elimu ambayo walitujengea sisi masikini wa kutupwa tukasome.

Jakaya Kikwete as president never gave a rat's arse about equal access to quality education for the dirt-poor children of the country. How on earth can he possibly lead such an effort at a global scale ????????
 
Mtoa maada unajiona una akili Sana Kuliko UN au sio?
Basi Sawa peleka barua Kwa Gutarez akuteue wewe usonge Kwa Wataliban
Yani wewe unamchukulia
JK ni kama jamaa yenu Jiwe?

Walinda Legasi za maturubai mna viroja Sana!
😁😁😁
 
Kwahiyo JK anaenda kupingana na koran ambayo watalibani wanaisimamia..yeye mwenye muislamu..watamuona kakengeuka..sidhani kam watamuelewa mana anaenda kinyume na maandiko ambayo yeye anapaswa kuyasimamia.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawa matelabani wa Sasa wana ahueni mkuu ,kidogo wanauelewa usihofu
Mimi bwana ninalohofia hao mataleban walivyo na vichwa vibovu, wasije wakaatuulia bure mzee wetu. Hayo mambo ya mataleban yabaki kwa hao hao taleban.
 
Nongwa na chuki zako hazimzuii kufanya Kazi aliyotumwa na Dunia..

Hajaanza leo,hata Libya alitumwa nk..

JK kafanya mengi,EPR unayoiona leo ni matunda yake ila kwa kuwa wewe ni mbuzi jike huna unachelewa subiria kupandwa tuu.πŸ‘‡

 
Hawa matelabani wa Sasa wana ahueni mkuu ,kidogo wanauelewa usihofu

Amina mkuu.
πŸ™πŸ™πŸ™
Maana ndiye tunayemtegemea tukivurugana.
The only symbol of unity available at our disposal.
 
Tunakuja kutwangwa.

Tanzania huwa inafanyakazi kubwa behind the scene.

Sasa tunajiweka frontier na tunaenda kuwa target
 
Unauliza Kikwete alifanya nini kwenye elimu
1. Unazijua shule za kata?
2. Unaijua UDOM?
3. Unajua udahili vyuoni uliongezeka kwa kiasi gani enzi za JK?
 
Hivi watoto kusoma shule za Academy ni jambo la kuona aibu, huu upuuzi wa kujifaharisha na unyonge tumeutoa wapi?
 
Mimi bwana ninalohofia hao mataleban walivyo na vichwa vibovu, wasije wakaatuulia bure mzee wetu. Hayo mambo ya mataleban yabaki kwa hao hao taleban.

Sidhani kama ataenda huko Kabul...

Huenda kikao kikawa kupitia mtandao au kikafanyika nchi nyingine tu...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…