Thecoder
JF-Expert Member
- Aug 10, 2015
- 1,590
- 4,244
Hapa nadhani kuna utofauti wa ile kutokuwapigia simu wakwe zako ili hali watu wengine unawasiliana nao vizuri ila pia kuna ile ya wakina sisi ya kutokua mtu wa simu kabisa, haijalishi ni ukweni au nyumbani au kwa watu wengine, yaani iko hivyo kwamba sio mtu wa kuwasiliana na watu kwa njia ya simu mara kwa mara.Bora iwe hivo japo imenishangaza mm navoelewa mkishaona familia zinaungana
Wakwezako ni wajibuwako kuwaangalia na wazaziwako ni wajibu wa mke pia kuwaangalia
Unajisikiaje mkeo akiwatenga nduguzako?
Kwakweli hapana utu hamna Bora uwe mvivu lakin uweke akilinj kuwa kukuozesha sio Kwamba hawamtaki nduguyao na ndio maana hata ukimuacha na watoto watano ndugyzake watampokea pale ndo damuyake ilipo
Kwa yule ambae anawasiliana na wazazi wake pamoja na ndugu zake wengine vizuri ila anashindwa kuwasiliana na wazazi au ndugu wa mkewe huyo ni mbinafsi, kwa maana mkishaoana tayari mshakua ndugu kwa namna moja au nyingine.
Ila kwa watu kama sisi ni character tu ndio zinatusumbua, kwamfano nikijizungumzia Mimi ni kwamba niko comfortable sana kwenye kuchat kuliko kuongea kwa simu, kwahiyo wanaonifahamu huwa wanaelewa hivyo.
Sasa shida inakuja unapokua na mkwe ambae umri umesonga, inakua ngumu kuanza kumjulia hali kwa msg na badala yake unajikuta tu kwamba imepita muda mrefu hujawasiliana na mkweo, ingawaje mashemeji na wengineo wa upande huo mnaweza kuwasiliana.