Jamaa anasema Zanzibar ilikuwa inamiliki ukanda wa Pwani

Mkuu kila mtu ana haki ya kusema yamfurahishayo. Yeye kasema yake ITV na wewe umesema yako Jamiiforum ngoma draw and thread closed.
 
Dawa yao ni kuwafanya wilaya ya mkoa wa Pwani
 
Hao kweli ni mbuzi.Hata kama muungano ukifa lakini haitatokea hiyo ndoto ya kuchukua pwani
 
Vipi hakutaja karne gani hiyo? Sikumsikia, ila pia sitaki kuamini kuwa hakuwa na weledi wa kutanabaisha kipindi au muda ili kuepuka sintofahamu.
Maana pwani, kuanzia Mombasa mpaka chini kusini huko , kuna kipindi ilikuwa chini ya Sultani.
 
hii ni sehemu ya historia tu hakuna aliyekuwepo wakati huo. Ni kama fundisho tu hakuna aliyesema 'undoing things'
 
Sio Pwani ya kwetu tu ni kuanzia pemba mozambique mpaka huko somalia ilikuwa inaitwa zanzibar kwa ujumla
Hata ingekuwa kweli kwanini tuendelee kutetea mipaka waliyoweka wakoloni na kabla ya wakoloni ilikuwa inamilikiwa na nani?
 
halafu unaona fahari kuita mwenzako mbuzi, wewe uitwe mnyama gani?

Hata ustaarabu huna, kama hujui historia si utulie tu ujifunze kwa ustaarabu.
 
Mambo mengine yanachekesha sana, yani Mwarabu atoke zake huko Oman aje kutua Zanzibar kisha auze ardhi ya Wandengereko, Wazaramo, Wasukuma, Wachaga, Wapogoro n.k kwa Wajerumani halafu watu watilie maanani upumbavu kama huo.
 
Hata ingekuwa kweli kwanini tuendelee kutetea mipaka waliyoweka wakoloni na kabla ya wakoloni ilikuwa inamilikiwa na nani?
hiyo ilikuwa kabla ya berlin conference, hence mipaka ya wakoloni
 
Kwahio ?

Hata (Tanzania, Rwanda na Burundi za Sasa) kuna kipindi fedhuli Mjerumani alijilimilikisha..., but that's neither here nor there....
 
Mambo mengine yanachekesha sana, yani Mwarabu atoke zake huko Oman aje kutua Zanzibar kisha auze ardhi ya Wandengereko, Wazaramo, Wasukuma, Wachaga, Wapogoro n.k kwa Wajerumani halafu watu watilie maanani upumbavu kama huo.
Hata ingekuwa kweli kwanini tuendelee kutetea mipaka waliyoweka wakoloni na kabla ya wakoloni ilikuwa inamilikiwa na nani?
Hehehe ila aliyeuza alivitoa wapi, maana Mwarabu Sultan sio Mbantu, yeye katokea huko Uarabuni na kuja kuuza ardhi ya watu aliyoikuta.
Technically na wao Waliuziwa, historia ipo ila watu wanai ignore na kufuata tu Utashi wao.

Ukisoma Historia ya Kilwa utaelewa mengi tu.

Zamani maeneo mengi haya yalikua Mapori tu, Kuna watu wakaanzisha Empire zao mfano Mzuri ni Kilwa ambayo ilikuwepo ukanda wa Pwani kiongozi wake akiwa ni Almuli,

Wakati huo huko Persia (Iran ya sasa) kulikua na mwana Mfalme ambaye mama yake alikua mtumwa toka Africa Alishindwa kinyang'anyiro cha kua Mfalme akaja Kilwa akainunua kwa Almuli,

Utawala ukadumu miaka kadhaa baadae akaja akauziwa Mu oman, nae Utawala ukadumu mpaka Portugal alipovamia huu Ukanda, Portugal akakaa kwa muda baadae Oman akampiga Portugal na kuendelea kumiliki hadi mambo ya Ukoloni yalipokuja.

Hivyo ilikua kawaida watu kuuziana ardhi na hao Wanaopondwa ndio walionyanyua makabila mengi Tanzania, makabila yanayosifika sasa hivi kama Wachaga, Wahaya, matajiri Wa pwani etc Historia yao ina link na historia hii.

Brief history ya kilwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…