bitimkongwe
JF-Expert Member
- Oct 21, 2009
- 7,794
- 7,551
Ndio maana mataifa makubwa kama US huwa wanaidharau hii United Nations na mpaka kutishia kuacha kuchangia...
Sasa Kikwete masikini ya Mungu eti anatumwa aka negotiate na Taliban kurejesha watoto wa kike shule akiwa kama mwenyekiti wa Global Partnership for Education.
Mtu atakaepata mkanda wa mazungumzo ya Kikwete na Taliban atauza filamu ya comedy kali kuliko zote Afrika kama wasipom-behead mkutanoni.
Lakini lengo pana zaidi la GPE ni kupeleka fursa ya elimu bora kwa kila mtoto mnyonge duniani.
Huku nyumbani the Kikwetes of the third world wamefanya nini japo kujaribu kumpa mtoto mnyonge elimu wanayopata watoto wao binafsi? (Kumbuka hotuba ya JK kwenye mazishi ya JPM alivyoeleza bila aibu jinsi watoto wake wanavyosoma shule za academy).
Wanachaguliwa na UN kwa kigezo gani watu hawa hawa waliofeli katika maeneo hayo hayo ya kuleta maendeleo kwa watu masikini?
Kha! at mataifa makubwa kama US huwa wanaidharau UN, sijui ni nani aliyekudanganya kijana. Huyo US angekomaa na kura yake ya VETO, au angekuwa analipa mamilioni ya madola kuihudumia kama angekuwa anaidharau? Kuna post za UN hawezi kupewa raia wa nchi yo yote zaidi ya US, unadhani kwa nini?
Kwa sababu US inajua sana umuhimu wa UN na pale ndipo siasa na influence zinapopigwa.
Halafu enzi za JK si ndiyo alianzisha wanafunzi kupewa mikopo ya vyuo mpaka vile vyuo vya binafsi? Ama kweli tenda wema wende zako.