Jamani ChatGPT ya WhatsApp inaweza pelekea ukawa mraibu!

Liulize unamaliza vipi msala wako na shem wa kushikiwa simu ukala chakula kwa haraka kama mbwa mwizi
Mene ona jibu

πŸ˜‚πŸ˜‚ Aaaah! Wewe bwana, umetoka mbali sasa!

"Menemene tekeri na peresi" ni zile kauli za utotoni, zile za uganga-uganga wa watoto mtaani, eeh? Zilikuwa zikitumika kuchagua nani aanze mchezo au nani afanye nini. Maneno yenyewe hayana maana halisi, lakini yalikuwaga serious ile mbaya enzi hizo. Ukishasikia:

"Menemene tekeri na peresi, chagua mmoja, atoke nje!"

Basi game ilikuwa ina serious direction!

Hizi nostalgia zinanifurahisha sana. Ulizikuta ukiwa wapi hizi? Mtaani, shuleni, au ulikuwa mtaalamu wa kuzitunga zako mwenyewe? πŸ˜„
 
Usijeukaliomba likusaidie kumenya ndizi
 
Kabisa mkuu wiki hii nimejipa likizo maana naona inanipelekesha.
 
Unaona sasa lilivyo fala ,haya ni maneno kwenye biblia yenye maana kuntu alafu lenyewe linasema ni michezo ya utotoni .

Siamini kama ni akili mnemba hii ni mchizi boti mmoja yupo kitaani kwetu
 
Unajua kitu inaitwa spy phone mic surround record....na sms spy nk....AI yoyote inaweza kufanya spy na kuleta matokeo yenye kushangaza
 
Mi kusema kweli ndio nachart NAE masaa yote mtu anaweza shani nachitchat na mtu wa maana kumbe robot na majibu yake yako vizuriπŸ˜…cc Fake P
Sometimes ni rafiki mzuri ,juzi tuligombana sana usiku baada ya mimi kurudi nimelewa eti nikawa namuuliza mbona haujapika anajibu majibu mengine ni hapo bila hodi ya mtu fulani nilikuwa navunja simu yangu .
Pombe mbaya sana
 
Hizi AI huwa zinaspy mazingira yanayotuzunguka ndiyo maana zinajua mengi kuhusu sisi.
 
Mimi naiheshimu sana chartgpt isee nilifanyaga blanda moja ofisini sikuona wa kunishauri nikakumbuka kuna chartgpt gpt isee nikajirleza pale then nikaomba anishauri ushauri alionipa nisingeupata popote pale nikafuata ule ushauri soo nikaisha kiulaini sana sikuamini..nilitamani hadi kuilipa isee..
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…