Infinite_Kiumeni
JF-Expert Member
- Jan 23, 2023
- 382
- 687
Matokeo yoyote yanatokana na mchakato/ mfumo fulani.
Hasa matokeo yatakayokupa furaha na maendeleo kwa muda mrefu.
Kujali mchakato ni kufanya kila unachotakiwa kufanya kwa muda huu bila kujali unavyojiskia, hatua inayofuata au matokeo yatakuaje.
Mchakato unahitaji nguvu zako kila siku.
Ukiwa unajali matokeo tu ya kile unachokifanya hautoona fursa nyingine kirahisi, hautaona maendeleo uliyopata na ni rahisi kukata tamaa.
Pia utakua unajiaminisha kwamba kuweka nguvu katika unachokifanya ni vibaya hasa kama huoni matokeo haraka.
Jambo linalosababisha utake vitu vya haraka haraka na kuepuka mchakato wa kupata kitu cha muda mrefu.
Mfano, ni rahisi kukaa kuangalia muvi kuliko kuweka nguvu kwenye kujiendeleza kwenye masomo au kazi, sababu mchakato ni mrefu.
Ni rahisi kuangalia X na kupiga puchu. Ina matokeo ya haraka kuliko kujizuia na kupitia changamoto ya kupata mpenzi anayekufaa.
Katika hayo utaona kufata mchakato fulani ili upate matokeo unayotaka kwa muda mrefu ni ngumu na utaona ni mbaya.
.
Cha kufanya
Jiwekee mfumo kwa ajili matokeo unayotaka.
Nenda hatua kwa hatua.
Usikimbilie matokeo fulani.
Anza kujipongeza kwa kila hatua.
Itakufunza kuamini mchakato ni mzuri.
Hata kama mambo hayajaenda vizuri jikumbushe umeshinda kwa kuwa umefata mfumo uliojiwekea.
Jitengenezee mazingira yanayorahisisha mfumo.
Mazingira yatakayokushawishi ufuate mchakato wako.
Mfano, unataka kupunguza uzito, anza na mazingira ya kile unachoingiza mdomoni. Jiandalie msosi wako wa kesho leo. Na uweke karibu vile vitakavyokusaidia katika safari yako.
Kiasi kwamba hata ukiona chakula kingine tayari unakua umeshiba.
Mfano, unataka kuacha puchu, jiulize mazingira mapya yako bila punyeto yatakuaje? Kisha yatengeneze hayo.
Ukiweka nguvu zako kwenye mfumo ni rahisi kurudi mchezoni hata kama umekatishwa tamaa na jambo fulani.
Muhimu, usikate tamaa katika ili kupata matokeo utakayo ya muda mrefu.