Jamaa anasema Zanzibar ilikuwa inamiliki ukanda wa Pwani

Jamaa anasema Zanzibar ilikuwa inamiliki ukanda wa Pwani

kuna mbuzi moja inaongea itv sasaivi anasema ukanda wa pwani ilikuwa mali ya zanzibar, bila kujua kuwa sulatan aliuza kwa wajerumani, hadi visiwa vya Mafia vikauzwa kwa mjerumani yeye akabaki na visiwa vile wanavyomiliki sasaivi wazenji tu. jamaa ana sura ya kiarabu fulani hivi. kama kuongea muungano waongee tu ila waache kuleta sera za uongo kwamba kuna maeneo bara ni ya kizazibar.
Mkuu kila mtu ana haki ya kusema yamfurahishayo. Yeye kasema yake ITV na wewe umesema yako Jamiiforum ngoma draw and thread closed.
 
kuna mbuzi moja inaongea itv sasaivi anasema ukanda wa pwani ilikuwa mali ya zanzibar, bila kujua kuwa sulatan aliuza kwa wajerumani, hadi visiwa vya Mafia vikauzwa kwa mjerumani yeye akabaki na visiwa vile wanavyomiliki sasaivi wazenji tu. jamaa ana sura ya kiarabu fulani hivi. kama kuongea muungano waongee tu ila waache kuleta sera za uongo kwamba kuna maeneo bara ni ya kizazibar.
Dawa yao ni kuwafanya wilaya ya mkoa wa Pwani
 
Hao kweli ni mbuzi.Hata kama muungano ukifa lakini haitatokea hiyo ndoto ya kuchukua pwani
 
Kuna mbuzi moja inaongea ITV sasa hivi anasema ukanda wa Pwani ilikuwa mali ya Zanzibar, bila kujua kuwa Sulatan aliuza kwa wajerumani, hadi visiwa vya Mafia vikauzwa kwa mjerumani yeye akabaki na visiwa vile wanavyomiliki sasa hivi wazenji tu.

Jamaa ana sura ya kiarabu fulani hivi, kama kuongea muungano waongee tu ila waache kuleta sera za uongo kwamba kuna maeneo bara ni ya kizazibar.
Vipi hakutaja karne gani hiyo? Sikumsikia, ila pia sitaki kuamini kuwa hakuwa na weledi wa kutanabaisha kipindi au muda ili kuepuka sintofahamu.
Maana pwani, kuanzia Mombasa mpaka chini kusini huko , kuna kipindi ilikuwa chini ya Sultani.
 
Yaani ukitaka kuangalia yaliyomo kwenye Heligoland Treaty ya 1890 inahusisha Malawi, Zanzibar kisiwa cha Heligoland kilichopo karibu na Germany ambacho kilikuwa mali ya Denmark kabla Uingereza haijakimiliki. Haya mambo yabaki kama yalivyo. You can't UNDO them
hii ni sehemu ya historia tu hakuna aliyekuwepo wakati huo. Ni kama fundisho tu hakuna aliyesema 'undoing things'
 
Sio Pwani ya kwetu tu ni kuanzia pemba mozambique mpaka huko somalia ilikuwa inaitwa zanzibar kwa ujumla
Hata ingekuwa kweli kwanini tuendelee kutetea mipaka waliyoweka wakoloni na kabla ya wakoloni ilikuwa inamilikiwa na nani?
 
Kuna mbuzi moja inaongea ITV sasa hivi anasema ukanda wa Pwani ilikuwa mali ya Zanzibar, bila kujua kuwa Sulatan aliuza kwa wajerumani, hadi visiwa vya Mafia vikauzwa kwa mjerumani yeye akabaki na visiwa vile wanavyomiliki sasa hivi wazenji tu.

Jamaa ana sura ya kiarabu fulani hivi, kama kuongea muungano waongee tu ila waache kuleta sera za uongo kwamba kuna maeneo bara ni ya kizazibar.
halafu unaona fahari kuita mwenzako mbuzi, wewe uitwe mnyama gani?

Hata ustaarabu huna, kama hujui historia si utulie tu ujifunze kwa ustaarabu.
 
Mambo mengine yanachekesha sana, yani Mwarabu atoke zake huko Oman aje kutua Zanzibar kisha auze ardhi ya Wandengereko, Wazaramo, Wasukuma, Wachaga, Wapogoro n.k kwa Wajerumani halafu watu watilie maanani upumbavu kama huo.
 
Hata ingekuwa kweli kwanini tuendelee kutetea mipaka waliyoweka wakoloni na kabla ya wakoloni ilikuwa inamilikiwa na nani?
hiyo ilikuwa kabla ya berlin conference, hence mipaka ya wakoloni
 
Kwahio ?

Hata (Tanzania, Rwanda na Burundi za Sasa) kuna kipindi fedhuli Mjerumani alijilimilikisha..., but that's neither here nor there....
 
Mambo mengine yanachekesha sana, yani Mwarabu atoke zake huko Oman aje kutua Zanzibar kisha auze ardhi ya Wandengereko, Wazaramo, Wasukuma, Wachaga, Wapogoro n.k kwa Wajerumani halafu watu watilie maanani upumbavu kama huo.
Hata ingekuwa kweli kwanini tuendelee kutetea mipaka waliyoweka wakoloni na kabla ya wakoloni ilikuwa inamilikiwa na nani?
Hehehe ila aliyeuza alivitoa wapi, maana Mwarabu Sultan sio Mbantu, yeye katokea huko Uarabuni na kuja kuuza ardhi ya watu aliyoikuta.
Technically na wao Waliuziwa, historia ipo ila watu wanai ignore na kufuata tu Utashi wao.

Ukisoma Historia ya Kilwa utaelewa mengi tu.

Zamani maeneo mengi haya yalikua Mapori tu, Kuna watu wakaanzisha Empire zao mfano Mzuri ni Kilwa ambayo ilikuwepo ukanda wa Pwani kiongozi wake akiwa ni Almuli,

Wakati huo huko Persia (Iran ya sasa) kulikua na mwana Mfalme ambaye mama yake alikua mtumwa toka Africa Alishindwa kinyang'anyiro cha kua Mfalme akaja Kilwa akainunua kwa Almuli,

Utawala ukadumu miaka kadhaa baadae akaja akauziwa Mu oman, nae Utawala ukadumu mpaka Portugal alipovamia huu Ukanda, Portugal akakaa kwa muda baadae Oman akampiga Portugal na kuendelea kumiliki hadi mambo ya Ukoloni yalipokuja.

Hivyo ilikua kawaida watu kuuziana ardhi na hao Wanaopondwa ndio walionyanyua makabila mengi Tanzania, makabila yanayosifika sasa hivi kama Wachaga, Wahaya, matajiri Wa pwani etc Historia yao ina link na historia hii.

Brief history ya kilwa
 
Back
Top Bottom