Jamaa anamuoa mchumba wa rafiki yake kama mke wa pili

Lakini huyo mwanamke mwenzetu hakutumia akili kwasababu mleta mada kasema bibie amesomeshwa , akatafutiwa kazi, akapangiwa nyumba nzima plus gari la kutembelea,.. hakuna mwanaume ambae Hana malengo na ww anaweza kukufanyia hayo yote ilikuwa ni uvumilivu ndo ulihitajika Kwa huyo mdada ..
 
Karma lazima ije ifanye kazi yake kwa huto mwanamke na wazazi wake

Yaani hao wazazi wamesaidiwa mtoto wao kusomeshwa na kutafutiwa kazi kweli bado wakawa hawamkubali jamaa?

Yaani mtu asomeshe mtoto wenu halafu asimuoe yaani jamaa awe amefanya kazi bure...hao wazazi hawakujiuliza Hilo?

Hawakujiuliza hiyo miaka minne ya uchumba mtoto wao kafanyiwa nini na huyo jamaa?

Yaani Kama huyo mwanamke kafanyiwa kila kitu na jamaa Basi lazima angeolewa nae

Maswali hayo hapo juu wazazi hawakujiuliza huko ni kukosa shukran kabisa na watajuta aisee

We mwambie jamaa atulie tu asikilizie kama huyo mwanamke hajarudi huku analia..

Na huyo jamaa mpumbavu Sana mpunguzeni Kama vipi yaani inawezekana kabisa ndani ya hiyo miaka minne alikua na yeye anatembea nae kisiri Siri daah
Hakufikiria madhara ya yeye kumchukua na kumuoa mchumba wa rafiki yake Tena mke wa pili wakati rafiki yake Hana hata mmoja ndo huyo anaetegemea amuoe?
Aisee Hilo lijamaa mlipunguze tuu halina maana mkuu

Hata wewe mleta mada angalia asije kukuolewa mke wako awe mke wake wa 3


Anyway mkuu hebu tuambie na sisi ni bidhaa gani mnauza maana zinaonekana zina hela sanaaa na sisi tuanze kuuza
 

Hauko sahihi

Amwache tu aolewe.

Na nyie mmezidi uchumba miaka 4 mtu mpaka ana hofu hataolewa.
 
Hiviiii we jamaa unamuamini tena huyo bidada?Kama aliweza kuficha hayo mambo anayo kuambia sasa hivi huoni kwamba atauvuruga huo urafiki wenu unaosema mmeshakuwa ndugu?Kwanini hakuyasema hayo kabla na aseme sasa hivi maji ya shingo yameshamfika.Huo ushauri wa kutorosha ndy atamuambia huyo B.Ndy hapo mtakapo vurugana mamen kisa huyo bidada
 
Anahitaji kuzibuliwa kibao aamka usingizini hivi imagine kama watu wanaokuzunguka wana mawazo hayo unasaidikaje?
 

Huku mbele sasa nahisi kuna chai.

Mafuta ya 350,000 kwa gari gani?

Semi tella?

Na kama ana gharamia hivyo, kwanini familia ya binti haimtaki na inamtaka huyo mwingine? Tena si wa dini yao? Na walianzaje kumtaka? Aliwatambulisha?
 
Mchumba hasomeshwi na mapenzi hayanunuliwi full stop!
 
Tafuta wazee wenye busara ambao wanaweza kumuangalia huyo unayemwota dogo kama mtoto wao waongee na wazazi wa huyo mwanamke na viongozi wa dini ili waweze kulichukua hilo Jambo kama la mtoto wao
 
Na mkiwa mnasomeshwa muwe mnakataa sasa
Ni wachache sana yaani mbele ya pesa lazima ukubali(hasa mtu akiwa na shida)yaani hata kama kugegeda hawezi utampenda hivohivo
Kila siku tunawambia mchumba hasomeshwi na mapenzi hayanunuliwi
Unakaa na mtu miaka minne mpaka anachumbiwa na mahari inapelekwa hujui una akili kweli?
 
Nb ushauri wako haukubaliki Mwanamke anayelazimishwa anatoa taarifa kwa mtu wake kama rafiki wa karibu hakikisha unawatenganisha inawezekana kwa sasa ni ngumu lakini mbeleni utaona matunda coz kwa maelezo ya Mwanamke inaonekana B anahudumia sana hiyo familia toka kitambo hivyo sio bahati mbaya
 
Hayo Mambo aliyofanyiwa na jamaa alafu asimuoe?
Kwani michepuko hawafanyiwagi hayo?

Lakini naona harufu ya chumvi kidogo.

Umpangishie nyumba, umnunulie na gari, halafu usioe kisa unasubiri nyumba iishe....thubutuuu

Na hakuna binti wa hivyo akubali kuolewa mke wa pili, kisa ndoa tu?
Nina mashaka.
 
Hayo Mambo aliyofanyiwa umeyaona?

Ameshindwa kuvumilia Hadi mwakani Kama alivyoahidiwa kiufupi wanawake wengine hawanaga shukrani kabisa
 
Sikushauri ufanye hiki ulichoandika hapa rafiki yangu,,

Demu hana akili na anaitaka ndoa kwa gharama yoyote,, kudeal na mtu aina hiyo itakutia hasara hata wewe kinamna fulani hivi.
Mara uchumba sugu, mara anampenda mara sijui famili inampenda B,, akili zake mavi mavi tu,,
 
Yap Kama chai hivi unajiuliza kwann ndani ya miaka hiyo minne asipate hata mtoto??

Hata hiyo reaction ya wazazi wake ya kutokumkubali kabisa jamaa na kumruhusu mtoto abadili na dini juu [emoji1][emoji1787]

Halafu hao wazazi hawakumuonya jamaa kuhusu kukaa mda mrefu bila kumuoa mtt wao ?? Kwamba walimpa jamaa kimya kimya ?

Hii kweli yaweza kua ni chai na karoti [emoji1787][emoji1787]
 
Liverpool VPN huwa mna mdharau sana

Yule jamaa ana hoja ya msingi anaposema MSIOE mtafute hela kwanza

Bila shaka hapo HELA ndio chanzo cha yote
Sidhani,
Maana Dogo kuumri Ni mdogo , ila KIUCHUMI katupiga gepu kubwa wote.

Huo ndo uhalisia mkuu
 
Pole yake. Speaking from experience; kijana anapitia kipindi kigumu sana! Ninalitambua hilo kwa kuwa nimewahi kupitia Scenerio kama hiyo miezi kadhaa iliyopita.
Kitu pekee ambacho mhanga anatakiwa kufahamu ni kuwa, yeye hajafeli! Bali mahusiano yao ndio yaliyofeli na kutokufikia malengo.
Hata hivyo, anatakiwa ajichanganye sana, asikae mwenyewe muda mrefu.
Pia, utetezi unaotolewa na huyo Bibie ni wa uongo tu! Speaking from experience.
Kwa sasa hakuna kitakachomponya zaidi ya muda. Akubali kuumia na apumzike kwanza.
I know ni vigumu sana but kama alizaliwa mwanaume aelewe kuwa, hayo maumivu yanamhusu mwenyewe na kwa mara ya kwanza atagundua kuwa, hakuna mtu wa kumsaidia maumivu hayo.
Akishapita hiki kipindi, anitafute nimpe mbinu mpya za kijasusi za kudeal na hawa viumbe waliojawa na ubinafsi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ubabaishaji kivipi wkt mwakani ndo jamaa alikua kapanga kuvuta jiko.

Mwanamke hakua TU mvumilivu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…