Jakaya Kikwete: Hayati Rais Mwinyi ndiye aliyenifikisha hapa nilipo leo

Jakaya Kikwete: Hayati Rais Mwinyi ndiye aliyenifikisha hapa nilipo leo

Jambo la uzuri ni kwamba walosoma na mzee Kikwete wapo khasa wale alochangia chumba kimoja cha bweni pale Kibaha.

Na pia wapo wale walosoma nae intake moja pale UDSM.

Wengi tunasahau kwamba familia ya Kikwete ilipewa nafasi gani katika serikali ya awamu ya kwanza na jinsi hayati Mwalimu alivyohakikisha aingalia uzuri familia hii.

Ingawa hapo baadae ikawa shida kidogo na ikawa hadi leo hii. Wakumbukeni mzee Mrisho, Shehe Ramiya na wengineo.

Ila kiukweli baadae mzee Mwinyi alifanya kama anasawazisha pale palipoharibika na JK akaanza kusogea juu na amshukuru sana rafikie Ditopile wa Mzuzuri.
 
Rais mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika kuhani msiba wa Hayati Ali Hassan Mwinyi huko Mikocheni Dar es Salaam ameonekana akiwa na huzuni kubwa sana na masikitiko makubwa akiwa anaongea na vyombo vya habari

Jakaya Kikwete amekiri kuwa yeye hakuwa lolote bali alikuwa katibu wa kawaida wa CCM wilaya ya Masasi huko Mtwara mara baada ya kutoka jeshini miaka hiyo ya 1980's

Kwa mujibu wa Jakaya Kikwete: Rais Mwinyi kwa maono yake ndiye aliyeamua kumtoa huko kijijini Masasi na kumpa ubunge wa viti maalum na baadae kumteua kuwa Naibu Waziri

Jakaya kikwete amesisitiza kwa yeye ni msiba mzito sana kwani amepoteza mtu muhimu kwenye maisha yake aliyamfikisha mpaka hapa alipo kwa sasa

Baada ya maneno hayo ya kukiri kutolewa kijijini Masasi na kuingizwa kwenye mfumo na hayati Rais Mwinyi, Jakaya Kikwete hakutaka kuulizwa maswali mengine toka kwa waandishi wa habari kutokana na majonzi aliyokuwa nayo
Si vibaya lakini mtani Ajue anachanganya wakulugwa, amewahi kulisifu kanisa, wakati mwingine Mwalimu Leo mzee mwinyi, haelezi nafasi ya Baba yake anahofia kuonekana alipewa upendeleo
 
Nchi hii hakuna cheo kama hicho serikalini, kipo chini ya wizara gani hiko cheo?
Dah, we jamaa nimekukumba ndo ulikuwa unakesha humu kutwa kucha eti ujibiwe hoja zako za bandari.
Kwa kimya chako nadhani ulipata majibu
 
Duh! Unaweza soma special school, lakini ukawa huna akili!

Wenzake aliosoma nao University of Dar Es Salaam, Uchumi most of them ni Phd holder's, kina Prof Benno Ndulu ndiyo darasa moja na Jakaya
Seriously?...kipindi Cha wakina Jakaya wachache sana walipata nafasi ya kusoma chuo kikuu! Tena wale wenye uwezo wa kipekee. Kusoma PhD ni maamuzi binafsi. Jakaya tayari alishaona fursa sehemu nyingine. Na akawa na mafanikio kuliko hao wenye PhD
 
Kaka uko sahihi kabisa!

Mimi nilikua natetea kwamba Kikwete kafanya kazi Nachingwea kama Katibu wa CCM Wilaya,Masasi alihamishiwa na sidhani hata mwezi alimaliza akateuliwa kua Naibu Waziri!

1. Nimewahi fanya kazi Lindi na Mtwara,pale Nachingwea ofisi za CCM Wilaya jina la Kikwete lipo kwenye orodha ya Makatibu.

2. Lakini Masasi jina la Kikwete halipo kwenye orodha ya Makatibu wa CCM Wilaya ya Masasi,maana yake Kikwete pale Masasi hakukaa kabisa zaidi yakupita tu!

3. Sawa na Maharage Chande,aliteuliwa kuwa MD wa TTCL,kabla hajaanza kazi akapangiwa kazi nyingine ya MD wa Posta,kwa hiyo Maharage Chande hawezi sema alikua MD wa TTCL wakati hata kazi hakufanya pale!

4. La mwisho kabisa,vijana wa 2000, wana shida sana,hawapingani kwa hoja,wao wanakimbilia matusi na kutweza utu wa mtu,sasa kuna wakati na sisi wazee tunashindwa vumilia,tunatoa kanzu na bargashia tunawashughulia kiswahili swahili! Jamii Forum imekua na vijana wa hovyo sana!

5. Zamani watu tulikua tunajadili kwa hoja zenye ujazo,mtu anakupinga kwa ushaidi,na sio matusi!
Nimekuelewa mkuu ila sijui kwa nini hapo Masasi hawajaweka jina lake kwenye orodha ya makatibu. Ila alikaa kwa muda mrefu kiasi. Hata alisimamia kilimo cha mihogo kwa kushirikiana na serikali ya wilaya ili kuepuka njaa. Na ndiye alikua anamsaidia mbunge mhe Mkapa ambaye alikua waziri wa mambo nje kulilea jimbo coz mkapa alikua na safari nyingi za nje.
Sasa kama alisimamia kilimo cha mihogo hadi akaona matokeo si ina maana alikaa kwa miez mingi?

Pili ni kweli kuna watu, wanapojadili hoja iliyowazidi akili hukimbilia kutukana mtu badala ya kujibu hoja iliyopo mezani. Hiyo sio kwa vijana wa 2000 tu bali ipo kwa watu wote wenye akili ndogo.
 
Hizi ndiyo hoja hua nazipenda sasa,unapinga kwa mifano hadi anayekupa majibu unapata lakujifunza kutoka kwake! Asante kwa hili kaka! Hapa nimeongeza jambo,kumbe Mzee Jakaya alisimamia jambo kubwa sana pale kwa Chinga boy!

Sijajua kwa nini Mzee Jakaya hayupo kwenye orodha ya Makatibu wa CCM wa Wilaya ya Masasi! Kuna siku nitapita pale niulize ulize kiutani!
 
Dah, we jamaa nimekukumba ndo ulikuwa unakesha humu kutwa kucha eti ujibiwe hoja zako za bandari.
Kwa kimya chako nadhani ulipata majibu
Kukumba ndio nini sasa, haya hiko cheo kipo chini ya wizara gani?
 
Rais mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika kuhani msiba wa Hayati Ali Hassan Mwinyi huko Mikocheni Dar es Salaam ameonekana akiwa na huzuni kubwa sana na masikitiko makubwa akiwa anaongea na vyombo vya habari

Jakaya Kikwete amekiri kuwa yeye hakuwa lolote bali alikuwa katibu wa kawaida wa CCM wilaya ya Masasi huko Mtwara mara baada ya kutoka jeshini miaka hiyo ya 1980's

Kwa mujibu wa Jakaya Kikwete: Rais Mwinyi kwa maono yake ndiye aliyeamua kumtoa huko kijijini Masasi na kumpa ubunge wa viti maalum na baadae kumteua kuwa Naibu Waziri

Jakaya kikwete amesisitiza kwa yeye ni msiba mzito sana kwani amepoteza mtu muhimu kwenye maisha yake aliyamfikisha mpaka hapa alipo kwa sasa

Baada ya maneno hayo ya kukiri kutolewa kijijini Masasi na kuingizwa kwenye mfumo na hayati Rais Mwinyi, Jakaya Kikwete hakutaka kuulizwa maswali mengine toka kwa waandishi wa habari kutokana na majonzi aliyokuwa nayo
sawa
 
Mkuu,

Tatizo ni kwamba, Watanzania hawana consistency wanataka nini.

Siko hapa kumtetea Nyerere, ana mapungufu yake, mengi. Mengi tumeyaongea hata kwenye thread ya kuangalia kama Nyerere alikuwa mkoloni nimetaja mazuri na mabaya yake, wiki ya jana tu hapo, napenda kuangakia ideas kuliko watu.

Ila, kwa sababu umemtaja Nyerere, naweza kumzungumzia kimuktadha, naweza kusema mara nyingine tunamuonea.

Nyerere analaumiwa kwa kufanya jambo, na hapo hapo analaumiwa kwa kutofanya jambo hilo hilo. Lawama hizi zinatuonesha sisi Watanzania tulivyo walalamishi kuliko mapungufu ya Nyerere.

Kwa mfano, kwenye hilo la kuandaa wenzake na kuweka mfumo wa kuandaa wengine, grooming, Nyerere alijitahidi sana kuwaandaa kina Salim Ahmed Salim nankina Mkapa toka wadogo. Salim aliandaliwa kimataifa. Bado kidogo awe Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kama si inda ya Wamarekani.

Na huyo ndiye Nyerere alimtaka awe rais. Lakini Wazanzibari wakaleta figusu zao, wakamkataa, wakasema huyu muarabu, huyu Hizbu. Hakupita.

Nyerere akaachia demokrasia ichukue mkondo wake, akawa mdogo. Akakubali matokeo licha ya mgombea aliyemtaka kutofanikiwa. Hapo utamlaumu kwamba hakuandaa watu?

Na angetaka kulazimisha mgombea wake apite, hapo napo mngemlaumu. Nyerere katumia nguvu kupitisha mgombea wake, licha ya Wazanzibari kumkatalia, Wazanzibari wanaburuzwa na Nyerere, Nyerere hafuati demokrasia.

Unaona dilemma ya kuwa Nyerere Tanzania?

Unalaumiwa kwa maamuzi yoyote yale utakayochukua.
Anyway pamoja na lawama zote Nyerere analaumiwa Kwa kuchagua Sera mbovu za kijamaa ambazo hazikuinufaisha nchi saana kuiingiza kwenye migogoro yakiuchumi

Vile vile aliendekeza mapenzi yake binafsi na Milton Obote na kulitia taifa katika vita iliyoharibu uchumi wetu.

Nyerere Alibana Uhuru wakisiasa akasabbisha kutokuwa na democrasia.

Anyway Nyerere bado anavyakulaumiwa. Hakuwa easily flexible kunusa hatari ya Sera zake kwamba hatotoboa mbele ya mabeberu. Alipaswa kuachana na azimio la Arusha miaka ya 1977's hivi...
 
Jambo la uzuri ni kwamba walosoma na mzee Kikwete wapo khasa wale alochangia chumba kimoja cha bweni pale Kibaha.

Na pia wapo wale walosoma nae intake moja pale UDSM.

Wengi tunasahau kwamba familia ya Kikwete ilipewa nafasi gani katika serikali ya awamu ya kwanza na jinsi hayati Mwalimu alivyohakikisha aingalia uzuri familia hii.

Ingawa hapo baadae ikawa shida kidogo na ikawa hadi leo hii. Wakumbukeni mzee Mrisho, Shehe Ramiya na wengineo.

Ila kiukweli baadae mzee Mwinyi alifanya kama anasawazisha pale palipoharibika na JK akaanza kusogea juu na amshukuru sana rafikie Ditopile wa Mzuzuri.
Ubaya na uzuri wa wabongo ni watu wa kujipendekeza pendekeza kwa watu wenye uwezo !
Hivyo basi hata hao ungeamini wanaujua ukweli hawatasema ukweli Abadan kama wanajua jamaa yao au swahiba wao hapendi ukweli ukajulikana !
Iko vile !!
 
Back
Top Bottom