Jakaya Kikwete na Ridhiwani, wageni rasmi kwenye sherehe za Jando na Unyago huko Msoga

Una Stress mbaya mno ondosha Kwa chuki iliyopo ndani ya nafsi yako ili ubaki mwema kama ulivo.Kinachokusumbua ni chuki iliyopo ndani mwako.
 
Uko sahihi mkuu
Kitu pekee ambacho watu wasichojua ni kuwa, huko watoto hawapelekwi kutahiliwa siku hizi, wanatahiliwa hospital isipokuwa kwenye jando na unyago unaenda kufundishwa elimu mbalimbali za kimila, kijamii pamoja na kufanya matambiko kwenye mizimu.
 
Huyu mzee anapenda sana hizo shughuli, kuna kipindi alikuwa hakauki kule kwa mfalme Mswati wa Swaz
 
Safi sana. Ni vizuri kuendeleza mila nzuri za jadi. Big sana Wakwere kwa kudumisha mila
 
sawa, swali je ridhwani alipelekwa unyago na raisi kikwete? au yeye ridhwani kama ana mtoto kampeleka kwenye huo unyago? jibu lake wewe mwenyewe unalijua kwamba ni no, sasa kwa nini huo unyago kama ni mzuri uwe kwa watoto wa wengine tu?
Mtoto wa riz yupo hapo ..na yy mwenyewe na Dada ake Dr salama wote wamekaa unyago

Kwa JK huo utamaduni uko toka akiwa mambo ya nje hadi sasa
 
Hivi vitu tuna vidharau ila ndivyo vilivyo toa wazee mashababi na wanawake bora.

Siku hizi ni vice versa,tumewaachia wapiga soga wa mitandaoni na wanasaikolojia. Kuna kuna mtu sababu tu ya uwezo wake wa kifedha,watoto zake wakisha balehe ana wapeleka kwa wanasaikolojia, upuuzi mtupu. Utakuta hata yy mwenyewe hajampa basic ya nini cha kufanya baada ya kubalehe.
 
Hao walichezwa ngoma tu tunaita, sio kutailiwa wala kukeketwa. Hao wamefundishwa tu tamaduni, nadhani kikwete amefikiria yeye yupo pale msoga ila hafanyi hivo vtu wakati jamii inayo mzunguka hucheza ngoma kila mara watoto wao wakifika umri flani.
Na kikwete wala mwanae hawakua wageni rasmi. Wao ndio wenye shughuli, hao ni wajukuu wa kikwete wote. Hamna haramia hapo, na pia ni watoto baadhi ya ridhiwani kikwete,ally kikwete na watoto wa wajukuu wa dada wa kikwete.
Hyo ilikua shughuli ya kifamilia. Na hata siku ya pili,familia nyingine hapo msoga ilifanya kitukama hiko.
Wakwere kwa ngoma. Ndio hyo sasa
 
Wajukuu zake wapo hapo …
 
Kitu pekee ambacho watu wasichojua ni kuwa, huko watoto hawapelekwi kutahiliwa siku hizi, wanatahiliwa hospital isipokuwa kwenye jando na unyago unaenda kufundishwa elimu mbalimbali za kimila, kijamii pamoja na kufanya matambiko kwenye mizimu.
Haya ni mambo ya kijima na ya zama za giza.
 
Sawa sawa uko sahihi kbs
 
Angetembelea Mbowe leo wote wangekuwa mahakamani kwa kosa la utesaji watoto.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…