Jakaya Kikwete: Hayati Rais Mwinyi ndiye aliyenifikisha hapa nilipo leo

Jambo la uzuri ni kwamba walosoma na mzee Kikwete wapo khasa wale alochangia chumba kimoja cha bweni pale Kibaha.

Na pia wapo wale walosoma nae intake moja pale UDSM.

Wengi tunasahau kwamba familia ya Kikwete ilipewa nafasi gani katika serikali ya awamu ya kwanza na jinsi hayati Mwalimu alivyohakikisha aingalia uzuri familia hii.

Ingawa hapo baadae ikawa shida kidogo na ikawa hadi leo hii. Wakumbukeni mzee Mrisho, Shehe Ramiya na wengineo.

Ila kiukweli baadae mzee Mwinyi alifanya kama anasawazisha pale palipoharibika na JK akaanza kusogea juu na amshukuru sana rafikie Ditopile wa Mzuzuri.
 
Si vibaya lakini mtani Ajue anachanganya wakulugwa, amewahi kulisifu kanisa, wakati mwingine Mwalimu Leo mzee mwinyi, haelezi nafasi ya Baba yake anahofia kuonekana alipewa upendeleo
 
Nchi hii hakuna cheo kama hicho serikalini, kipo chini ya wizara gani hiko cheo?
Dah, we jamaa nimekukumba ndo ulikuwa unakesha humu kutwa kucha eti ujibiwe hoja zako za bandari.
Kwa kimya chako nadhani ulipata majibu
 
Duh! Unaweza soma special school, lakini ukawa huna akili!

Wenzake aliosoma nao University of Dar Es Salaam, Uchumi most of them ni Phd holder's, kina Prof Benno Ndulu ndiyo darasa moja na Jakaya
Seriously?...kipindi Cha wakina Jakaya wachache sana walipata nafasi ya kusoma chuo kikuu! Tena wale wenye uwezo wa kipekee. Kusoma PhD ni maamuzi binafsi. Jakaya tayari alishaona fursa sehemu nyingine. Na akawa na mafanikio kuliko hao wenye PhD
 
Nimekuelewa mkuu ila sijui kwa nini hapo Masasi hawajaweka jina lake kwenye orodha ya makatibu. Ila alikaa kwa muda mrefu kiasi. Hata alisimamia kilimo cha mihogo kwa kushirikiana na serikali ya wilaya ili kuepuka njaa. Na ndiye alikua anamsaidia mbunge mhe Mkapa ambaye alikua waziri wa mambo nje kulilea jimbo coz mkapa alikua na safari nyingi za nje.
Sasa kama alisimamia kilimo cha mihogo hadi akaona matokeo si ina maana alikaa kwa miez mingi?

Pili ni kweli kuna watu, wanapojadili hoja iliyowazidi akili hukimbilia kutukana mtu badala ya kujibu hoja iliyopo mezani. Hiyo sio kwa vijana wa 2000 tu bali ipo kwa watu wote wenye akili ndogo.
 
Hizi ndiyo hoja hua nazipenda sasa,unapinga kwa mifano hadi anayekupa majibu unapata lakujifunza kutoka kwake! Asante kwa hili kaka! Hapa nimeongeza jambo,kumbe Mzee Jakaya alisimamia jambo kubwa sana pale kwa Chinga boy!

Sijajua kwa nini Mzee Jakaya hayupo kwenye orodha ya Makatibu wa CCM wa Wilaya ya Masasi! Kuna siku nitapita pale niulize ulize kiutani!
 
Dah, we jamaa nimekukumba ndo ulikuwa unakesha humu kutwa kucha eti ujibiwe hoja zako za bandari.
Kwa kimya chako nadhani ulipata majibu
Kukumba ndio nini sasa, haya hiko cheo kipo chini ya wizara gani?
 
sawa
 
Anyway pamoja na lawama zote Nyerere analaumiwa Kwa kuchagua Sera mbovu za kijamaa ambazo hazikuinufaisha nchi saana kuiingiza kwenye migogoro yakiuchumi

Vile vile aliendekeza mapenzi yake binafsi na Milton Obote na kulitia taifa katika vita iliyoharibu uchumi wetu.

Nyerere Alibana Uhuru wakisiasa akasabbisha kutokuwa na democrasia.


Anyway Nyerere bado anavyakulaumiwa. Hakuwa easily flexible kunusa hatari ya Sera zake kwamba hatotoboa mbele ya mabeberu. Alipaswa kuachana na azimio la Arusha miaka ya 1977's hivi...
 
Ubaya na uzuri wa wabongo ni watu wa kujipendekeza pendekeza kwa watu wenye uwezo !
Hivyo basi hata hao ungeamini wanaujua ukweli hawatasema ukweli Abadan kama wanajua jamaa yao au swahiba wao hapendi ukweli ukajulikana !
Iko vile !!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…