Hua tunasagiwa sana kunguni na (haters) wanaotujua ili wawaaminishe wale(haters) wasiotujua!Hapo kwenye kuwa bright nakataa kwani 99% ya aliosoma nao hasa Chuo Kikuu wanasema alikuwa Mchovu kama akina Fred Michael na Papa Job wa Simba SC.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hua tunasagiwa sana kunguni na (haters) wanaotujua ili wawaaminishe wale(haters) wasiotujua!Hapo kwenye kuwa bright nakataa kwani 99% ya aliosoma nao hasa Chuo Kikuu wanasema alikuwa Mchovu kama akina Fred Michael na Papa Job wa Simba SC.
NextUsilolijua ni sawa na usiku wa giza......lala tu bwana mdogo.
Haters wa JK kazi mnayo; mtamzushia na mtasema kila kitu ila jamaa, kwa uwezo wa Mungu, mtamuona anadunda tu mamamamamamae zenu.
Huo ndio ukweli, ila dini yake ilimsaidia. Alimteua kuwa mbunge, akampatia uwaziri wa Nishati, Maji na Madini 1994. JK alivyo na tamaa akagombea urais 1995.Rais mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika kuhani msiba wa Hayati Ali Hassan Mwinyi huko Mikocheni Dar es Salaam ameonekana akiwa na huzuni kubwa sana na masikitiko makubwa akiwa anaongea na vyombo vya habari
Jakaya Kikwete amekiri kuwa yeye hakuwa lolote bali alikuwa katibu wa kawaida wa CCM wilaya ya Masasi huko Mtwara mara baada ya kutoka jeshini miaka hiyo ya 1980's
Kwa mujibu wa Jakaya Kikwete: Rais Mwinyi kwa maono yake ndiye aliyeamua kumtoa huko kijijini Masasi na kumpa ubunge wa viti maalum na baadae kumteua kuwa Naibu Waziri
Jakaya kikwete amesisitiza kwa yeye ni msiba mzito sana kwani amepoteza mtu muhimu kwenye maisha yake aliyamfikisha mpaka hapa alipo kwa sasa
Baada ya maneno hayo ya kukiri kutolewa kijijini Masasi na kuingizwa kwenye mfumo na hayati Rais Mwinyi, Jakaya Kikwete hakutaka kuulizwa maswali mengine toka kwa waandishi wa habari kutokana na majonzi aliyokuwa nayo
Kwl, magu alikuwa mwovuBila shaka Makamba amemuweka JK kwenye nafasi ya juu kabisa katika lile kundi la "wema hawafi"
Mnafiki ni weweNi kawaida ya mtu mnafiki na mwenye ghilba daima kupenda kuonekana ni mwema zaidi na anapendwa zaidi.
Ila kwa Kikwete hampati mtu tena. Ulimwengu wote unamjua kwa unafiki wake.
Kwa akili za kishuleshule huo ndo mtazamo wako. Yaani kuwa bright ni kufaulu masomo ya darasani.Hapo kwenye kuwa bright nakataa kwani 99% ya aliosoma nao hasa Chuo Kikuu wanasema alikuwa Mchovu kama akina Fred Michael na Papa Job wa Simba SC.
Kumchukia JK ni kujitafutia maradhi ya kujitakia tuKwa nchi zenye Watu Makini na Werevu huyu hivi sasa angekuwa Jela anataabika tu.
Kumbuka alisoma Kibaha sekondari Shule ya vipaji maalumHapo kwenye kuwa bright nakataa kwani 99% ya aliosoma nao hasa Chuo Kikuu wanasema alikuwa Mchovu kama akina Fred Michael na Papa Job wa Simba SC.
Binadamu, haswa wanaume, tumeumbwa kutafuta zaidi na kushindana zaidi......usiwe bwege wewe. Au mwenzetu umeleft nn mpaka unaongea maneno 'laini laini' kiasi hicho?!!!!Huo ndio ukweli, ila dini yake ilimsaidia. Alimteua kuwa mbunge, akampatia uwaziri wa Nishati, Maji na Madini 1994. JK alivyo na tamaa akagombea urais 1995.
Umemaliza kila kitu na uzi ufungwe,Rc Ukiwaona Mwinshehe Ditopile Mzuzuri ndiye aliyemtengenezea cross pass kwa kumtambulisha kwa Rais Hayati Mwinyi !
Kwahiyo Swahiba wake ndiye hasa aliyeanzisha ile move iliyompandisha mhe Kikwete !
Na huyo sio mwingine bali ni Ukiwaona Mwinshehe Ditopile Mzuzuri !!
Ukweli utatuacha Huru 🙏🙏 !
Mkuu, hakuna mwanasiasa asiye na tamaaHuo ndio ukweli, ila dini yake ilimsaidia. Alimteua kuwa mbunge, akampatia uwaziri wa Nishati, Maji na Madini 1994. JK alivyo na tamaa akagombea urais 1995.
Nchi hii hakuna cheo kama hicho serikalini, kipo chini ya wizara gani hiko cheo?Amiri Jeshi Mkuu mstaafu na Rais mstaafu wa JMT cheo ambacho kati ya watanzania milioni 60 tuliopo na zaidi ya milioni 100 waliopita ni watu 6 tu ndo walobahatika kukipata
Kaka uko sahihi kabisa!Hamna haja ya kutukanana. JK amefanya kazi Masasi ambako alihamia kutokea Nachingwea. Na aliteuliwa kuwa mbunge akiwa katibu wa CCM wa wilaya ua Masasi mbona hilo liko wazi mkuu!!
Duh! Unaweza soma special school, lakini ukawa huna akili!Kumbuka alisoma Kibaha sekondari Shule ya vipaji maalum
Masuala ya kisiasa Hata AI inazimia ikiulizwa mambo hayo. Nadhani umenielewa.Mwinyi.Na kwamba hakuwa na connection yeyote,kwa kuwa alikuwa katibu wa CCM tu pale Masasi. Cheo cha chini kabisa. Nyuz nyingi humu zinakuwa chai tu.
Wema hawafi!Huenda kifo alichomaanisha makamba si kifo cha mwili bali utawala. Makamba Jr, Mwinyi Jr,Ridhiwani wote hawa ni watawala wajao.
Duh! Unaweza soma special school, lakini ukawa huna akili!
Wenzake aliosoma nao University of Dar Es Salaam, Uchumi most of them ni Phd holder's, kina Prof Benno Ndulu ndiyo darasa moja na Jakaya
Mmh ulitafuta sababu ukajiridhisha? Kina Zuckerberg na vipawa vyao ni dropoutDuh! Unaweza soma special school, lakini ukawa huna akili!
Wenzake aliosoma nao University of Dar Es Salaam, Uchumi most of them ni Phd holder's, kina Prof Benno Ndulu ndiyo darasa moja na Jakaya
Kweli umeandika ukweli 100 %Kaka uko sahihi kabisa!
Mimi nilikua natetea kwamba Kikwete kafanya kazi Nachingwea kama Katibu wa CCM Wilaya,Masasi alihamishiwa na sidhani hata mwezi alimaliza akateuliwa kua Naibu Waziri!
1. Nimewahi fanya kazi Lindi na Mtwara,pale Nachingwea ofisi za CCM Wilaya jina la Kikwete lipo kwenye orodha ya Makatibu.
2. Lakini Masasi jina la Kikwete halipo kwenye orodha ya Makatibu wa CCM Wilaya ya Masasi,maana yake Kikwete pale Masasi hakukaa kabisa zaidi yakupita tu!
3. Sawa na Maharage Chande,aliteuliwa kuwa MD wa TTCL,kabla hajaanza kazi akapangiwa kazi nyingine ya MD wa Posta,kwa hiyo Maharage Chande hawezi sema alikua MD wa TTCL wakati hata kazi hakufanya pale!
4. La mwisho kabisa,vijana wa 2000, wana shida sana,hawapingani kwa hoja,wao wanakimbilia matusi na kutweza utu wa mtu,sasa kuna wakati na sisi wazee tunashindwa vumilia,tunatoa kanzu na bargashia tunawashughulia kiswahili swahili! Jamii Forum imekua na vijana wa hovyo sana!
5. Zamani watu tulikua tunajadili kwa hoja zenye ujazo,mtu anakupinga kwa ushaidi,na sio matusi!