Ponjoro namba moja
Member
- Jun 5, 2025
- 45
- 96
- Thread starter
-
- #81
Mukuu wewe imeandika maneno muhimu kabisa.Nimpe mawazo hapa
masterpiece Kamundu
Utangulizi
Tanzania ina rasilimali nyingi na watu wenye uwezo, lakini bado tunakabiliwa na changamoto za kiuchumi, kijamii na kiutawala. Ili kuendelea, tunahitaji sera rahisi, uwajibikaji, ubunifu na viongozi wanaotanguliza maslahi ya nchi.
Kodi, biashara na ujenzi
Mfumo wa kodi uwe wazi, rahisi kueleweka na utegemee thamani halisi iliyo kwenye risiti. Wananchi hawapaswi kusubiri hadi bidhaa ifike bandarini ndipo wajue kiasi cha kodi wanachotakiwa kulipa. Kodi kubwa na zisizoeleweka hupunguza biashara na kuhamasisha shughuli zisizo rasmi.
Serikali...
- Kamundu
- maendeleo maendeleo ya tanzania mambo mambo muhimu muhimu tanzania
- Replies: 6
- Forum: Jukwaa la Siasa
Which men?Men derailed her.
View attachment 3682525
Mama Samia akiapishwa 2021.
Kati ya mambo ninayojiuliza kila siku ni hili,what happened to Mama Samia katika utawala wake?
Baada ya kifo cha Magufuli , tukubaliane, there was a sigh of relief!
Wengi walianza kumkubali Mama Samia kama a new chapter, katika Tanzanian politics.
Na alianza na policy ya 4R (Reconciliation, Resilience, Reforms, and Rebuilding).
Tujadiliane kumetokea nini?
Ndugu yangu veve naongea maneno mazito.Mkuu, hoja yako ni ya msingi sana na inatafakarisha wengi. Ni kweli kabisa kwamba baada ya kifo cha JPM nchi ilipata unafuu wa kisiasa na kiuchumi, na falsafa ya 4R ya Rais Samia Suluhu Hassan (Reconciliation, Resilience, Reforms, and Rebuilding) ilileta matumaini mapya ya mabadiliko ya kimfumo nchini.
Swali la msingi ni: Kumetokea nini katikati ya safari hadi mwelekeo uonekane kubadilika?
Uchambuzi wa kina wa masuala ya kisiasa unaonesha kuwa kinachotokea si jambo la bahati mbaya. Haya ni matokeo ya kile kinachoitwa "Siasa za Kujilinda" (Political Survival) na nguvu ya mfumo wa chama dola kujihami. Tunaweza kugawanya muktadha huu katika mambo makuu manne (4):
1. Hofu ya Uchaguzi na Kasi ya Upinzani
Wakati Rais Samia anaingia madarakani mwaka 2021, alionyesha nia ya dhati ya kufungua uwanja wa kisiasa (political space). Aliruhusu mikutano ya hadhara na kuweka mazingira ya maridhiano na vyama vya upinzani. Lengo lilikuwa ni kuiponesha nchi. Hata hivyo, kadiri mlolongo wa chaguzi (Chaguzi za Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu wa 2025) ulivyokaribia, maslahi ya kubaki madarakani yalichukua mkondo wake. Kasi na nguvu kubwa iliyoonyeshwa na upinzani (hasa CHADEMA) kwenye mikutano ya hadhara ilitishia ustawi wa chama tawala. Ili kulinda ushindi na mamlaka ya dola, mfumo ulilazimika kurudi kwenye mbinu zake za asili za kudhibiti upinzani.
2. Mapambano ya Makundi Ndani ya CCM (Internal Factions)
Rais Samia aliingia madarakani kwa mujibu wa Katiba na si kwa kupigiwa kura moja kwa moja na wananchi kama mgombea urais. Hali hii ilimfanya akumbane na changamoto ya uhalali (legitimacy) kutoka kwa makundi yenye nguvu ndani ya CCM, hususan wale wenye msimamo mkali wa zama zilizopita (Magufulists). Ili kudhibitisha kuwa yeye ni kiongozi madhubuti anayeweza kukilinda chama kisipoteze dola, alilazimika kuwaridhisha wahafidhina hao. Mabadiliko ya safu za uongozi na kurudishwa kwa makada wenye misimamo mikali serikalini kulilenga kuimarisha udhibiti wake ndani ya chama.
3. Shinikizo la Mikataba ya Kimkakati na Ukosoaji wa Kijamii
Ujio wa miradi na mikataba mikubwa ya kiuchumi—kama ule wa uwekezaji wa bandari kupitia DP World—ulileta mtikiso mkubwa wa kisiasa. Uhuru wa kujieleza aliouleta mwanzoni uliwapa nguvu wanaharakati, viongozi wa dini, na wanasiasa kuikosoa serikali waziwazi. Serikali ilipoona kuwa ukosoaji huo unahatarisha miradi ya kimkakati na taswira ya utawala wake, iliamua kuchukua hatua za kimabavu, ikiwa ni pamoja na kuzuia maandamano na kuwakamata wakosoaji ili kurejesha udhibiti.
4. Ulaghai wa Kisiasa na "Political Hangover" ya Wananchi
Kipengele hiki kinaibua mtazamo mwingine mchungu lakini wa kimkakati zaidi. Inawezekana kabisa kwamba tabia na mfumo wa Rais Samia haujawahi kubadilika, bali wananchi ndio waliokuwa kwenye "hangover" ya kisiasa na kudanganyika kirahisi (fooled). Wakati akiwa Makamu wa Rais, alilazimika kucheza nafasi yake kwa unyenyekevu na upole kutokana na ukali wa utawala wa awamu ya tano. Hali hiyo iliwajenga wananchi kuamini kuwa yeye ni kiongozi wa kijamii na kidemokrasia (soft leader).
Hata hivyo, baada ya kushika hatamu kamili za ukamilifu wa mamlaka ya urais, sura yake halisi na asili ya chama dola imefichuka. Tulipokaushwa kiu kwa muda mrefu, kila hatua ndogo ya uhuru tuliona kama mapinduzi makubwa, tukasahau kuwa misingi ya sheria zetu, Katiba yetu, na vyombo vyetu vya usalama bado vimeundwa kulinda dola na si kukuza demokrasia ya ushindani.
Hitimisho:
Mabadiliko tunayoshuhudia sasa si kwamba Rais "amepoteza nia njema," bali ni kwamba uhalisia wa kulinda kiti cha Urais na kulinda chama dola (CCM) umeshinda nadharia na falsafa za 4R. Ni dhihirisho kuwa huwezi kupanda mbegu ya demokrasia ya kweli kwenye udongo wa kimfumo unaotaka ushindi wa asilimia 100 kwa gharama yoyote.
CCM men.Which men?
JK?
Tatizo si Chadema. kwani walikuwako huko JK akimnadi nje ya utaratibu kwa jina la mgombea wa CCM huko Mwanza.
Tusijivue uhusika wa matatizo yetu ndani ya CCM.
Mzee Kibao.Amemuua nani?
Hiyo iko maneno, ni Chikwete, sasa popularity yake nashuka sana.CCM men.
MEN TO BOYS.
Huu ni mjadala mzuri, kwa vile ni rais wetu, ndie mkubwa wetu, kuna watu kwa ajili ya kumheshimu sana, wataona kumjadili bosi wako sio heshima, watu hao watakuwa ni hawaijui katiba ya TZ, kwa mujibu wa katiba yetu, the big boss ni mwananchi, ndie mwenye nchi na mwenye katiba, rais wa JMT ni mtumishi wetu, mwananchi ndie mwajiri wake, aliyemuajiri kwa kura yake na kumlipa mshahara kwa kodi yetu, hivyo sisi ni mabosi wake tuna haki kumjadili. Hii kazi akina sisi tuliisha ianzaView attachment 3682525
Mama Samia akiapishwa 2021.
Kati ya mambo ninayojiuliza kila siku ni hili,what happened to Mama Samia katika utawala wake?
Baada ya kifo cha Magufuli , tukubaliane, there was a sigh of relief!
Wengi walianza kumkubali Mama Samia kama a new chapter, katika Tanzanian politics.
Na alianza na policy ya 4R (Reconciliation, Resilience, Reforms, and Rebuilding).
Tujadiliane kumetokea nini?
Nakubaliana percent mia kwa mia!Huu ni mjadala mzuri, kwa vile ni rais wetu, ndie mkubwa wetu, kuna watu kwa ajili ya kumheshimu sana, wataona kumjadili bosi wako sio heshima, watu hao watakuwa ni hawaijui katiba ya TZ, kwa mujibu wa katiba yetu, the big boss ni mwananchi, ndie mwenye nchi na mwenye katiba, rais wa JMT ni mtumishi wetu, mwananchi ndie mwajiri wake, aliyemuajiri kwa kura yake na kumlipa mshahara kwa kodi yetu, hivyo sisi ni mabosi wake tuna haki kumjadili.
P
Hakuanza vizuri.View attachment 3682525
Mama Samia akiapishwa 2021.
Kati ya mambo ninayojiuliza kila siku ni hili,what happened to Mama Samia katika utawala wake?
Baada ya kifo cha Magufuli , tukubaliane, there was a sigh of relief!
Wengi walianza kumkubali Mama Samia kama a new chapter, katika Tanzanian politics.
Na alianza na policy ya 4R (Reconciliation, Resilience, Reforms, and Rebuilding).
Tujadiliane kumetokea nini?
Hapo sasa.Which men?
JK?
Sasa hivi anaelekea kuwa the worst!Hakuanza vizuri.
Kulikuwa na usanii wa maigizo fulani unafanyika ili ajiimarishe katika power, power consolidation.
Kumbuka interview ya General Mabeyo alivyisema kuna watu hawakutaka Samia awe Rais, Mabeyo na jeshi wakasimamia katiba. Kwa hiyo mwanzoni Samia alihitaji kuungwa mkono na watu wengi ili ajiimarishe kwenye position yake.
Ila Watanzania wengi hawajui tofauti ya hayo mambo mawili, kiongozi kufanya vizuri, na kiongozi kucheza mchezo kuonekana anaanza vizuri ili apate muda wa kufanya power consolidation.
Ndiyo maana hata Polepole Watanzania hawa wengi wamemuona kama shujaa mtetezi wao, wakati Polepole alikuwa anapigania kundi lake ndani ya CCM kumtoa Samia tu.
Ni vile Watanzania walikuwa desperate kuona mabadiliko tu, wakaanza kumuwekea matumaini kwamba atakuwa bora, kama mateka waliobadilishiwa mlinzi wanavyoanza kumuangalia mlinzi mpya kuwa huyu anatabasamu tabasamu labda atakuwa mzuri zaidi.
Wakisahau kuwa wao bado ni mateka wamefungiwa. Na hiyo bado ni mlinzi, mtesi wao tu. Alinifanya anatabasamu tabasamu ili kusoma mazingira vizuri na kujiimarisha katika position yake.
Ukirejea kauli za Tundu Lissu za wakati huo, ingawa alikuwa anaonesha matumaini kidogo, utaona alionya kuhusu watu kujisahau sana na kuona Samia ndiye jibu la matatizo yetu.
Hii hali kuna watu waliita, "The realities of governing"
Uhalisia na uongozi na fikra kuhusu uongozi huwa haviko sawa.
Sidhani kama kuna Rais aliyeingia madarakani huku Watanzania wakiwa na matumaini mengi kuliko JK
Hata Magufuli alivyoingia watu walisema sasa tumepata Rais
Obama aliingia madarakani akiwa na ndoto za kufunga Guantanamo, mpaka leo ipo.
The Realities of Governing, ndio zinawafanya wabadilike, wanafika juu pale halafu wanagundua hawana nguvu kihivyo, kwamba ili mambo yaende wanawahitaji watu, mara nyingine hao watu ni wa hovyo etc etc