Jamani naombeni msaada wenu, mke wangu katapelewi Magufuli stand

Sijui akili Iko wapi mke unamuacha akakate tiketi mwenyewe, asafiri mwenyewe kimasihara ikitokea uje uombe ushauri, yaan angalau ungeenda ukamkatie na kumpandisha gar lkn wapi aisee ovyo kabisa, magar ya nyumbani kwenu hamuyajui?
Yaani mimi niko South nije nimkatie mke tiketi Magufuli? Au naota ndoto
 
Mheshimishe mkeo kwa watu. Hata kama ni mjinga, wewe usiwe mtu wa kumwita mjinga hadharani.
 
Kumbe dini inaruhusu nuchukue tu mkuu jioni ya leo watu wale chai na kalmat
Naona hujanielewa vizuri wake zetu wako ndani ya Vilakazi street wamevaa mabaibui na majuba wanasambaza mzigo halafu kesho nije nimpige chini haitakuja kutokea
Maana hivyo ni viapo zaidi ya damu,ogopa maisha ya mbogo akiwa ndani ya South Africa
 
Ni utapeli tu wa kijinga wa baadhi ya Watanzania hasa kwenye sekta ya usafiri na uzembe wa usimamizi wa serikali,hivi kuna maana gani stand ya mabasi kuwa na watu wamejaa hawana kazi?
Mbona inchi nyingine huo ujinga hamna,yaani mimi nimeamka nyumbani naenda Songea na kunamabasi ya songea halafu kuna mtu kati wa kunionyesha hasi la Songea?hao ni wezi kama wezi wengine
 
Yaani mimi niko South nije nimkatie mke tiketi Magufuli? Au naota ndoto
Mtu akikujibu ufikir kwanza kabla ya kuanza kumjib, unapokua na familia Lazima Kuna masuala fulan Lazima ufanye wewe au Kuna mtu unayemwamini anaweza fanya, mfano wewe haupo familia inasafir ungetafta mtu au uwe na mtu unayemjua stend atafanya kazi hiyo, au ndugu kifupi ulichukulia ni kitu kidogo nd shida imeanzia hapo.
 
Unajua wapiga debe kawaambia anaenda Songea wakamkatie tiketi ya kwenda Kyela na hayuko peke yake yuko na abilia mwenye tatizo kama lake,na kumbuka Songea nauli 64,000 wakati Kyele 76,000
Kwahiyo yeye katapeliwa pesa na siyo safari kama alitakiwa kulipia 64,000 kwenda Songea yeye akalipia 76,000 hapo inaonekana bado atasafiri kwa tickets hio hio tu lakini atakua katumia pesa zaidi ya bei halisi.
 
Huyu mke wako anashiida kwanini akubali kunyang'anywa ticket na Kwanini asitoe taarifa polisi baada ya kuona kanyang'anywa ticketing au huyo Mke wako anaonekana anafanya mambo bila kukushirikisha yeye ana fanya jambo badae anakupa taarifa tu.
 
Nilikua naskia tu wanasema kosea kila kitu lakini sio kuoa. Leo ndo nimejua.
Kweli Mimi kuoa Mwanamke mwenye uelewa mdogo sitafanya ujinga huo, na Mwanamke anakua muelewa na mjanja kutokana na jinsi ya Mume wake alivyo.
 
 

Huyu mke wako anashiida kwanini akubali kunyang'anywa ticket na Kwanini asitoe taarifa polisi baada ya kuona kanyang'anywa ticketing au huyo Mke wako anaonekana anafanya mambo bila kukushirikisha yeye ana fanya jambo badae anakupa taarifa tu.
Yaani naweza kusema ni uoga fulani ambao huwa wanakuwa nao wanawake,
Hakuwa peke yake alikuwa na abilia mwingine aliyefanyiwa huo utapeli,kwa hiyo walikuwa wanashilikiana maamuzi ya kiuoga,maana niliwambiwa mkifika Chalinze,Morogoro,Mikumi,Ruaha Mbuyu au Iringa Check point mripoti polisi,jibu walilokuwa wananipa wamesama watatupeleka Songea,Mwisho wa siku walipandishwa Costa makambako na nauli hawakuludishiwa iliyozidi
Maana yake mpiga debe ndiye aliyekula cha juu cha kwenye nauli akaenda kuwakabidhi kwenye basi bovu la kyela ambalao halina umaalufu wa kupata abiria,inamaana ni utapeli wanaoshirikiana na wenye mabasi
Kilichotokea wakati yeye yuko makambako saa 5:30 asubuhi Mabasi ya Songea mda huo huwa wanakuwa wamepita Njombe,
Mabasi yaliingia saa 4 asubuhi Songea yeye akajikuta anaingia saa 7 mchana tena kwa nauli ya alfu 76 wakati nauli halisi alfu 64,
 

Kweli Mimi kuoa Mwanamke mwenye uelewa mdogo sitafanya ujinga huo, na Mwanamke anakua muelewa na mjanja kutokana na jinsi ya Mume wake alivyo.
Hao wajanja mara nyingi ndoa zao hazifiki mwisho heli sisi tuliyoowa hawa mafala
 
Zipo kwa ajili ya kuangalia X mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…