Kuna mmoja kapata VVU juzi alikuwa anajisifia kama wewe, alipotuonyesha demu, tukamwambia huyo dada mumewe ni mgonjwa, alipofuatilia akakuta kweli ni mgonjwa na alikuwa hataki kutumia dawa akisema hawezi kujichoresha eti anaenda kupewa dawa.
Jamaa alipoujua ukweli akaliuliza hilo pisi kali kuhusu ugonjwa, hilo pisi likasema nani ka kwambia, likamwambia hata wao hawajui maradhi ya huyo mumewe, wao waliambiwa ana kisukari sugu, na siyo VVU.
Jamaa alipoenda kupimwa kakutwa na maambukizi, katudanganya kaambiwa majibu yatatoka baada ya miezi 3 hadi 6.
Sisi tunamfahamu, kawa mpole ghafla, anakunywa pombe sio za kawaida, hataki kusema ukweli, habari za pisi kali hazisemi tena.
Ujanja umemuisha. Ana mke na watoto wawili wakubwa wako chuo.
Mnapolegezewa masharti muwe mnajiuliza pia kuhusu magonjwa. Unaweza kudhani umepata kumbe umepatwa.