Jamaa alieoa dada yangu mgumu kuwasiliana na sisi ndugu wa mkewe

huyu jamaa ni kweli tulimkabidhi dada yetu kifamilia, lakini baada ya miezi 6 kupita kuwasiliana adi tumpigie sisi, na sisi tumeamua hatutomtafuta akijisikia sawa tu, jengine bado hajamalizia mahari, kuhus maisha wanaishi vizuri na dada yetu ila sina uhakika 100%.nyie vijana acheni zadhau, tu nampigia tu dada yetu. yeye no.
Akili za kimaskini hizi. Sema unadai mahari sasa gia ya kuingilia ndo tatizo.
Kwenye mahusiano mengi mashemeji wengi wanawaza kupiga hela tuu. issue za mahusiano ooh kupiga simu ni geresha tuu. kwani wao wanakatazwa kupiga simu? Mimi ndoa yangu ina zaidi ya miaka 15 kwa sasa ila nimeamua kuchinjia baharini mijinga jinga yote inayoitwa mashemeji. Nilioa, nikalipa mahari yote, nilihangaika baba yao alipoumwa hadi akafariki tukaenda tukazika. Miaka michache baadaye mama yao akaumwa nikahangaika naye hadi nikamchukua nikamleta kwangu kumuuguza kila kitu nikawa nagharimikia hadi bima nikamkatia. Hapo kuna mashemeji wakikwama kidogo wanampigia dada yao ananiambia kwa huruma nawasaidia.Baadaye mama akaforce kurudi kwao nikamrudisha. Tukaendelea kumuuguza hadi akafariki nilienda nikagharimikia almost nusu ya gharama zote za msiba. baada ya mwaka, mama yangu mzazi akafariki. Umbali wa mahali msiba wa mama yangu ulipotokea na kwa wakwe zangu nauli ni sh 5000. Lakini hakuna aliyekanyaga kwa kisingizio cha kukosa nauli, mashemeji zangu wana familia zao, mwingine anamiliki duka, mwingine mashine ya kusaga na mashamba kibao. Nikawapa taarifa kwamba sisi tumeandaa gari Costa kusafirisha mwili pamoja na abiria basi mwakilishi afike atasafiri na kurudi bure. Maana yake akisafiri hadi msiba ulipotokea gharama a kusafiri kwenda kwetu ni bure, takriban nauli ya kwenda na kurudi isingepungua 50k. bado hakuna aliyetokea. Yaani wao wameshindwa kuchangishana hata wamtume mmoja aje wawakilishe? Gari lililokodiwa lilienda na abiria pungufu, Nilienda msibani na mke wangu tuu. Wao haya kuja hawakuja, basi hata salamu za rambirambi hata wangechangishana wakatuma hata kwa M Pesa hata elf moja haikutumwa.

Baada ya miaka michache napigiwa na Bwashemeji ananiambia mbona sipigi simu wala siendi kuwatembelea? au kwa vile wazazi wamefariki wote sasa hata wao siwatembelei? Niliwaza cha kumjibu sikupata. Mimi ni wa muhimu kwao as far as nawapa chochote, ila kibao kikigeuka kwangu hawana muda.Basi kila mtu ashinde mechi zake
 
Kwahio unataka awasiliane na nyie ili awalipie mahali familia nzima awaoe..? Nyie mbona wapuuzi kias hiko..? Amemuoa binti yenu hajaoa familia nzima kenge nyie... Kama kuna ulazima wa kuwapigia cm kuwasalimia au kuwajulisha atafanya hivyo, kama haoni ulazima muacheni wapuuzi nyie... Mnaonekana mnapenda sana umbea na kufuatilia maisha ya watu ndio maana anawakwepa...
Halafu mtambue kuna watu amani yao ya moyo ni kutokuwasiliana na watu hovyo, wanapenda maisha binafsi tu...
Kama mnataka taarifa na kusalimiwa binti yenu ndie afanye hivyo maana yeye ndie ndugu yenu sio mumewe...
 
huyu jamaa ni kweli tulimkabidhi dada yetu kifamilia, lakini baada ya miezi 6 kupita kuwasiliana adi tumpigie sisi, na sisi tumeamua hatutomtafuta akijisikia sawa tu, jengine bado hajamalizia mahari, kuhus maisha wanaishi vizuri na dada yetu ila sina uhakika 100%.nyie vijana acheni zadhau, tu nampigia tu dada yetu. yeye no.
Hana undugu na nyie na mazoea,mwashe kijana wa watu ajibandulie dada yenu,subirini azae wapwa zenu!Hao ndio damu yenu watawasiliana na nyie wakikua.
 
huyu jamaa ni kweli tulimkabidhi dada yetu kifamilia, lakini baada ya miezi 6 kupita kuwasiliana adi tumpigie sisi, na sisi tumeamua hatutomtafuta akijisikia sawa tu, jengine bado hajamalizia mahari, kuhus maisha wanaishi vizuri na dada yetu ila sina uhakika 100%.nyie vijana acheni zadhau, tu nampigia tu dada yetu. yeye no.
Wewe nae kama mpumbavu au unataka uolewe wewe
 
huyu jamaa ni kweli tulimkabidhi dada yetu kifamilia, lakini baada ya miezi 6 kupita kuwasiliana adi tumpigie sisi, na sisi tumeamua hatutomtafuta akijisikia sawa tu, jengine bado hajamalizia mahari, kuhus maisha wanaishi vizuri na dada yetu ila sina uhakika 100%.nyie vijana acheni zadhau, tu nampigia tu dada yetu. yeye no.
Amemuoa dada yako au wewe ? Anambato dada yako au nyie ?
 
Kwahio unataka awasiliane na nyie ili awalipie mahali familia nzima awaoe..? Nyie mbona wapuuzi kias hiko..? Amemuoa binti yenu hajaoa familia nzima kenge nyie... Kama kuna ulazima wa kuwapigia cm kuwasalimia au kuwajulisha atafanya hivyo, kama haoni ulazima muacheni wapuuzi nyie... Mnaonekana mnapenda sana umbea na kufuatilia maisha ya watu ndio maana anawakwepa...
Halafu mtambue kuna watu amani yao ya moyo ni kutokuwasiliana na watu hovyo, wanapenda maisha binafsi tu...
Kama mnataka taarifa na kusalimiwa binti yenu ndie afanye hivyo maana yeye ndie ndugu yenu sio mumewe...
Mimi ni mmojawapo ya watu wasitaka kuwasiliana sana yaani energy yangu ipo katika ubinafsi wa mambo yangu.
 
Back
Top Bottom